KERO Ni muda mrefu sasa taa za kuongoza magari za Kibasila, Chang'ombe hazifanyi kazi

KERO Ni muda mrefu sasa taa za kuongoza magari za Kibasila, Chang'ombe hazifanyi kazi

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
  • Tags Tags
    mataa
Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Mataa ya kuongozea magari katika eneo la Kibasila, Chang'ombe, yamekuwa hayafanyi kazi kwa muda mrefu sasa. Hali hii imesababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa barabara, huku baadhi ya madereva wakipita kwa kasi na kufanya eneo hilo kuwa hatari zaidi.

Changamoto ni kubwa zaidi kutokana na uwepo wa shule karibu na eneo hilo. Wanafunzi pamoja na watembea kwa miguu wanapata shida kuvuka barabara kwa usalama, jambo ambalo linaweza kuhatarisha maisha yao.

Tunaomba mamlaka husika zifanye matengenezo ya haraka ya mataa hayo ili kurejesha usalama barabarani na kuzuia ajali zinazoweza kutokea, hasa kwa wanafunzi na watumiaji wengine wa barabara.
 
Back
Top Bottom