Ni Mimi tu ndio naona na kusikia! Kampeni za CCM hazina Mvuto

JF Member

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2014
Posts
7,914
Reaction score
10,793
Ninajaribu kudadisi kuona namna CCM inavyoendesha kampeni zake.

Naona hazina Mvuto. Nimejaribu kuangalia kwenye magroup ya wasapu kimya kingi.

Nafatilia mtaani wengi wanasubiri kupewa chochote.. wafia chama wamepungua Sana.

CCM embu changamkeni Ili kampeni zichangamke.

Au komba kakosa mrithi.
 
Mkuu umeanza kukisakama chama chako.

Hata hivyo zaidi ya kusikia Mbowe kakamatwa umesikia habari za uchaguzi mwaka huu?

Mitano tena
 
Ccm haiwezi tena kushindana kihalali wala kuvutia wananchi, nguvu yao kubwa iko kwenye kumwaga hela zisizofahamika zinatoka wapi, na kutegemea mbeleko ya vyombo vya dola, ndio maana unaona wanalazimisha zaidi kushinda kwa kuengua wapinzani.
 
Wameshamaliza uchaguzi hao kwa kura za wizi
 
My friends, ladies and gentlemen,

mvuto wa kishindo kikuu kwa CCM ni Nov 27, 2024 siku ya J5,

hakuna haja ya kubabaika wala kuwa na mawenge ya mapema ndrugu zango πŸ’
 
Mtaji wa CCM unatokana na ujinga na umaskini wa Watanzania waliokuwa wengi. Kundi hili halijui kuhoji wala kufanya tathimini juu ya madudu yanayofanywa na watawala.

Ni kundi lenye macho lakini halioni, na lina masikio lakini halisikii. Kutokana na kutamalaki kwa ujinga limejaa watu waoga na wasiojitambua kabisa.

Kundi lililokata tamaa, huku likisubiri miujiza na kuonewa huruma. Halijiamini wala kujitambua kuwa ndilo lenye suluhu katika mustakabali wa maisha yao wenyewe. Kundi lenye kudanganywa na kukubali kudanganyika.
 
Ukilinganisha na za chama gani?
 
Yaani hawana kitu cha maana wanachofanya, Jana nilikua Manzese, wameweka nyimbo za wahuni na wamejaza Watoto. UJINGA mwingi
 
achana na ramli chonganishi gentleman
Najua ninachokiaema nimekuwepo kwenye upigaji kura na usimizi muda mrefu kuliko wewe. Ccm haishi inashindishwa. 2020 kura zilipigwa siku 2 kabla pale ofisi za ccm magomeni. Walitafutwa vijana mitaani. Walipikiwa wali maharage na kuahidiwa 5000 hawajpewa hadi leo. Ukitaka kukubali sawa ukikataa pia sawa
MFALME YUPO UCHI
 
Mambo ya kura sawa.

Ila kampeni Sasa. Watu wazito sana kujitokeza, Hadi wapewe mihera.

Shida iko wapi?
kampeni za CCM zilianza kwenye kuhamasisha nyumba kwa nyumba kujiandikisha na zinaishia kwenye kampeni za nyumba kwa nyumba hadi siku ya kupiga kura,

ndiyo maana kura za maoni ndani CCM zinahamasa kuliko Uchaguzi wenyewe ambao ni kukamilisha ratiba na katiba tu πŸ’
 
Okay.

Ngoja tuone sasa itakavyo kuwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…