Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hapana ni nini mkuu??Unajua kitu inaitwa DUREX dogo?
Mkuu tukiisikiliza sauti ya shetani atatuingiza mitegoni halafu yeye anakaa pembeni, lakini pia tutambue huyo binti nae sio mwanamke wa maana ni mshenzi fulani hivi, kwa maana mke wa mtu anayejiheshimu na kujua maadili ya ndoa hawezi kuwa lainilaini kwa watu wa pembeni.Shetani mkuu anajaribu kututoa kwenye track eti usizini Ni amri ya sita.
We pia unaishi Mtwara??Dah...! Hatari ukute huyo ni mke wangu ndio unamtama hivyo aisee na mpaka hapo hayupo kasafiri.
[emoji23][emoji23][emoji23]Asee Tuition ya nini tena mkuu??Tulia Dogo soma tution kwanza
Nimekupata mkuu[emoji120] ila huyu mschana pia ni driving force ya mimi kutaka kufanya nae hiki kitendo kwa kuwa naona yeye kadhamiria zaidi kwa sasaUsitamani Mke wa jirani yako.
Tamaa tu hiyo Hakuna upendo hapo. Usiruhusu tamaa izidi uwezo wako wa kufanya maamuzi sahihi.
Asee[emoji26]Fikiria kuwa huyo mke ni wako, halafu kuna mtu pembeni anammendea na udenda unamtoka kwa mkeo ambaye mnaishi vizuri kwa mapenzi na amani halafu kidudumtu anataka kuwaharibia,
Utamfanyaje ukigundua? Jibu utakalopata utaamua kuendelea kumfuatilia au la.
Na kama utashindwa kudhibiti moyo wako kwa huyo kumbuka wako zaidi ya huyo utakuwa chizi.
Mche mola wako, tafuta chako cha halali wacha kumendea vya watu, siku ukipata wako watajakupigia mpaka kitandani kwako.
Kijana pambana na maisha umri unaenda, kadili siku zinavyokwenda ndio mabinti wazuri wanazaliwa kuujaza ulimwengu.
Tafuta hela na maisha kwanza watakuja mpaka uwakimbie tena akina Cleopatra kabisa kutoka Iraq na Egypt...
Mkuu wa kupuliza naomba maana ya hiki kituUnajua kitu inaitwa DUREX dogo?
[emoji120][emoji120]Nimemuelewa mkuu naona wengine wanani simanga tu na wakati nimeomba ushauri....Nitazingatia alichonieleza ndugu yangu hapo juu ila..Zingatia ushauri huu [emoji115]
Shukrani kaka[emoji120]Mkuu jifanye kama humujui na umpoteze itakusaidia sana kuepukana na mambo mengi nakuambia kama kaka yako.
bad enough mumewe yupo anasoma haya maandishi yako...Habari zenu waungwana??? Mimi mdogo wenu leo naweka hili bandiko humu kuomba ushauri kwa maana akili na maamuzi yangu naona kama yanashindwana na matamanio ya mwili wangu...
Kiufupi kuna msichana hapa mtaani kwetu anaonesha hisia za kunipenda sana na ukweli ni kuwa nampenda pia na sijui ni kwanini imekuwa rahisi kushawishika naye...
Huyu mschana nilikuwa namchukulia kama dogo tu kipindi ambacho tumehamia hapa mtaani nilipo (tulihamia mwaka 2005) akiwa bado mdogo tu na alikuwa na dada zake wengine hao ndo nilikuwa nawafukuziaga kipindi kile tupo wadogo sana kama 15years hivi...
Sasa hivi ameolewa huko Mtwara lakini kipindi anaolewa mimi sikuwepo hapa mtaani ambapo nimerudi tena kukaa hapa kwasababu zangu binafsi,mwaka jana alikuja kwenye harusi ya ndugu yake ndo nikapata bahati ya kuonana nae tena akiwa kabadilika sana infact she is so beautful,she has nice figure na kitabia yuko fresh kifupi ana vigezo vya mke ninaemhitaji.....Nikampaga namba kwa maana nilikutana nae juu juu na aliniambia kuwa baada ya hiyo harusi ataondoka tena mtwara lakini hakunitafuta hata kidogo na sikujua sababu kabisa nikampotezea (Kumbe aliolewa)....
Mwaka huu mwezi wa kwanza alikuja tena kutokea huko Mtwara aseee nilimface na kumshutumu kwanini hakunitafuta na mixer kutoa yangu ya moyoni ndio la haula! ananiambia kuwa kaolewa asee nilikata tena hayo mazoea nikaamua nifanye mambo yangu mengine mpaka alipoondoka tena kurudi kwa mmewe huko Mtwara..
Kwenye Tatizo Sasa; Kwenye Mwezi wa 7 mpaka hivi ninavyotype yuko tena hapa mtaani na naona bado wana mahusiano mazuri tu na mumewe huko alipo (Kwa kuwa mara kwa mara namkuta akiwa anazungumza nae) lakini tatizo ni kwamba na yeye ameamua kureveal hisia zake kwangu ila kikwazo ni mumewe....
Kipindi hiki sasa mara kwa mara amekuwa akinilalamikia kuwa anakuja homboi hanikuti mpaka jana nilipoamua kumpanga aje home leo asubuhi (Agenda ya kukutana wote wawili tulikuwa hatuifahamu) asee ni kama masikhara leo alfajir kabla sijaamka kumbe alikuja na kunigongea mlango nikiwa bado nimeuchapa usingizi yaaani asubuhi sana....Na mida ya saa mbili hivi akapita tena na kuja mtaani kwangu na kwa wakati huo akawa amenikuta nishaamka najiandaa kuingia bafuni,inshort kakawa kanalalamika kuwa nimelala sana na hapa nikajua kuwa kuna kitu alihitaji kunipa...
Nikampanga nikirudi kuoga na yeye arudi hapo (kwa kuwa yeye kaja na mdogo wake kwenda kuchota maji karibu na hapa nyumbani ikiwa ni kigezo cha kuja kuonana na mimi baada ya ile mara ya kwanza kufeli)...Naweza sema kama haikupangwa hii leo maana baada ya hapo hakurudi tena (Sababu ni huu mtaa tunaoishi jinsi ulivyo na ukaribu wetu na majirani,pia muda haukuwa rafiki kwake) na kuna sehemu ameniaga kuwa anaelekea na atarudi kesho yake (Jumapili).
Nampenda sana na Naona ananipenda kiukweli tatzio ni mke wa mtu na wallah akili na imani yangu inanituma nisifanye hiki kitu kwa kuwa nilijiapiza before kuwa sitaweza kuingia katika mahusiano yanayohusisha ndoa ya mtu mpaka mimi nitakapokuja kuoa lakini dah huyu ananipa wakati mgumu sana..
Anavyodai ananipenda tangu tuko wadogo mapindi yale niliyokuwa ninamdharau kumuona dogo tu kwa kuwa dada zake ndo walikuwaga wa moto kipindi kile ila inshu ndo kaolewa sasa[emoji26] kiukweli naona kadhamiria tu kunipa tunda kabla hajarudi tena huko Mtwara
Wakuu mnanishauri vipi mdogo wenu....I'm 23 Years na Yeye ni kama 20 years hivi ila kaozwa mapema na mumewe sijawahi kumfahamu
Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app