CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Habari ya asubuhi wanachama wa JamiiForums,
Ukiwafuatilia kwa makini wagombea wawili wenye ushindani mkali Tundu Lissu dhidi ya John Magufuli kwenye uchaguzi wa Tanzania wa mwaka 2020 utagundua yafuatayo:
UAMUZI NI WAKO NDUGU, MIMI NIMEAMUA KUMCHAGUA TUNDU LISSU MAANA NI MZALENDO WA KWELI NA MWENYE MALENGO YA KUWEKA MISINGI IMARA YA NCHI YETU.
Ukiwafuatilia kwa makini wagombea wawili wenye ushindani mkali Tundu Lissu dhidi ya John Magufuli kwenye uchaguzi wa Tanzania wa mwaka 2020 utagundua yafuatayo:
- Tundu Lissu ni mgombea mwenye maono ya mbali na mwenye malengo ya muda mrefu wakati John Magufuli ni mgombea mwenye maono mafupi na malengo ya muda mfupi.
- Tundu Lissu anaitazama Tanzania ya miaka 100 ijayo wakati hata yeye hatokuwepo duniani wakati John Magufuli anaitazama Tanzania ya miaka 5 mpaka 10 ijayo na kwamba anataka awepo hai yote yakifanyika kitu ambacho hakina uhakika.
- Ukitazama hotuba za Tundu Lissu na maongezi yake na wahariri wa habari utagundua akitaja upeo wa mbali zaidi mfano kuhusu maendeleo ya kilimo na maisha ya vijijini aligusia miaka 50 ijayo kwa John Magufuli utagundua maamuzi yake ya hapo kwa hapo bila kujali uendelevu wake mfano alipoamuru kujengwa kwa barabara huko Geita na kwamba nyumba za watu zinaweza kubomolewa.
- Anayeweza kuifanya Tanzania kuwa Ulaya ni Tundu Lissu na siyo John Magufuli kwa maana Ulaya hawakurupuki bali hukaa na kuweka malengo ya muda mrefu kwa zaidi ya miaka 100 bila kujali kuwa waweka malengo watakuwa waliisha kufa. Huu ndiyo uzalendo halisi kwa nchi. Maana unataka vizazi vingi vijazvyo vinufaike.
UAMUZI NI WAKO NDUGU, MIMI NIMEAMUA KUMCHAGUA TUNDU LISSU MAANA NI MZALENDO WA KWELI NA MWENYE MALENGO YA KUWEKA MISINGI IMARA YA NCHI YETU.