NI MTAZAMO TU: ukiwa unakula macho yako yanatazama chakula kingine huwezi kufurahia kilichopo mezani kwako

NI MTAZAMO TU: ukiwa unakula macho yako yanatazama chakula kingine huwezi kufurahia kilichopo mezani kwako

Dogoli kinyamkela

JF-Expert Member
Joined
Nov 21, 2024
Posts
618
Reaction score
1,440
Ukiwa mezani unakula chakula chako,lakini akilini mwako na macho yakiwa yanatazama meza nyingine kamwe huwezi kusikia wala kufurahia ladha ya chakula kilichopo mezani kwako
Huo ni mtazamo tu msijenge chuki.

NENDA NA HII
Masomo na mafunzo ya namna ya kuishi na mwanaume,au wanaume wanapenda nini hawa mabinti walitakiwa wafundishwe na wanaume wenyewe. Kwa maana sisi wanaume tunaotaka kuoa ndio tunaojua tunataka kuoa mwanamke wa namna gani?

Na mwenye tabia zipi
Mfano: Ukichukua wanaume hamsini 50Ukawauliza wauliza wanatamani kuishi na mwanamke au kuoa mwanamke wa namna gani? 45 watakueleza vigezo vinavyofanana Na watano 4 watatoa sababu za ujana Kama anapenda matako, Shape, nk, Na mmoja 1 atasema aisee mkuu mimi nataka kuoa mwanamke mwenye akili kwajili ya watoto wangu, halafu niongeze mmoja mwenye makalio makubwa, na asiyejitambua kwajili ya starehe zangu binafsi hivyo.

Utagundua kina wanawake wanafaa kwa matamanio ya starehe za muda mfupi tu!

SASA
Hizi kitchen party sikuizi hazisaidii mabinti kuingia kwenye ndoa ipasavyo..Bali imekua ni miradi ya waendeshaji shughuli..natania tu msinimaindi. Hem fikiria kwenye shughuli anaye mfundisha binti namna ya kuishi na mume ni singo maza halafu ni kungwi mwenye hasira na wanaume atafundisha ama kushauri nini kwa binti ambaye anatakiwa kwenda kua mtii?

Kama sio kumwandaa mwanamke ambaye ni mkorogaji ambaye akishindwa atarudi nyumbani kwa babaye na kuanza kujiita strong woman kumbe moyoni ana msiba mzito tayari ni mtazamo mabinti msinichukie.

Jinsi ya kuishi na mume, na mume anapenda nini?

Haya ni mafundisho ambayo binti alitakiwa ajifunze kwa baba yake
Na ajionee ni kwa namna gani mama yake anamchukulia baba yake!

ANGALIZO
Wa mama wengi hujikuta hawana namna nzuri za kuwalea watoto wao wa kiume pia vizuri. Hii imepelekea wanawake wanaolea watoto wao wa kiume wengi kukosa msingi mzuri wa baba zao.

Maana;
BABA: Hutoa Maagizo ambayo ni Amri
MAMA: Hutoa hutoa sheria ambazo kazi yake ni kusimamia zile amri za baba kwa mtoto.

Hii imepelekea tumekua na vijana wengi wa hovyo wanaoendeshwa kwa hisia badala ya kutumia akili
Hawa ndio vijana wanatoa mpaka jasho kutuimbia nani Kama mama?Ukiwauliza kwanini unaimba hivyo?

Atakujibu eti ni kwasababu Mama amenibeba tumboni miezi 9! Heeh sasa ulitaka ubebwe na nani? Eti kanizaa kwa uchungu? Heeh kwani kuzaa kwa uchungu si ni fungu lao! Au we ulitakaje! Lakini yakishakua ni majitu mazima yamepata majukumu na ugumu wa maisha ndio yanaanza kuona kweli mwanaume ni mwanaume.!!

Ni Mtazamo tu na utani Maana kwajinsi wanawake walivyo waongo. Kama tabia waliyoshare na nyoka....inawezekana hata kuzaa hawapati huo uchungu wanaoukuza Natania wamama.

MWISHO
Mwanamke mwema mafunzo mazuri hupokea kwa baba yake... Na yeye akijionea picha halisi kutoka kwa mama yake?

Ndio maana kwenye familia ambayo mama ndio kiongozi na Mwenye nguvu kuliko baba hata Kama baba ndio mwenye pesa.. Lakini ikiwa mwenye sauti kubwa ni mama... Sio mahali pazuri pa kijana wako kukimbilia kuoa... Maana huyo binti anajichukulia picha halisi kwa mama... Na baba hana nguvu nzuri ya kumfunza mwanaye.

Huu ulikua ni MTAZAMO wangu tu
Msinijengee chukiii

Content created by : Dogoli kinyamkela
 
Back
Top Bottom