Nimepokea kwa mshangao taarifa ya kusudio la kukodishwa kwa klabu ya Yanga kwa M/ kiti wake Yusufu Manji, uamuzi ambao umepitishwa kwa kauli moja na mkutano mkuu leo hii tarehe 6 Agosti 2016. Kwa umri wangu huu wa utu uzima wa kati sijawahi kusikia mfumo wa namna hii kwa uendeshaji wa klabu ya mpira wa miguu duniani. Naomba kwa yeyote mwenye kuufahamu mfumo húu anielezee na mm, ili tujifunze kwa pamoja ufanisi wa mfumo huu huko duniani. Lkn pia nataka kujua huu mkutano ulioitishwa kwa dharura ulikuwa ni kwa ajili ya ukodishwaji huu pekee au kulikuwa ni kitu kingine cha msingi?