Ni Muda muafaka sasa Tanzania tuwe na Senate "Bunge la mabwanyenye"

Kenya wana senators, vipi unaweza kuwaita wale senators ni mabwanyenye?
 
Huoni kama ni gharama? You can’t be serious!!

Hiyo tija unayoizungumzia inaweza kupatikana na muundo huu huu tulionao sasa!
Sio lazima iwe gharama. Kwani huwezi kupunguza idadi ya majimbo kwa zaidi ya nusu ili pia uwe na nusu nyingine ya wawakilishi ambao ni senators! Ni utashi tu na tamaduni! US wana House of representatives na Senate ambao kwa pamoja wanatengeneza Congress, na wameweza kubalance gharama. Hata kama sioni tija kwa sasa bado kuna uwezakano wa kutoka unicameral na kuwa bicameral kwa gharama zilezile.
 
Kenya wana senators, vipi unaweza kuwaita wale senators ni mabwanyenye?
Walianza kuwa elected 2013 baada ya mabadiliko ya katiba,

Kuna aina mbali mbali za useneta, wa kurithi, kuteuliwa ama kuchaguliwa,

Ila msingi wa neno senate umetoholewa ukimaanisha an assembly of the senior,

Being an upper chamber of the legislature members wake wanategemewa kuwa wiser than those from the lower house.

Vyovyote vile utavyowaita au itavyokua naona kuna umuhimu wakawepo.
 
Hahaha sasa hao wote umewataja wana sifa, Babu Tale yupo successful kwenye Music industry so atachangua Arts, Musukuma ni businessmam kwenye madini na usafirishaji, Juakali kasomea sheria (nadhani) which ndo field muhimu sana kwa mbunge kujua sheria
 
Kwa elimu yangu naona kabisa suala la unicameral na bicameral systems lipo kwenye mabadiliko makubwa ya kikatiba na sio hizi hadithi za sokoni! Ni suala la unitary system versus federalism, je tupo tayari kwa serikali zinazojitegemea za majimbo? Sio suala rahisi la kuwa na the so called 'bunge la mwabanyenye'. It is complicated.
 
Hahaha sasa hao wote umewataja wana sifa, Babu Tale yupo successful kwenye Music industry so atachangua Arts, Musukuma ni businessmam kwenye madini na usafirishaji, Juakali kasomea sheria (nadhani) which ndo field muhimu sana kwa mbunge kujua sheria
Sio hivyo! Jamaa hajui kuwa anacho suggest ni total system overhaul na sio hao individuals na ambitions zao. Mimi sio constitutional law expert lakini naona kabisa haya yatakuwa matakwa ya katiba nyingine kabisa.
 
We don’t need a bicameral legislature.

It’s wasteful spending.
How is that so? Just pick a couple of "seniors", knowledgable and the experienced amongst the incumbent MPs, and give them tools to be senators. It does not have to be like Kenyan or Nigerian style, let us have our own.

Kwa mfumo tulio nao sasa mtu yoyote anaweza kuingia bungeni kwa kigezo cha umri na elimu ya chini kwa kupigiwa kura na wanajimbo. Mtu huyo sio tu anakwenda kuwakilisha mambo ya wapiga kura wa jimbo lake, lakini pia anaenda kuwa sehemu ya maamuzi ya kisheria na hata mambo makubwa ya maswala yanayohusu taifa. Hii inatoa fursa ya mtu kupewa haki na nafasi ya kufanya maamuzi, lakini hajaandaliwa kielimu na kiujuzi kuwa na weledi ya kufanya hivyo. Baraza la mabwanyenye linaweza kuwa dawa.

If we do a cost benefit analysis of the current arrangement, it is possible to see that we may be saving money but losing more that that.
 
Ulichowaza ni sahihi kabisa coz tushaona mara nyingi maamuzi ya bunge kwa kiasi kikubwa ni kupendelea serekali hata kama ni maamuzi ya kuumiza nchi.
 
Nimewaza tu kwamba tunahitaji kuwa na mawazo mbadala ya bunge lililopo sasa,

Hata hivyo kwakua nchi nzima hatuna mikoa zaidi ya 35 bajeti yake nayo haitakua kubwa kwani maseneta hawatazidi idadi ya mikoa.
Kwa kuwa ni dhahiri bunge letu halina faida yoyote, labda bunge lolilopo lifanyiwe marekibisho kwa kuwa na uwakilishi wa kimkoa badala ya majimbo na, pamoja na majukumu yake ya sasa, liongezewe hayo majukumu ya ki-senate uliyoainisha.

Hii itasaidia kupunguza gharama kwa kuwa na bunge dogo.
 
Ulichowaza ni sahihi kabisa coz tushaona mara nyingi maamuzi ya bunge kwa kiasi kikubwa ni kupendelea serekali hata kama ni maamuzi ya kuumiza nchi.
I have sometimes wondered if we even need this institution. Kama ni kutunga sheria, sheria zinaandikwa na serikali wao wanapelekewa kupitisha. Kama ni bajeti, bajeti inaandaliwa na serikali wao wanakutana zaidi ya miezi miwili kuipitisha.

