Pre GE2025 Ni mtu asiye kawaida anayeweza kuiamini hii tume ya uchaguzi isiyo huru

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Subira the princess

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2018
Posts
3,474
Reaction score
3,744
Wasalaam.

Ndugu zangu wadanganyika hakika sisi ni wadanganyika na tumekua tukidanganyika tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Hapo nyuma kulikua na chombo cha kusimamia uchaguzi kilichoitwa tume ya uchaguzi Tanzania ambapo viongozi wake wote walichaguliwa na mwenyekiti WA CCM na hivyo kuwajibika kwa mwenyekiti huyo Moja Kwa moja.

Mwaka jana hawa CCM chini ya mwenyekiti wao wakaja na kuongeza neno huru kwenye tume ile ile ya uchanguzi ambapo kuanzia mwenyekiti WA tume hyo ya uchaguzi isiyo huru mpaka wasimamazi ni wale wale waliochaguliwa na mwenyekiti WA CCM na wanawajibika kwake.

Tafakari yangu ni kwamba hapa tumepigwa hakuna tume huru ya uchaguzi bali kuna tume ya uchaguzi ya ccm ambapo wasimamizi wa uchaguzi Ni makada watiifu WA ccm na Si watu huru wa kutenda haki na kusimamia chaguzi. Ajabu ni kwamba hata wanaopita leo kuandikisha wapiga kura wapya Ni makada watiifu wa ccm waliovaa koti la tume huru ya uchaguzi huku wadanganyika wakiendelea kudanganyika kwamba kutakua na uchaguzi huru chini ya tume huru ya uchaguzi ya ccm.

Pia soma:Wajumbe wa Tume Huru kuteuliwa na Mgombea Urais uhuru wa tume upo wapi?
 
Mleta mada hilo jambo linajulikana, lkn bahati mbaya wadanganyika hawajali, wako bize na umbea, kudanga, kubeti na utani wa Simba na Yanga.
 
Uchawa pro ndio tatizo la Taifa hili kwa miaka mingi.
 
..uchaguzi serikali za mitaa utasimamiwa na wizara ya Tamisemi, mbayo Waziri wake ni Mh.Mchengerwa, ambaye ni mume wa binti wa Rais Samia Suluhu.
 
Muda ukifika wataondoka kwa aibu

Na historia yao itafutika na mahali Pao hapata onekana tena
 
Muda wao ukifika wataondolewa tu hakuna kinachodumu Sina mpango wa kupiga kura kwenye hayo maonesho
 
Wasalaam.

Ndugu zangu wadanganyika hakika sisi ni wadanganyika na tumekua tukidanganyika tangu kuanzishwa kwa vyama vingi vya siasa mwaka 1992. Hapo nyuma kulikua na chombo cha kusimamia uchaguzi kilichoitwa tume ya uchaguzi Tanzania ambapo viongozi wake wote walichaguliwa na mwenyekiti WA CCM na hivyo kuwajibika kwa mwenyekiti huyo Moja Kwa moja.

Mwaka jana hawa CCM chini ya mwenyekiti wao wakaja na kuongeza neno huru kwenye tume ile ile ya uchanguzi ambapo kuanzia mwenyekiti WA tume hyo ya uchaguzi isiyo huru mpaka wasimamazi ni wale wale waliochaguliwa na mwenyekiti WA CCM na wanawajibika kwake.

Tafakari yangu ni kwamba hapa tumepigwa hakuna tume huru ya uchaguzi bali kuna tume ya uchaguzi ya ccm ambapo wasimamizi wa uchaguzi Ni makada watiifu WA ccm na Si watu huru wa kutenda haki na kusimamia chaguzi. Ajabu ni kwamba hata wanaopita leo kuandikisha wapiga kura wapya Ni makada watiifu wa ccm waliovaa koti la tume huru ya uchaguzi huku wadanganyika wakiendelea kudanganyika kwamba kutakua na uchaguzi huru chini ya tume huru ya uchaguzi ya ccm.

Pia soma:Wajumbe wa Tume Huru kuteuliwa na Mgombea Urais uhuru wa tume upo wapi?
Naomba kabla ya uchaguzi watu wa tume ,kuundwa sheria ya kumuwajibisha kila mmoja kwa jina lake ,kama ni huru ,na iwe sheria kali
 
