Ni media ipi naweza peleka matangazo na yakaenda viral

Ni media ipi naweza peleka matangazo na yakaenda viral

Media nyingi inategemea na aina ya kipindi ambacho unategemea kupitishia matangazo yako.

Azam Tv wanapoonyesha mechi ya simba vs yangu naskia gharama ya tangazo moja ni 10m+
Mechi za kawaida tangazo moja ni 3m+

Hvy hvy pia kwenye media zinginezo
 
Kwa nature ya biashara yangu ya vipuli vya magari kwa Whatsapp Huwa napost ila sipati positive impact kutokana na kwamba asilimia kubwa ya viwers wangu hawana magari

Kwa upande wa facebok ndo Sjawahi kujaribu na Sina hata account 😄
Ila kwa ushaur wako mzuri nitafanya hivo

JE kwa nature ya biashara yangu nipeleke tangazo kipindi gani kwa hizo radio ulizotaja?
Achana na radio na TV mkuu. Kwenye bajeti yako ya 10M unaweza kwenda viral na ukapata matokeo chanya. 5M wekeza kwa influencers wa Instagram mfano saivi TX Dullah anatrend na subaru nenda mtie hata milioni mbili kila siku akupost kwa story flani ya huduma yako ya spare parts kwa mwezi mmoja.
3M nenda Facebook nnua page weka challenge ya shares kwa wadau watashinda zawadi na huku ni hizo spares na vipodozi zote zinaenda. Nenda boost tangazo lako liweze kuwafikia watu wengi zaidi, jiunge kwenye magroup tofauti na upost habari zako huko na kama group lipo active basi mtie mzigo admin aioandishe na itoleww challenge ya likes and shares.
2M weka Tweeter (X) huko tafuta wale wanaopost habari za magari wenye followers wengi gawanya hela kwa watu wawili tu ambao utaona wana engagement kubwa ya shares na umuambie awaombe followers wake kushare zaidi huku iwe ni kazi ya mwezi mmoja.
Hakikisha unaijua biashara yako vizuri au una mtu anayezijua vizuri bidhaa unazouza ili awe na maelezo ya ziada juu ya bidhaa kwa mteja halafu hakikisha simu yako inapatikana mda wote na upo active kwenye hiyo mitandao ili uweze kujibu maswali kwa wakati.

Kila la kheri.​
 
Back
Top Bottom