Nilikuta na demu m'moja wa kimburu. Sikuwahi kuishi nae before ingawa alikuwa ni mradi ambao ninauendesha bila ubia na mtu. Balaa likaja baada ya kukubaliana nae tuishi pamoja.
Kwanza hajiamini muda mwingi ni kama anahisi ameingia kwenye mji wa mwanamke mwenzake au anatoka na mume wa mtu.
Alikuwa mtu wa kunyong'onyea sana,mara chakula aseme kashiba au apike wali ila yeye atasonga ugali ndio ale na hapo chakula unakuta ni kizuri sana tu. Ikawa inanipa maswali sana hii hali.
Sasa changamoto ilinishinda baada ya kuwa anazingua chumbani. Mara aseme anaumwa wakati ni demu kipindi alikuwa akija room kwangu kule chuo tulikuwa tunapelekeana show ya kibabe for hours. Na hats tukikutana lodge moto ni ule ule. But baada ya kuingia ndani ikawa changamoto kama hivyo.
Mara aseme anajisikia vibaya,mara aseme anajiskia homa ukimgusa wa baridi,ukikausha anakwambia mbona haukunibembeleza tufanye umeniacha tu nimelala na hamu zangu. 😂😂.
Siku zingine anastuka usiku mnene saa saba,nane au tisa. Anakuamsha ghafla utadhani kuna mwizi kaingia ndani,mtu unaamka mapigo ya moyo yanalipuka,anakwambia kwa kunong'ona unasikia ? Una muuliza "nini?" Anakwambia hausikii watoto wanaongea kwenye korido?
Au akwambie kuna mtu hapo chumbani anamuona amevaa nguo nyeupe. Unaamka kwa mshituko unawasha taa,unamkuta amekodoa macho ka mtoto aliyeota ndoto ya Zimwi. Kuna siku akawa ana mawenge ya kulala chumba kingine yaani as if mume na mke wamegombana. Nikimuuliza anasema anakuja na kweli unashangaa baadae anaingie chumbani kulala anajikumbatisha.
Nikaona hapa huu msala. Hii ni mental health issue. Alipokuja kusepa ile kwenda kwao, nilianza kumkwepa hadi leo.