Ni mimi tu au....!

Ni mimi tu au....!

Samboko

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2011
Posts
5,420
Reaction score
7,788
Kuna hali hua inanitokea na hii ni tangu nakua nimegundua hili,
Inapotokea ninapo onana na jinsia ya kike kwa mara ya kwanza alafu akanivutia sana, sasa kadri ninavyozidi kumuona na hata pengine kumzoea anazidi kunibadilkia hadi mwisho wa siku namuona wa kawaida sanaa,

Sasa na kwa wale ambao nawaona wabaya au wa kawaida kwa mara ya kwanza hunibadilikia na kua wazuri sana kadri tunavyozidi kuonana au kuzoeana.

Pia vivyo hivyo kwa wale ninaowatongoza ikiwa hatujazoeana ni asilimia tatu ya mia wanaoonyesha ushirikiano kwa wakati huo, sasa katika wale ambao hunikataa na wengine dharau kibao na kuniringishia mabwana zao ni haohao wanakuja kunipenda tena sana baadae kadri wanavyonizoea zaidi.
Hata maeneo ya kazini hutokea wanawake wakiniona kwa mara ya kwanza hawanichangamkii hata wengine salam tu ni shida lkn kadri siku zinavyoenda wananizoea sana kupita kiasi,
Sasa mimi nashindwa kuelewa hii hali.
 
Ni hali ya kawaida kama umemtamani tu. Kutokana na tamaa zako utakuwa na hamu kubwa ya kumsogeza karibu haraka. Akishasogea ukaonja kibubu cha asali hali huwa tofauti. Unakuwa ushamkinai maana huna upendo kwake.

Hali huwa tofauti kama unapenda kwa dhati maana kila mnapokuwa pamoja ndio kuna bond zinazidi ku form na mnakuwa attached to each other zaidi.

Unaambiwa watu wanaopendana kwa dhati mifumo yao hata ya upumuaji/mapigo ya moyo hu synchronise na kuwa sawa.. Kuna chemistry inajijenga kati yao.

Hapo kazi ni kutia tu catalyst ku speed up chemical reactions, mambo yanakuwa motoo
 
Hahaaa, sawa mkuu,
Ila haya hutokea wakati wa ugeni na wahusika hata kabla wengine sijawatongoza
 
Back
Top Bottom