Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Man utd vs bayern UCL fainal



Man utd vs Newcastle January 2008
 
1.ufaransa Vs senegal fainali za kombe la dunia 2002 ilikuwa mechi ya ufunguzi,, Ufaransa alipigwa 1-0 huku zidane akiwa benchi na huo ukawa mwanzo mbaya wa mabigwa hao watetezi wa kombe la dunia 1998 kwan hawakuweza hata kwenda 16 bora

2.uruguay Vs ghana robo fainali ya kombe la dunia south Afrika,, Ghana walipata penalti ambayo Waafrika tukiamini Gyan angefunga penalti hyo,,, cha ajabu akakosa,,, na Ghana tukatolewa
 
hii game siwezi isahau.. bonge ya game kwa nusu fainali za world cup zote nilizowai kuona ikifuatiwa na holland vs brazil 1998.... game ipo extra time ila watu wana spidi timu zote kama game inaanza vile.... hakuna.kujiungausha wala kuomba omba mwenzako apewe kadi... anaanguka mchezaj wa ujeruman ananyanyuliwa na mchezaji wa italy huku wanacheka... na game inaendelea..

enzu hizo babu pirlo ni kijana katikati.. huku germany nao ballack kijana kati kati

wachambuzi wanasema fifa wana irank ile game kwenye training za ma refereee.... game kubwa ichezwe kwa sportmanship na iwe kaliiii..

philip lahm anakwambia ile ndio game kali aliyowai kucheza.. hadi mabek mnafunguka mnashambulia kisha mnageuza mnarudi kuzuia.. shot on goals kibaoooo

Germany 0-2 Itary semi final world cup 2006 mpira mwingi ulichezwaaa aseee goli safi kabisa la Grosso kwenye Extra tym..katikati pale Pirlo na Barrack yani siwez kusahau.
 
Uruguay vs Ghana, Kombe la dunia Suarez alizuia mkwaju uliokuwa unaenda golini kwa mkono
 
Juventus 1 Inter Milan 0, Mechi ya pili Series A 1998, mbio za ubingwa. Mechi hii ilikuwa na kasi kubwa sana. Ronaldo Lima akiwa kwenye ubora na Del Piero akiwa kwenye ubora wake. Ufundi wa magolikipa Angelo Peruzi na Gianluca Pagliuca ulikuwa kivutio sana.

Iyo mechi hapana chezea. Del Piero, Davids, Conte, Zidane, Inzaghi, Montero, Dilivio. Ronaldo, Diego Simone, Zamorano, Zanetti, moriera. Ilikua ni zaidi ya vita va dunia jinsi uwanja ulivotimuliwa vumbi.

Laizmen alijisahau akijaikuta katikati ya uwanja huku mpira ukiendelea.
 
1998-1999, Arsenal 0-1Leeds ,Gunners walikuwa na uhakika wa kuchukua EPL, walikuwa wanahitaji droo tu halafu Highbury. Dk ya 89 Jimmy Fold Hasselbank akapiga goli la meta 33.
Pia nusu fainali ya FA Man U walivyokuambia Arsenal kwa goli la miujiza la Giggs
 
Inaniuma Arsenal vs baca uefa fainal arsenal akiwa amemshika baca vilivyo golikipa akapewa redcard mwisho matokeo 2-1 arsenal kakosa ndoo.
 
German vs Cameroon WorldCup 2002, Ubabe wa kufa mtu. Kadi 16 za njano yaaan ilikua mguu jiwe.
 
Back
Top Bottom