Afadhali tuwe na bunge dogo sana lenye wawakilishi wawili toka kila mkoa watakaofanya haya kwa gharama ndogo.
 
Nimewaza tu kwamba tunahitaji kuwa na mawazo mbadala ya bunge lililopo sasa,

Hata hivyo kwakua nchi nzima hatuna mikoa zaidi ya 35 bajeti yake nayo haitakua kubwa kwani maseneta hawatazidi idadi ya mikoa.
Nakubali bungee la mabwenyenye ila nakubali wajumbe wake,kwani tatizo la wabunge walio ni umaskini wanaproject nyingi za kuwaingizia pesa halali na zisizo halali,wajumbe 35 watanunulia wote.wajumbe wawe watu wenye investment zinazo fikiabilion 50 na wastaafu Maris nawenyeviti wa chama vyenye wabunge kadhaa walio maliza muda wao
 
Npaka sasa tunao Wabunge Mabwanyenye kadhaa wakiwemo Bashiru na Polepole
 
Hahaha sasa hao wote umewataja wana sifa, Babu Tale yupo successful kwenye Music industry so atachangua Arts, Musukuma ni businessmam kwenye madini na usafirishaji, Juakali kasomea sheria (nadhani) which ndo field muhimu sana kwa mbunge kujua sheria
Babu Tale mafanikio ya kukaribiana na Diamond na kuwa janjajanja ndio yatumike kuleta mawazo chanya bungeni?

Musukuma hana elimu, hizo biashara za madini wapo wenye elimu ndogo kabisa wamefanikiwa uko kama Mzee Layzer hatuwezi kuwaleta bungeni. Hawawezi kutunga sheria wala kujadili hoja ya msingi. Ndio maana anachoweza Musukuma bungeni ni kuchekesha.

Lijualikali kasoma sheria ila hana career yeyote. Kadumu kuwa mwanasheria kwa muda gani, wapi na kashiriki kesi ngapi. Hana accomplishment muhimu ukiachana na degree yake.

Elimu, successful career, uwezo wa mtu binafsi na kipato lazima vizingatiwe. Sasa bunge likijaa vilaza, watu hoehae hata kodi hawajawahi lipa, ukiachana na degree hana kazi aliwahi fanya. Hapo mtegemee maajabu gani.
 
Mataga mnataka serikali za majimbo kama Marekani??
Nimewaza tu kwamba tunahitaji kuwa na mawazo mbadala ya bunge lililopo sasa,

Hata hivyo kwakua nchi nzima hatuna mikoa zaidi ya 35 bajeti yake nayo haitakua kubwa kwani maseneta hawatazidi idadi ya mikoa.
 
Tunahitaji serikali za majimbo, sio kila kitu kwenye nchi ya watu milioni 60 hadi tusubirie maamuzi yafanyike Magogoni au Chamwino.
Zamani ilikuwa Chato pia!
We don’t need a bicameral legislature.

It’s wasteful spending.
 
Kwa mfumo wa nchi nyingine huko wanaingia elites tu ambao watakua wanachuja maazimio ya Bunge la kawaida na kuyaboresha ili maamuzi yatayotoka yanakua bora zaidi.
Ndio mkuu huwezi kumkuta dogo graduate hana hata chumba cha kupanga eti anapewa mamlaka ya kutunga sheria za nchi.
Pale US mwanasheria akiwa mwanasiasa unakuta kawa Prosecutor wa jimbo kwa miaka kadhaa au kahudumu kampuni kubwa ya sheria na kuna kesi za kusisimua zilimfanya ajulikane uwezo wake. Mtu kama McCain alishiriki vitani Vietnam, ni veteran aliyekuwa anajua sana jeshi na alitumika mno kwenye Defense Budget. Bloomberg huyu billionaire na media tycoon atasaidia kujadili uwekezaji, kodi, regulations na mengine.

Mle ndani wote wana elimu na exposure, wako screened hakuna mkwepa kodi wala mwenye skendo. Sisi uku tuna wabunge wanakamatwa kwenye ujangili kesi hazisikilizwi mpaka leo.
 
Walioshika mpini wa kisu hawatakubaliana nawe, kumbuka yule mstaafu aliyeshauri matokeo ya uchaguzi yahesabiwe hadharani baada ya kuonja joto ya jiwe ya aliyemwachia kiti
 
Walioshika mpini wa kisu hawatakubaliana nawe, kumbuka yule mstaafu aliyeshauri matokeo ya uchaguzi yahesabiwe hadharani baada ya kuonja joto ya jiwe ya aliyemwachia kiti
Tukiamua itawezekana.
 
Kuwa na bunge effective ni muhimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…