Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

pia umenikumbusha mechi hii:
Nusu Fainal World Cup 1990. Argentina 2-1 Italy

Mechi ilipigwa Stadio San Paolo, Uwanja wa nyumbani wa Napoli.

Ikumbukwe Maradona alikuwa anachezea Napoli, hivyo katika mechi hii alikuwa kama yupo Nyumbani.

Baada ya Waitaliano kuona timu yao imeelemewa, Waitaliano wengi wakiongozwa na mashabiki wa Napoli waliojaa uwanjani kumuona shujaa wao Maradona akiwa na timu yake ya Argentina wakaanza kuishangilia Argentina haswa Maradona.

Mechi ikaisha kwa mwenyeji Italia kutolewa na Argentina ambayo ilienda kufungwa na Ujerumani kwenye Fainali.

Mkuu Mussolin5, baada ya game Kuisha magazeti ya kitaliano asubuhi yake yakatoa sababu tano za wao kuondolewa. Kumbuka Italia ndio ilikuwa mwenyeji.

Walisema ni mkosi. Sababu nilikuwa 5
1. Mchezaji aliyekosa penalt alivaa jezi no 17
2. Mchezaji aliyekosa penalti ilikuwa mechi yake ya 17 akiwa ndani ya Uzi wa Azzuri
3. Ilikuwa ni mechi ya 17 kwa Italia kucheza kwenye uwanja huo waliofungwa.
4....
5....
Sababu nyingine mbili kidogo nimesahau. Mourinho unaweza kuja kunisaidia hapa.
 
Last edited by a moderator:

Nimeangalia tena rekodi zangu, Italy alifungwa kwa matuta, aliyekosa penati ni Roberto Donadoni ambaye baadae alikuja kuwa kocha wa Italy kwenye Euro 2008
 
Last edited by a moderator:
Unaikumbuka mechi hii?
Ac Milan 4-1 Derpotivo

Mechi ya Marudiano, Ac Milan akiwa bingwa mtetezi anakula 4-0.
Derpotivo laCoruna ilikuwa na watu kama Walter Pandiani, Diego Tristan, Roy Makaay.

Naikumbuka sana. Kama sikosei ilikuwa 2004 final akachukua Porto ya Mourinho wakikipiga na Monaco ilikuwa balaa akina Evra na Ibara
 
Man utd vs arsenal 1999 -2000 ilikuwa final nadhani ya kombe la FA mpaka dk 90 bao 1 kwa 1 exrtra time Giggs alianza kuwahesabu toka nje ya mstari wa kati walikuwa kina viera unapigwa chenga unawahi mbele unakuja kupigwa nyingine, jamaa mpaka akafunga bao David seaman ndio alikuwa golini nakumbuka arsenal ilikuwa ya kina Bergkamp, wiltord, kanu mechi ilikuwa tamu sana ile mwisho man 2 arsenal 1

Hiyo mechi ndio nilimpa Giggs heshima mpaka leo. Ilikuwa nusu fainal na man u anaenda final kujipigia Newcastle.
 
Arsenal vs Man U kwenye ligi mechi ya pili msimu wa 2003/2004 ambayo iliisha kwa droo ya bilabila huku Van Nestrooy akikosa penalt. Hiyo mechi ilikuwa na ubabe sijawahi ona. Viera, R. Kean, Kewon, Phil Nevelle, na wengineo hatareee
 
Taifa Stars vs Ethiopia uwanja wa Taifa mgeni rasmi baba wa taifa....stars walicheza nusu uchi na kupigwa saana wahabashi mbele ya baba wa taifa...ikiwa mwisho wake kwenda mpirani
Simba vs Yanga......nyamagana mwanza dk ya 90 yanga anasawazisha 1-1 extra time yanga anaongeza moja anachukuwa kombe.
 
Vieira alikuwa red

Mwamuzi alitoa penati dk za lala salama

Van Nistelrooy akapiga besela akakosa.

Martin Keown na wenzake walimshambulia sana baada ya filimbi ya mwisho.
 
hakika uko sahihi mkuu...Msimu ule ulikuwa na maajabu yake.

Na mwingine aliyetisha kwa upande wa Monaco alikuwa Nonda Shaban akifunga goli dhidi ya Chelsea ya Ranieri kweye nusu/robo final sikumbuki vizuri
 
Na mwingine aliyetisha kwa upande wa Monaco alikuwa Nonda Shaban akifunga goli dhidi ya Chelsea ya Ranieri kweye nusu/robo final sikumbuki vizuri

Robo nafikiri, maana nusu walikutana na Real Madrid nadhani
 
'09 Fifa Confederations Cup final.

United States vs Brazil. Hiyo comeback ya Brazil, whoo!!
 
Real Madrid vs Real Mallorca. La Liga 2006/07 last game of the season. Madrid na Barca equal on points, Madrid anahitaji kushinda ili kuwa bingwa coz first Clasico alishinda, ya pili akatoa draw.

Mpaka half time Mallorca wako mbele goli 1 na wamepaki basi zao za kutosha. Upande wa pili Barca kashampa mtu 4. The pressure is mounting, Rafa Nadal anatia huruma tu kwenye stands, Tom Cruise na wife wamekuja kumcheki Beckham. Top Scorer wetu Ruud Van the goals-man anaumia dakika ya 38 nadhani, no hopes. Inabidi tumtegemee Beckham kupiga mipira mirefu watu waotee headers, Becks nae anaumia 2nd half mwanzoni kabisa nadhani, machozi. Only Robinho could dribble.

Then, Jose Antonio Reyes na Mamadou Diarra happen, 3 -1 in the end. Campeones baada ya misimu minne patupu. Na Capello anatimuliwa.
 
Taifa Stars vs Ethiopia uwanja wa Taifa mgeni rasmi baba wa taifa....stars walicheza nusu uchi na kupigwa saana wahabashi mbele ya baba wa taifa...ikiwa mwisho wake kwenda mpirani
Simba vs Yanga......nyamagana mwanza dk ya 90 yanga anasawazisha 1-1 extra time yanga anaongeza moja anachukuwa kombe.

Masahihisho. Game ilikuwa stars vs Sudan na c Ethiopia
 
Back
Top Bottom