chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 16,859
- 28,112
Kuna wimbi kubwa sana la kughushi nyaraka.
Mikoa kama Morogoro, Dar es salaam na kwingine imekithiri, cha kushangaza. Huduma ya wataalamu wa forensic, kama uchunguzi wa miandiko Jeshi la Polisi limewaweka Dar es Salaam tu.
Kama nyaraka imeghushiwa Tarime, Tandahimba, Kilimanjaro, Kagera, Dodoma, lazima ipelekwe Dar es salaam. Yaani nchi nzima inapeleka nyaraka Dar.
Hii si sawa kwa wakati huu serikali inaposogeza huduma karibu na wananchi.
Mashauri mengi yanakwama mahakamani kwa kusubiri mtaalamu aje atoe ushahidi, na mtaalamu anazidiwa, anazurura nchi nzima.