Ni Mikutano ya Hadhara au Mikutano ya Wanachama wa CHADEMA? CHADEMA wamefeli wapi?

Ni Mikutano ya Hadhara au Mikutano ya Wanachama wa CHADEMA? CHADEMA wamefeli wapi?

Ukweli usiofichika mikutano ya CHADEMA imekosa mvuto. Watu walikuwa wachache sehemu zote walizofanya. Na ikageuka kuwa mikutano ya wanachadema. Haina tofauti na vikao vya ndani vya chama.

CHADEMA inapaswa kujua sababu ya yote hayo ni nini, sikubaliani na wanaosema eti mwenyekiti Mbowe ndio chanzo. Chama kikifeli lawama zinapaswa ziende kwa viongozi wote.

Tuseme Mbowe hakuwa amejiandaa na hakuwa na sera ya kuvutia watu, je ni yupi Kati ya viongozi wa chadema mwenye sera? Viongozi wote wameshindwa kudeliver, hivyo lawama zisiende kwa mwenyekiti pekee.

Mikutano kujaa Wanachama wa CHADEMA peke yao ni dalili mbaya.

Nitoe ushauri kwa chadema, ushauri huu hata mbowe anaujua na ndio maana alisema amechagua maridhiano badala ya maandamano kwa kuwa anawajua watanzania hawawezi kufanya maandamano. Yalishaitishwa maandamano mara nyingi tu Ila yalishindwa kufanyika.

Ushauri:
Chadema iachane na mikutano ya hadhara, kwa kuwa watanzania hawapendi hii kitu. Wapo busy na maisha. Huko kwingine watapata aibu kubwa mno zaidi ya waliyopata Mwanza na musoma.

Angalia usichanganyikiwe. CHADEMA wanafanya siasa wewe unaleta maneno.
 
Wengi tuna hamu ya kusikia Sera lakini bado hawa jamaa wamejaza hotuba za kulaumu,kutukana na kutengeneza chuki.
Kama ilivyo MITANDAONI agenda kubwa ni matusi na kujimwambafai oooh! Hawatuwezi walitushindwa wanatuogopa alafu mwingine anasema walituuwa walitunyanyasa walituweka ndani NK

Muhimu hapa tuleteeni hoja ili tukiwachagua mtusaidie kuondoa shida za Wananchi ikiwemo kuondoa chuki baina yetu ili tuwe kitu kimoja katika UJENZI wa Taifa.
 
Kama kwenye mkutano wa uchaguzi mkuu ambao mgombea na mgeni mkuu wa mkutano huo alikuwa mbelgiji Lisu lakini watu wahawakuhudhuria kumuona, vipi mikutano hii ambayo inasemekana wageni wakuu wa mikutano hiyo ni walevi waliokuwa wamelewa chakali huko Mwanza na Musoma?

Siasa za Tanzania zili turn around mwaka 2015. Asilimia kubwa ya vijana na wazee hawaamini tena katika siasa wala wanasiasa.

Kwa sasa siasa hasa za wapinzani zimebakia mitandaoni na hii ni kwa sababu wengi wanalipwa kwa kuandika thread zenye kupotosha umma wa watanzania.
View attachment 2492722
Unajaribu kuvunja in mioyo ya wanamageuzi wa maeneo mengine, lakini nakuhakikishia tayari umefeli.
 
Tatizo wana ajenda ya Katiba ambayo sio public interest

Issue zingine zote Mama anaupiga mwingi
 
Wengi tuna hamu ya kusikia Sera lakini bado hawa jamaa wamejaza hotuba za kulaumu,kutukana na kutengeneza chuki.
Kama ilivyo MITANDAONI agenda kubwa ni matusi na kujimwambafai oooh! Hawatuwezi walitushindwa wanatuogopa alafu mwingine anasema walituuwa walitunyanyasa walituweka ndani NK

Muhimu hapa tuleteeni hoja ili tukiwachagua mtusaidie kuondoa shida za Wananchi ikiwemo kuondoa chuki baina yetu ili tuwe kitu kimoja katika UJENZI wa Taifa.
Kuna chuki hii nchi?

Njoo na mifano hai kwamba hilo ni tatizo
 
Back
Top Bottom