Ni mchekeshaji gani wa Kibongo huwa hakuchekeshi kabisa?

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Chalalamila huwa hanichekeshi kabisa. Ingawa watu wengi wanasema anachekesha.
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh Chalalamila huwa hanichekeshi kabisa. Ingawa watu wengi wanasema anachekesha.
Sema hapa huyu kibushuti samia alinichekesha sana
 

Attachments

  • Duh kiongozi kama huyu mchapa kazi kumpata tena ni mitano tena 🫣.mp4
    947.9 KB
  • AQNL9KwvgNwOGe3X7iWw35pDYtTgm3PmnnSAtZlH282vFEEJ_TPg63tAkGfJAtwjxiJiImeK_MRsNkKaZyISS6Q3J_m1zj...mp4
    1.1 MB
Leonard anachekesha bila kumsahau Joti, wengine wanalazimisha kazi za watu.
 
Kwani Wew hauwez kucheka mwenyewe mpaka uchekeshwe??
 
Mwangalie Brother K uvunjike mbavu
 
Chalie champion mchekeshaji wa muda wote Hawa wa kisasa hakun kitu
 
Siku hizi kuna Mwadawa wa Kombolela usipocheka upelekwe ukachekiwe mfumo wa kucheka una shida gani... Haua wajuaji utawasikia unaangaliaje Kombolela haya karibuni[emoji41]
 
Labda ni vile maisha yanakimbiza watu mchakamchaka. Ila akili ikitulia kila mtu anachekesha
 
Mie na Uzee huu nikiwaza tozo na hili deni la Taifa hata wangekuja wachekeshaji wote siwezi kucheka labda nikiwaangalia na vile wengi ni machawa ntaishia kulia tu
 
Me naangalia comedy za kenya na Nigeria zaidi.
Hapa bongo walau joti na brother k wanajitahidi.
 
Me nikiwa na hela kila mchekeshaji naona anachekesha ila nikiwa sina hela wote naona hawachekeshi labda marehem majuto
 
Jeymond asee huwa nawaza yule jamaa nani alimuambia kukata kata viuno na kale kazungu kake ndio hitaji la wabongo. Kila anapokuwa lazima akate kiuno.
 
Uchekeshaji ni sanaa kama utunzi na uimbaji wimbo. Upo wimbo unavutia na usiovutia pale kila msikilizaji anaposikiliza. Ndio maana kila mtu hucheka kwa hisia zake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…