Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

The special one beat the special team(Intermilan vs Barca),semi final Uefa champions league,2010. Barca anakufa tatu.Cambiasso,Motta,Sneijder miguu imejaa kama ndoo za litre 10,sijawahi kuona viungo waliokua wanazingatia,wanakaba kama hawa na kwa ujumla wao siku hiyo kilometres walizokimbia uwanjani ni kama kutoka Dar mpaka nyumbani Shinyanga.Bonge moja la gemu

Inter Milan ile haiji kutokea tena, namkumbuka Dejan Stankovic, Walter samuel, Lucio na wengineoo
 
Milan 5-0 Madrid...
mechi ya Pili ya Nusu Fainali msimu wa 1989-1990

Unaikumbuka mechi hii?
Ac Milan 4-1 Derpotivo

Mechi ya Marudiano, Ac Milan akiwa bingwa mtetezi anakula 4-0.
Derpotivo laCoruna ilikuwa na watu kama Walter Pandiani, Diego Tristan, Roy Makaay.
 
1.Mechi ya Man U 8-2 Arsenal
2.LFC 3-3 Man U ,Man U mpaka half time alikuwa anaongoza kwa goli 3 LFC karudisha yote nilikuwaje mdogo.
3. Germany vs Cameroon enzi za kina G.Song WC 2012 mechi hii ilikuwa na ubabe si mchezo kadi zilitembea kama mvua, Germany alishinda.
4.WB 1-0 Man U 2015 nililia kabisa nikatukana matusi kweli kweli na sijui niliyatoa wapi.

Pole sana ndugu.
 
chelsea hakucheza na bayer fainal uefa
hii ilikua supercup mkuu nakumbuka mourinho alishaingia akishangilia dressing room mara akatoka uko tena kama panya alokimbizwa na paka baada ya Robben kufanya yake ikawa 1-1 [emoji1] [emoji1] [emoji1] ngoma likaingia matuta Bayern akashnda baada ya lukaku kukosa penati apo ndo chuk ilianzia yeye na Mou siku iyo nilifurahi sana
 
World cup 1994. Quarter final. Spain vs Italia. Game iliisha 2-1 Italy akiibuka mshindi. Italy walielemewa sana na baada ya game Kwisha mzee Ariggo Sacchi anasema Italia hufanya vema pale wewe usipotegemea. Baadhi ya wachezaji ninaowakumbuka ni Andoni Zubizareta aliyekuwa goalkeeper. Joseph pep Guandiola, Luis Endriq Martinez, Fernardo Hiero, exeberia hao walikuwa kwa upande wa Spain.

Italy ilikuwa na Roberto Baggio, Costacuta, Paulo Maldini, Conte, Daniele Massaro, Franco Baresi, Albertin, Betri nk.

Game ilikuwa ya kufanya MTU. kama kuna mdau anaweza kuiweka hapa .

Umenikumbusha ukuta wa chuma, Costacurta na Baresi moja ya kombinesheni bora ya beki wa kati.
 
pia gem ya WC 2014 German v Algeria nilifurahi siku iyo Algeria walionyesha kiwango kikubwa sana German alshnda kwa tabu extra time
 
World cup 1994. Quarter final. Spain vs Italia. Game iliisha 2-1 Italy akiibuka mshindi. Italy walielemewa sana na baada ya game Kwisha mzee Ariggo Sacchi anasema Italia hufanya vema pale wewe usipotegemea. Baadhi ya wachezaji ninaowakumbuka ni Andoni Zubizareta aliyekuwa goalkeeper. Joseph pep Guandiola, Luis Endriq Martinez, Fernardo Hiero, exeberia hao walikuwa kwa upande wa Spain.

Italy ilikuwa na Roberto Baggio, Costacuta, Paulo Maldini, Conte, Daniele Massaro, Franco Baresi, Albertin, Betri nk.

Game ilikuwa ya kufanya MTU. kama kuna mdau anaweza kuiweka hapa .

pia umenikumbusha mechi hii:
Nusu Fainal World Cup 1990. Argentina 2-1 Italy

Mechi ilipigwa Stadio San Paolo, Uwanja wa nyumbani wa Napoli.

Ikumbukwe Maradona alikuwa anachezea Napoli, hivyo katika mechi hii alikuwa kama yupo Nyumbani.

Baada ya Waitaliano kuona timu yao imeelemewa, Waitaliano wengi wakiongozwa na mashabiki wa Napoli waliojaa uwanjani kumuona shujaa wao Maradona akiwa na timu yake ya Argentina wakaanza kuishangilia Argentina haswa Maradona.

Mechi ikaisha kwa mwenyeji Italia kutolewa na Argentina ambayo ilienda kufungwa na Ujerumani kwenye Fainali.
 
pia gem ya WC 2014 German v Algeria nilifurahi siku iyo Algeria walionyesha kiwango kikubwa sana German alshnda kwa tabu extra time

Algeria walikuwa wanataka kulipa kisasi cha kufungwa kwa hujuma wolrd cup ya 1982 pale Espana (Spain)
 
Inter Milan ile haiji kutokea tena, namkumbuka Dejan Stankovic, Walter samuel, Lucio na wengineoo
Hatari mpwa barca wakarudi Catalunya na visingizio kibao,mara safari ya basi ilituchosha,mara referee alikua anatoka Portugal akambeba Jose kiukweli viungo wa shoka,waliiua hii game
 
Man utd vs arsenal 1999 -2000 ilikuwa final nadhani ya kombe la FA mpaka dk 90 bao 1 kwa 1 exrtra time Giggs alianza kuwahesabu toka nje ya mstari wa kati walikuwa kina viera unapigwa chenga unawahi mbele unakuja kupigwa nyingine, jamaa mpaka akafunga bao David seaman ndio alikuwa golini nakumbuka arsenal ilikuwa ya kina Bergkamp, wiltord, kanu mechi ilikuwa tamu sana ile mwisho man 2 arsenal 1
 
Ilikuwa ni marudiano ya nusu fainali ya Fa cup, mechi ilipigwa Villa Park.

Bergkamp alikosa penati dk za majeruhi. kabla ya Giggs hajafanya mahesabu yake.
 
Man utd vs arsenal 1999 -2000 ilikuwa final nadhani ya kombe la FA mpaka dk 90 bao 1 kwa 1 exrtra time Giggs alianza kuwahesabu toka nje ya mstari wa kati walikuwa kina viera unapigwa chenga unawahi mbele unakuja kupigwa nyingine, jamaa mpaka akafunga bao David seaman ndio alikuwa golini nakumbuka arsenal ilikuwa ya kina Bergkamp, wiltord, kanu mechi ilikuwa tamu sana ile mwisho man 2 arsenal 1

wenger anakuambia hii game ndio inayomumiza kuliko hata ile ya 8
 
Manchester utd vs barcelona

uefa champs final
2011
ahahahah jamaa walipiga soka had kero... Nakumbuka.mr. Ferguson alitetemeka
 
Back
Top Bottom