Ni Mchezaji gani wa Taifa Stars alikuvutia kwenye mchezo wao na Algeria jana?

Ila Tanzania tuna uzalendo wa kijinga sana uliojaa ubinafsi.

Kuna mchambuzi anasema Novatus ndiyo man of the match kwa kuwa amepata 7.5 kwenye mtandao mmoja wa kutoa takwimu za wachezaji ila hapo hapo anaonyesha wachezaji 3 wa Algeria nao wana 7.5. Na hapo amelibeba hilo kwa sababu huyo Novatus kapitia njia zake. Watu wanamkumbusha mpira tumeangalia wote kuna ambao wanaonekana walikuwa bora zaidi.
 

Fotmob wamempa Novatus man of the match, sofascore pia, AI score pia, kwa hio nadhani alikuwa sahihi
 
View attachment 2743166
Fotmob wamempa Novatus man of the match, sofascore pia, AI score pia, kwa hio nadhani alikuwa sahihi
Labda kwa upande wa Tanzania ndiyo anawazidi wenzake ila pia kuna mtandao wamempa rating kubwa zaidi Msuva, Mzamiru na Boko ambaye amecheza kwa dakika 1 na wote wamemzidi Novatus na rating ya chini kabisa ya mchezaji wa Algeria ni kubwa kuliko ya mchezaji mwenye rating kubwa wa Tanzania
 
Mbwana ally samatta na feisal salum wanajisikiaje kukosa mechi ya Jana.
Feisal hajawahi kufanya maajabu kimataifa iwe taifa staz, yanga na sasa azam hata hasipokuwepo hakuna pengo lolote. Kuhusu samata katubeba sana kipindi ambacho umri wake ulikua unaruhusu tatizo pro alikua peke yake ila kwa sasa umri ushamtupa mkono akiwa taifa staz lazima acheze kwa tahadhari kuepuka majeruhi ili kulinda kibarua chake ulaya. Hata angekua Cristiano Ronaldo asingeweza kutufikisha mbali peke yake kwaiyo Samata tumpe heshima yake.
 
Taja huo mtandao, tuujue, mana mitandao yenye kuheshimika wamempa Novatus
 
Heri umeona hili,
Watu wanamdharau Samata haraka sana na yote aliyotufanyia kama taifa
 
Taja huo mtandao, tuujue, mana mitandao yenye kuheshimika wamempa Novatus
Hizo ziko computer generated au wakati mwingine zinaweza kuwa biased na wapigaji kura wenyewe. Na kama kigezo ni rating nimekuonyesha hiyo hiyo FOTMOB wameonyesha wachezaji 3 wana rating sawa na Novatus.


 
Jana mchezaji mmoja tu wa Tanzania kacheza kuliko wote na ndiye ametuvusha hatuwa hii:

Mama Samia ndiye aliyeucheza mpira wa jana. Kacheza peke yake, tumpe mauwa yake.
Kiundani huenda ikawa ni kweli et😳
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…