Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 37,630
- 47,434
Wingu la siasa za nchi yetu limechafuka kwa mijadala mbali mbali kuhusiana na maswala muhimu ya kitaifa yaliyoibuliwa na ripoti ya CAG pamoja na comments za wadau mbali mbali kuhusiana na ripoti hiyo.
Ripoti hiyo imegusia unaosemekana ni ufisadi uliotokana na mambo yanayohusiana na mikataba iliyopelekea ujenzi wa miradi ya maendeleo na ununuzi wa mali mbali mbali.
Kwa nyakati tofauti viongozi mbali mbali wa mihimili ya dola na vyama vya upinzani wametoa maoni yao kuhusiana na ripoti hiyo pamoja na maswala mengine ya kitaifa.
Maoni hayo yamepelekea kuibuka kwa mijadala mizito ambayo kwa ufupi nimeona suluhisho lake ni kuwa na Senate au Bunge la Mabwanyeye ambalo litasaidia kupunguza lawama lukuki inazotupiwa serikali na viongozi wakuu wa nchi.
Senate ni Bunge la juu ambalo wawakilishi wake hutokana na mikoa na sio majimbo ya uchaguzi.
Bunge hili huwa na majukumu yaliyogawanyika katika sehemu kuu tatu.
1. Kuidhinisha au kutoidhinisha mikataba iliyoingiwa na Rais kwa niaba ya Nchi.
2. Kuidhinisha au kutoidhinisha wateule wa Rais.
3. Kufanya uchunguzi na kutoa adhabu kwa viongozi wa serikali ambao wamefanya makosa mbali mbali dhidi ya nchi.
Mara nyingi senate hutumika kama mhuri kwa maamuzi yaliyofanyika na bunge la kawaida, na pia hupewa hadhi ya kikao cha bunge kinachochuja na kutolea maamuzi maazimio ya bunge kawaida.
Ukiangalia mambo yanayotajwa kama mapungufu katika ripoti ya CAG utaona kwamba kuna umuhimu wa kuwa na bunge hili ambalo litakua likichuja maazimio ya bunge la kawaida, kupitia tena miswada ya sheria, kupitia tena bajeti za wizara mbali mbali na kutoa ushauri kwa Rais.
Aidha lingekuwa jambo la heri kwa Taifa letu kama tungeweka sifa za kielimu ambazo zitawafanya maseneta kuwa na ubobevu katika maeneo flani ili kutoa michango na maamuzi yenye tija kwa Taifa.
Mfumo huu wa Bunge la Senate unatumika na nchi takriban 64 hapa Duniani na naimani kwamba kama tukiutumia utatusaidia sana na kupunguza lawama kwa serikali na viongozi wa kitaifa.