Ni msanii gani ambae unaona kabisa ana talent kubwa lakini anachukuliwa wa kawaida?

Ni msanii gani ambae unaona kabisa ana talent kubwa lakini anachukuliwa wa kawaida?

Jobless_Billionaire

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2022
Posts
3,106
Reaction score
8,101
Wakuu habarini..

Katika tasnia (nazungumzia music), kuna wasanii wana vipaji vikubwa sana ingawa namna wanavyochukuliwa na jamii inaweza kuwa kawaida tofauti na uwezo walio nao labda kutokana na kutokuwa na promo, na kuna wengine wana uwezo wa kawaida ila ndio hivyo tena wamefanikiwa kupenya.

Msanii kama ONE SIX ni miongoni mwa wasanii ambao wana talent ya hali ya juu sana, vocal na melodies zake yuko poa sana. Ni msanii ambae nasujudu uwezo wake. Upande wa chorus ndio hafai hata kidogo. Ameshafanya chorus kwenye baadhi ya nyimbo za wasanii na ameua sana mfano wimbo wa
• Baba ft stamina
• I'm sorry ft Stamina,
• Mkombozi ft Roma
• Anaitwa Roma ft Roma
Na nyingine nyingi

Pia zipo alizofanya peke yake kama I feel na Mama don't cry. Kuna session moja aliwahi kuifanya Nadhani ni EATV alikuwa akiimba live, nilimpa salute sana.

Jinsi anavyoimba, sauti yake kwa asilimia fulani ipo kama ya Nyashinski.

Nilichoshindwa kujua tu ni kwanini hazungumzwi sana kama baadhi ya wasanii wanaoimba makelele tu na wanasumbua kitaani. Sina haja ya kuwataja hao watu, nadhani kila mmoja anajua kuwa kuna wasanii ni overrated kwenye game na wengine ni Underrated mfano huyu One Six toka pande za Dodoma.

Kwako ni msanii gani unaona ana uwezo mkubwa lakini hazungumzwi sana?
 

Attachments

  • images (33) (23).jpeg
    images (33) (23).jpeg
    35.2 KB · Views: 3
  • images (33) (22).jpeg
    images (33) (22).jpeg
    22.3 KB · Views: 4
shusho yule dada anasauti tamu!
 
Jobless billionaire ana kipaji sema tu watu wanamu underrate
 
Back
Top Bottom