Paramagamba
Member
- May 12, 2017
- 85
- 129
Mimi ni mwanaume wa miaka 31 sasa. Mnamo mwaka 2002 nilipokuwa form II nilianza kusikia kaharufu flani hivi kabaya kabaya kanatoka kwenye mwili wangu kaharufu ka uvundo sio uvundo mkojo sio mkojo lakini niliamua kupuuzia kwa sababu nilikuwa ninaoga vizuri kila siku mara 2 kwa sabuni na dodoki zuri kwahiyo nikahisi labda ni kale kaharufu ka nguruwe kamebakia kwenye mwili wangu kwa sababu shuleni tulikuwa na zamu ya kulisha na kusafisha mabanda ya nguruwe mara kwa mara.
Siku zikazidi kwenda mbele harufu ipo na mimi popote pale niendapo. Nilizidi kuparangana kwa kuzidisha kuoga mara 1 zaidi kwahiyo nikawa ninaoga mara 3 kwa siku na kufua nguo zangu kwa sabuni ya OMO na kujiwekea kanuni kutovaa nguo mara 2 hata kama nimeivaa kwa nusu saa tu. Nimefanya kila aina ya mbinu ili harufu itoke mwilini mwangu lakini ndio kama nikawa ninazidi kufeli. Nilihangaika nayo kwa muda wa mwaka 1 na nusu hatimaye sasa ile harufu ikawa kama imejeruhi pua zangu kabisa kwa sababu nimeishaizoea na imekuwa sehemu ya mwili wangu, sasa nikawa kama sihisikii kabisa tatizo likabaki kwa yoyote yule aliyepo karibu yangu, lazima kamasi zimtoke au wengine naona wanapata mafua kabisa.
Kutokea hapo kipimo cha harufu yangu kikawa ni mtu aliyepo karibu yangu. Nikawa ninaangalia ni namna gani mtu yoyote aliyepo karibu yangu anavyo jitahidi kupambana na harufu yangu. Wengine mpaka wakawa wanaziba pua kabisa kwa nguvu ila wengine hali hii huwa inawashinda na wanaamua kuhama mahali nilipokaa mimi na kuhamia sehemu nyingine. Hii ninaiona sana hasa hasa kanisani na kwenye daladala. Mtu akipata tu fursa ya kwenda kutoa sadaka au kwenda kupokea ekaristi takatifu harudi. Kwenye daladala unaona mtu yanamshinda anaamua kuhamia siti nyingine sio kwamba haina mtu au labda ni siti ya dirishani hapana, ni usawa ule ule aliyokuwa amekaa na mimi mwanzo anahamia kwa jirani ilimradi apate ahuheni kwenye safari yake.
Baada ya muda mrefu sana kujichunguza mara kwa mara nikaja kugundua kwamba hii harufu inatoka sehemu za map*mbu na sio kwingine kokote. Katika maisha yangu ninaamini hakuna mtu msafi duniani zaidi yangu. Naoga na kila aina ya sabuni na shampoo mara 3 mpaka 4 kwa siku. Nimekuwa nikisugua sana hizi p*mbu wakati wa kuoga. Huwa inanilazimu kutumia muda mrefu bafuni ili kupunguza hii harufu lakini wapi. Asubuhi inanilazimu kuhamka saa 10 ili niweze kuoga si chini ya dakika 45 kabla ya kwenda kazini, wakati wa lunch kazini natumia nusu saa kwenda kula na nusu saa chooni kusafisha p*umbu kwa maji na sabuni. Jioni saa 12 nikifika tu nyumbani moja kwa moja bafuni saa nzima naoga na kujisuhuza mara 2 mbili. Saa 4 usiku kabla sijalala ni bafuni kwanza kuoga kisawasawa kwa dodoki. Wikiendi ikifika huwa ninashukuru kwa sababu hata sijui huwa ninaoga mara ngapi kwa sababu ninaoga kwa fujo kila muda. Harufu haijawahi kupungua.
