Ni mchezo gani wa self defence ambazo zinafaa Kwa watu wazima?

Behind the camera

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2019
Posts
315
Reaction score
756
Nafikiri wakitajwa watu wazima watoke, nami naweza kutoka mbele. Miaka 30 sio mchezo aisee

OK TUYAACHE HAYO.

Aisee naomba ushauri kidogo katika suala la kupata elimu kidogo ya kujilinda binafsi walau unapopata dharura upate angalau upenyo wa kukimbia.

Kuna jamaa yangu mmoja (MJEDA) nilimuuliza kuhusu hili lakini alinizunguusha zunguusha mpaka akanipotezea. (Sasa sijui ndo Sheria haziruhusu au nnn?)

Nimekona nilete shauri langu huku,

Je?
Ni sanaa gani nzuri ya mapambano ambayo Kwa mtu mzima kama Mimi anaweza fundishwa na kupata angalau moja mbili.

KWANINI NIMEOMBA USHAURI JUU YA HILI?.

Aisee nimeshuhudia vijana wawili wenye mbavu nene baada ya kushiba bia na kuku, wakizichapa kavu kavu Kwa muda unaozidi dakika 5, Aisee nilihuzunika pale ambapo mmoja alibahatika kuwekwa roba mpaka almanusura kukata pumzi kama sio wasamaria wema kumuokoa.

Leo kwa mwenzako, kesho yaweza kuwa kwako. Kibano alichopewa jamaa kile laiti ningekuwa Mimi na haka kamwili kangu huenda ningepoteza maisha.


Nikaona kuna haja ya kujua chochote kuhusu kujilinda dhidi ya adui.


Na watu wenye miili myembamba wanaweza kupata mafunzo akaja akamkalisha mtu mwenye 6 park / mwili wa mazoezi??



Aisee naomba ushauri juu ya hili.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwanza si kila mjeda anajua mkono..wengine Ni maboya tu

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Reactions: rr4
Back to the thread.

Boxing+ krav maga utakuwa njema sana

Lakini punde, akakwingilia Jack Chan shashaaa
 
Inategemea na wepesi wa mwili wako na akili, michezo yote inakanuni zinazofanana ukakamavu, uvumilivu, wepesi wa mwili na akili (spiritual) na ubunifu.
Hakuna mchezo bora kuliko mwingine ila kuna mchezaji bora kuliko mwingine hivyo unaweza kuuchagua mchezo wowote na ukajifunza vizuri na ukawa hodari bila kujali umri.
Nacheza boxing nikaanza kuvutiwa na Kick boxing, taekwondo, shotokan ila boxing naipenda sana punch zake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemuelewa Sana ndugu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ingia YouTube sachi self defense techniques utapata za kutosha yaani mtu akirusha teke unamkalisha vipi akirusha ngumi pia unamkalisha vipi
Kingine kama wewe mwembamba ukipigana na mtu mwenye mbavu hakikisha hakushiki inakubidi upigane kama unakimbia kimbia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…