Vodacom ndio wana latency ndogo, hata Halotel kama upo eneo zuri unapata 4G yao full sio wabaya, mitandao yote ya 3G na 4G ina local ping chini ya 80ms mingi inacheza 20 mpaka 30ms local.
Pia kama una 5G wote Tigo, Voda na Airtel watakupa Latency nzuri.
Kwa UK hapo ndio muhimu pa kuangalia maana si tu local ping bali route inayotumika, unaweza kuta ili uwasiliane na UK waya unatoka TZ, unaenda South Africa, upitie South America, Usa hadi UK, wakati Isp mwengine anakatiza katikati Africa anatokea Morocco Ulaya hiyo.
Hii Tigo nime ping Century link, Latency zaidi ya 300ms
View attachment 2717626
Nikipata mda nitakuchekia isp wengine kwa hio server.
Pia kama unacheza game ama kufanya kitu serious stability pia muhimu