Ni mkoa gani Tanzania kinafanyika kilimo Cha umwagiliaji?

Ni mkoa gani Tanzania kinafanyika kilimo Cha umwagiliaji?

Kama unataka Mali basi utaipata shambani, Mimi nimeamua kuunga juhudi nikashinde na kuteketea shambani huko labda tutatokea huko, nilichogundua biashara sio kwa ajili ya Kila mtu huko competition+uchawi ni mkubwa.

Mtaji wa kilimo kianzio kama million 5 upo, nataka nilime kwa kutegemea umwagiliaji na mbolea maana bongo hapa ulisema utegemee mvua ni kubahatisha tu, unaweza teketeza hata million 10 hivi hivi.

Niko Mwanza kwa Sasa, je mkoa gani Unafaa kwa kilimo Cha umwagiliaji? Nilifikiria niende SINGIDA nikalime vitunguu Lakini pote huko ni pakame sidhani kama Kuna bonde la maji.

Natanguliza shukrani.
Kilimanjaro na Arusha maji yapo ya kutosha kule umwagiliaji ni wa uhakika
 
Iringa kuna scheme kubwa ya umwagiliaji maeneo ya Kalenga kwa chief Mkwawka.

Sema uchawi pia upo sana tu kuna uchawi unaitwa lukupi huu n balaa


Kwa ushauri chochote utacholima usiache kuweka mahindi walau heka moja
 
Iringa kuna scheme kubwa ya umwagiliaji maeneo ya Kalenga kwa chief Mkwawka.

Sema uchawi pia upo sana tu kuna uchawi unaitwa lukupi huu n balaa


Kwa ushauri chochote utacholima usiache kuweka mahindi walau heka moja
NIMELIMA NAO WAHEHE WABENA ILA KIBOKO WA WOTE MWANJI NI NOMA ila hayo mambo ni km ukaamini.
 
Mbeya wilaya ya Mbarali kata ya Lugelele kitongoji cha Igomelo kuna scheme ya wagiliaji maji yanatiririka mwaka mzima sasa hivi waliolima vitunguu wananeemeka. Pia kuna wanaolima hoho, mahindi, matango, nyanya na mazao mengine mengi tu
 
Kikubwa maji yawepo mkuu na mazao yanayo kula maji ya kutosha yanakuwa super sokoni.
Nilienda kwa ndugu yangu mmoja mlandizi nilikuta kaendelea sana hadi gari analo na stock ipo ya mpunga wa kutosha almost gunia 100 na ushee

Toka ameanza irrigation system mafanikio yapo kikubwa ni kuwa karbu tu.

Uliza pia na morogoro mana sijafika huko kuhus kulima mpunga kwa umwagiliaji.
Mlandizi kuna kilimo cha umwagiliaji

Sent from my WAS-TL10 using JamiiForums mobile app
 
Katika harakati zako mtangulize Mungu.Kama ni muislamu shika IMANI yako vizuri, kama ni mkristo fanya vivyo hivyo,,, n.k.KAZI NA SALA mkuu.
 
Back
Top Bottom