Ni msanii gani wa Kenya anakubalika sana Tanzania?

Just Distinctions

JF-Expert Member
Joined
May 5, 2016
Posts
3,230
Reaction score
6,742
Habari zenu Wakuu, natumai mko poa bila kupoteza muda niende kwenye mada nikirejea uzi uliopostiwa na Member mmoja humu hapa juzi kati akionyesha clip ambayo inamuonesha msanii wa bongo kama sikosei ni aslay akiwa kajaza umati wa watu huko kenya,

huu uzi ulileta mjadala kiaina humu ndani wabongo wakidai kuwa wabongo wanakubalika sana kenya ila hakuna mkenya anaweza kutua bongo na kujaza umati kama huo.

Hivyo taja msanii au celebrity yeyote yule wa kenya ambae Unahisi akitua bongo lazima iwe ni shida Hasa kitaa kwa jinsi anavyokubalika.

Mi naanza na Khaligraph Jones dah huyu jamaa namuelewa kinoma na wabongo wengi wanamkubali huyu akitimba tena bongo ni shida kwani hata iwe sh ngapi hela yangu natoa nikamwone tu, wewe je??
 
Ogaaah! Unajua mpka sasa hakuna Mkenya ambaye atakuja yy kama yy personal na show yake ajaze watu hapa bongo ni lazma awe wa kusapoti show ya mmbongo hawa akina Omondi,Nyashski na Sauti Sol ni lazma wakiitwa basi show itakuwa ya mmbongo SIO yao wao wanakuja kama supporter tyu
 
Shida ni hela pia kusema ukweli Tanzania pande ya hela wapo chini sana kuweza kuwahost wasanii wa Kenya lakini inakuwa ni kinyume na hapa Kenya Jinsi wabongo wengi wamenufaika kwa uwepo wa hela kwa wanakenya. As a matter of fact for any Tanzanian Musician to make it ama akubalike duniani lazima aingie Kenya aweze kupitishiwa kwa moto kama vile dhahabu hupitishiwa hadi ikakubalika.
 
Hata wapige bure hawawezi kujaza, njoo uangalie jinsi Wasafi wanavyojaza ktk show zao pamoja na kwamba entrance fee ipo juu, katika muziki Kenya ipo nyuma sana.
 
😂😂😂😂and here I thought bongolalas don't know any Kenyan. So there are others who EV. know Kenyan socialites. I know corazon kwamboka by name only. Najua vera na huddah pekee. My fav is vera sidika
 
Tatizo mfumo wenu wa ujamaa uliwadumaza kiasi kwamba huwa hamna uwezo wa kufurahia diversity, yaani mkielekeza pua kwa kitu kimoja, nyote mnamwagika humo. Unakuta mnao mtindo mmoja tu wa sanaa, na ili Mkenya atambulike huko lazima aimbe Kibongobongo ndio aeleweke.
Sisi huku tunafurahia kila aina ya mtindo, iwe Bongo au mitindo ya kwetu na ndio maana unaona wasanii wenu wakija wanakubalika, hatujafugwa kwenye zizi moja kama mbuzi.
 
Amini kwamba.
#DG
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…