Nimejaribu kutafuta visingizio labda ni joto au mwili kuchemka lakini kipindi cha masika kinatosha kunipinga juu ya hypothesis niliyokuwa najaribu kuitengeneza kwenye utafiti wangu. Ofisi yangu imefungwa na air conditioner kwa hiyo swala la kisingizio cha joto au jasho hakiwezi kuchukua nafasi kwa sababu remote controller ya AC ipo mezani kwangu na muda wote huwa inacheza kwenye 18° mpaka 16° nyuzi joto.
Muda mwingine ninapata ugumu sana wa kufanya kazi zangu niwapo kazini. Yani wote wananijua kwamba ninanuka lakini kwa sababu swala la kunuka ni swala la aibu kubwa, hakuna hata siku moja mtu yoyote amekwisha niambia. Yani mfano nikiwa kwenye korido alafu kuna mtu mwingine kwa mbali anakuja kwenye korido akaniona kwa ghafla ataanza kutafuta mahali pa kutorokea ili mradi asikutane na mimi akasumbua pua yake kwa harufu hii kali na kama kuna mlango wowote wa kuingia kwenye ofisi nyingine kwenye korido basi huo huo ndio utakuwa pona pona yake vinginevyo utamuona anaanza kuhangaika na kujikuna kuna kichwa mara uso na mwishoni kwenye pua na ataiziba kisawasawa mpaka tutakapo pishana ndio anaiachia tena kwa kupiga chafya kali, kuvuta vuta mafua au kuungurumisha koromeo lake kana kwamba kuna kitu kama koozi kubwa limemkaba anataka aliteme.
Najua utajiuliza nimetumia dawa gani au manukato gani ya kujipaka. Nimetumia dawa na manukato ya kila aina. Nimekutana na madaktari bingwa wa ngozi wa kila aina na wengine wameniandikia dawa, wengine wamesema ninywe sana maji, wengine niende kanisa gani sijui nikaombewe na wengine wameishia kusema eti nina matatizo ya kisaikolojia na kupendekeza mimi kwenda kuonana na wanasaikolojia lakini ukiwauliza harufu wanaisikia au hawaisikii hapo ndio unakuwa umewaweka njia panda kwa sababu hata wao inawakera na wanakubali kwamba ipo. Mwezi uliopita nimetoka muhimbili kuonana na wataalamu wengine tena wamenipatia mafuta flani ya cream yanaitwa EPIMAX kopo kubwa nimetumia mwezi mzima na sasa linakaribia kuisha lakini harufu bado ina mimi.
Maisha yangu yamekuwa ni ya gharama sana kutokana na hii harufu. Mpenzi wangu ni mvumilivu sana ingawa bado sijamuoa na ilikuwa nimuoe mwaka jana lakini nikasema wacha kwanza nipambane na hii harufu niweze kuitokomeza na baada ya hapo ndio anipeleke ukweni kunitambulisha na baadae taratibu za kutoa mahali zianze. Nimekuwa nikiwaza sijui harusi yangu itakuwaje na hii harufu kwa msururu wa wageni waalikwa kuja kunipatia mkono wa pongezi au kugonga cheers. Ni fedheha kubwa sana kwangu na sipo tayari kuhaibika namna hiyo. Hivyo ninawaalika wataalamu mbali mbali mnipe ushauri wa namna gani nitaweza kutokomeza hii harufu na nina aidi zawadi nono kwa yoyote atakayefanikiwa kunipatia ufumbuzi wa fumbo hili gumu. Kwa hakika tatizo langu ni One in a Million. Sijawahi kukutana au kusikia mtu mwenye tatizo kama la kwangu hivyo ni bahati sana kukutana na mtu kama mimi kwenye maisha ya mwanadamu. Kwa kweli kuna muda mwingine hata ninakosa hamu ya kuishi. Naombeni msaada wenu ndugu zangu.
Mubarikiwe wote. Amina.