Mleta Mada, Ahsante sana kwa kuona mbali sana. Hili swali lipo vichwani mwa WATANGANYIKA kadhaa waliojipambanua toka miongoni mwa Wa -DANGANYIKA. Mchangiaji mwingine kasema sasa tufanye nini? Mie nasema, Je, kama wewe una akili kamili ni sii zuzu, ukadanganywa kwamba "fuata njia hii ni salama, hutaliwa na simba wala hutaangamia" Hali halisi ukijua kuwa sii kweli ni uwongo! Je, utakubali? Je, utakataa?
Pia mimi, huwa najiuliza, hivi ni kweli sisi WATANGANYIKA wote hatuna AKILI? Kama la, mbona tuko hivi? Tofauti kati yetu na mazuzu mbona ni ndogo sana? Au niseme, hivi sisi WAAFRIKA hatuna AKILI? Kama ni hapana, mbona tangu UHURU (1961) hadi leo mbona tupo na tuko hivi? Chukulia wenzetu (weupe) Malaysia, Singapore, n.k. waliotawaliwa na wazungu, mbona leo wapo mbali tu? Kuna methali moja yetu sisi Wazaramo inasema, " mtu mwenye tabia ya "Zilongwa mbali na zitendwa mbali" basi hujibiwa kwa vitendo, kwa methali moja pia yetu Wazaramo isemayo " Amani haiji bila ncha ya upanga/jambia" Hili ndilo jibu lililowatoa wote wenye AKILI pahala pabaya na kuwapeleka pazuri na kujengeana heshima. Pia ndiyo chanzo cha "WAO" kuwapatia KATIBA iliyo bora kabisa ya kuifuata na kuleta MAENDELEO. Kwani sasa kila mmoja wetu atafahamu faida ya kutenda haki, kusema ukweli na kuacha udanganyifu, hapo WA-DANGANYIKA automatic wataondoka! Pia, tawala kama hizi zilikuwepo, na tunasema, " Kila chenye chanzo, pia kina mwisho" Je, tusubirie huo mwisho, lini?
Au tuwe na mjadala wa WATANGANYIKA, wa -DANGANYIKA na WA-LAMBA ASALI?
Kumbe hili ni letu sote, hasa WAZALENDO, je, wapo? Hapa ni kuwa tuanze na imani yetu kwamba kila mmoja wetu tunawajibika kwa kuwa tunavyo vizazi vyetu bado vitaendelea kuishi kwa karne nyingi zijazo. Tuache ubinafsi, tufanye yote kwa kumwogopa Mwenye Enzi MUNGU. Lakini pia tuiogope kitu kinaitwa KARMA, hii itawakumba wengi wasitenda haki, waongo, waganganyifu, wenye imani na wasio na imani, haichagui. Mbaya zaidi, hufuata hata kwa watoto wao, wajukuu na inasemwa hadi kizazi cha "NNE" Hapa sifahamu neno kizazi cha NNE ni nini?
 
Hakuna tume hapo za ya wahuni wa ccm waliogwiza aina ya matokeo ya kutangaza.
 
..uchaguzi serikali za mitaa utasimamiwa na wizara ya Tamisemi, mbayo Waziri wake ni Mh.Mchengerwa, ambaye ni mume wa binti wa Rais Samia Suluhu.
Na aliapa mbele ya ma mkwe kwamba wapinzani hatapata hata Kata moja na alipigiwa makofi na kushangiliwa na WANACCM pamoja na mwenyekiti wa tume ya uchaguzi. Nakumbuka alichekulea tu
 
Mleta Mada, Ahsante sana kwa kuona mbali sana. Hili swali lipo vichwani mwa WATANGANYIKA kadhaa waliojipambanua toka miongoni mwa Wa -DANGANYIKA. Mchangiaji mwingine kasema sasa tufanye nini? Mie nasema, Je, kama wewe una akili kamili ni sii zuzu, ukadanganywa kwamba "fuata njia hii ni salama, hutaliwa na simba wala hutaangamia" Hali halisi ukijua kuwa sii kweli ni uwongo! Je, utakubali? Je, utakataa?
Pia mimi, huwa najiuliza, hivi ni kweli sisi WATANGANYIKA wote hatuna AKILI? Kama la, mbona tuko hivi? Tofauti kati yetu na mazuzu mbona ni ndogo sana? Au niseme, hivi sisi WAAFRIKA hatuna AKILI? Kama ni hapana, mbona tangu UHURU (1961) hadi leo mbona tupo na tuko hivi? Chukulia wenzetu (weupe) Malaysia, Singapore, n.k. waliotawaliwa na wazungu, mbona leo wapo mbali tu? Kuna methali moja yetu sisi Wazaramo inasema, " mtu mwenye tabia ya "Zilongwa mbali na zitendwa mbali" basi hujibiwa kwa vitendo, kwa methali moja pia yetu Wazaramo isemayo " Amani haiji bila ncha ya upanga/jambia" Hili ndilo jibu lililowatoa wote wenye AKILI pahala pabaya na kuwapeleka pazuri na kujengeana heshima. Pia ndiyo chanzo cha "WAO" kuwapatia KATIBA iliyo bora kabisa ya kuifuata na kuleta MAENDELEO. Kwani sasa kila mmoja wetu atafahamu faida ya kutenda haki, kusema ukweli na kuacha udanganyifu, hapo WA-DANGANYIKA automatic wataondoka! Pia, tawala kama hizi zilikuwepo, na tunasema, " Kila chenye chanzo, pia kina mwisho" Je, tusubirie huo mwisho, lini?
Au tuwe na mjadala wa WATANGANYIKA, wa -DANGANYIKA na WA-LAMBA ASALI?
Kumbe hili ni letu sote, hasa WAZALENDO, je, wapo? Hapa ni kuwa tuanze na imani yetu kwamba kila mmoja wetu tunawajibika kwa kuwa tunavyo vizazi vyetu bado vitaendelea kuishi kwa karne nyingi zijazo. Tuache ubinafsi, tufanye yote kwa kumwogopa Mwenye Enzi MUNGU. Lakini pia tuiogope kitu kinaitwa KARMA, hii itawakumba wengi wasitenda haki, waongo, waganganyifu, wenye imani na wasio na imani, haichagui. Mbaya zaidi, hufuata hata kwa watoto wao, wajukuu na inasemwa hadi kizazi cha "NNE" Hapa sifahamu neno kizazi cha NNE ni nini?
Mkuu naona umechanganya demokrasia na maendeleo kwa nchi za South East Asia yaani Malaysia na Singapore.
Singapore ilipelekwa ki tuten na Waziri mkuu mtangulizi hadi nchi ikanyoka,vivyo hivyo Malaysia.
Tofauti ya Malaysia ilikuwa inachuma fedha nyingi kutoka visima vyaa mafuta,wakati Singapore isiyokuwa na mafuta ikatumia nafasi yake kijogrofia kama senta ya kusafisha mafuta toka kwa majirani zake,na kituo muhimu cha biashara kubwa kubwa.
 
Back
Top Bottom