Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,618
Sikumbuki mwaka vizuri lakini ilikuwa kati ya 1997-2000 mechi kati ya wakimbizi wa Burundi na wale wa DRC (zamani Zaire).
Mechi ilichezwa kwenye uwanja wa TTC Kasulu, mpaka mpira unaenda dakika ya 80 bado bila bila na kila goli linalindwa kwa nyuma ili watu wasitegue ndumba.
Dakika kama ya 85 Burundi walipata goli na katika purukushani za kushangilia kuna jamaa wa DRC walirusha vitu kwenye goli la Burundi na muda huo huo goli likarudi. Mpaka dakika ya 90 1-1, nyogeza 30 haikuzaa goli.
Kimbembe penati, kila timu ilipata 5 za kwanza, kila wakipiga goli linaingia, sasa DRC wakakosa penati ya 14, ilikuwa kama Burundi akifunga ndio basi ameshinda, lilipigwa shuti golikipa akalala huku mpira badala ya kuingia golini ukaganda na kudondoka chini bila kuzuiliwa na kitu.
Hapo si refa wala kamisaa alijua cha kufanya, ilikuwa mzozo mpaka mpira ukaisha bila mshindi.