Ni Muda muafaka sasa Tanzania tuwe na Senate "Bunge la mabwanyenye"

Nimewaza tu kwamba tunahitaji kuwa na mawazo mbadala ya bunge lililopo sasa,

Hata hivyo kwakua nchi nzima hatuna mikoa zaidi ya 35 bajeti yake nayo haitakua kubwa kwani maseneta hawatazidi idadi ya mikoa.

Kungekuwa na mifumo ya haki ya kuwapata hapo sawa, ila utashangaa yale yale majizi ya kura toka ccm ndio yanakwenda kuwa kwenye hiyo senate.
 
Ulichowaza ni sahihi kabisa coz tushaona mara nyingi maamuzi ya bunge kwa kiasi kikubwa ni kupendelea serekali hata kama ni maamuzi ya kuumiza nchi.

Kimsingi wabunge wengi huwa ni wa ccm kutokana na mfumo dhaifu/mbovu wa uchaguzi. Hivyo unakuta huko bungeni wengi wanaenda kwa mabavu ya serikali na sio kwa maamuzi ya wapiga kura. Kwa vyovyote wabunge wa hivyo ni lazima watalalia upande wa serikali, ili kulipa fadhila ya wao kuingizwa bungeni. Mfano mrahisi ni wabunge wengi wa bunge la safari hii, zaidi ya nusu wako bungeni kwa matumizi mabaya ya madaraka ya hayati Magufuli, na sio matakwa ya wananchi.
 
Wabunge wake wakiwa na uhusiano na CCM basi hakuna kitakachobadirika.. watapitisha madudu yale yale
 
Vile vile tunaweza kuondoa ma DC tukabakia na RC 's na DED's itapunguza gharama.
Tupunguze idadi ya wabunge kwa kila halimashauri kuwa na mbunge mmoja, pia tuondoe viti maalumu, after that tuanzishe baraza LA Senate. Gharama zitakuwa zimejifidia na fedha nyingi kuokolewa kuliko kuwa na waimba mapambio na kusinzia bila tija yoyote
 
Vipaji, elimu na kadhalika viambatane na uwezo wa siasa (ushawishi, uzoefu, charisma etc.), simtetei yoyote kati yao, ila hata hao waliosoma na kuingia straight bungeni wapo waliomudu, kina Silinde, Zitto, Mdee, muhimu ni uwezo tu, msukuma ukiacha lugha yake ya ucheshi mara nyingi amechangia kuonyesha sera mbaya zinazoharibu biashara hata kwenye kikao cha wafanyabiashara na Hayati Magu alichangia vizuri sana kupelekea mpaka Waziri atolewe, lijuakali alivyokua upinzani alisifiwa shida kahamia CCM, hata Mdee hutasikia akisifiwa sana tena

Sent from my SM-J510L using JamiiForums mobile app
 
Hii point ni ya muhimu sana.

Tunaweza kuachana na habari za ma DC tukatumia fedha za kugharamia ofisi za wakuu wa wilaya

katika kugharamia senate yetu. Ingelipa zaidi hata kama tungekuwa na maseneta 60. Linapokuja

suala la maslahi mapana ya taifa sometimes tusifikirie sana gharama
 
Tupunguze idadi ya wabunge kwa kila halimashauri kuwa na mbunge mmoja, pia tuondoe viti maalumu, after that tuanzishe baraza LA Senate. Gharama zitakuwa zimejifidia na fedha nyingi kuokolewa kuliko kuwa na waimba mapambio na kusinzia bila tija yoyote
Hili nalo neno. Nimeipenda sana hii
 
Kwa alichokisema Rais Leo ,

Bado ni muhimu tuwe na senate,

Kuna haja ya kuwa na kikao cha pili cha maamuzi ya kibunge.
 
Hatuhitaji mabunge mawili ya kitaifa. Mabaraza ya madiwani yawe mabunge ya mikoa yenye mamlaka. Federal government tayari
Kwa alichokisema Rais Leo ,

Bado ni muhimu tuwe na senate,

Kuna haja ya kuwa na kikao cha pili cha maamuzi ya kibunge.
 
Hatuhitaji mabunge mawili ya kitaifa. Mabaraza ya madiwani yawe mabunge ya mikoa yenye mamlaka. Federal government tayari
Una haki ya kutoa maoni ila sio lazima uwe sahihi.
 
Nadhani hii hoja yako ni ya msingi Sana,kwanza hilo bunge likiwa limetawaliwa na watu wenye uwezo kiuchumi na walio na elimu zao pengine litaweza leta hoja za kimapinduzi kwenye sekta mbalimbali.Na Ili kufanikiwa hili ni kufuta kabisa Viti maalumu bunge,Ili hizo nafasi wawe hao wabunge wa bunge la pili
 
Mambo kama haya ya tozo yangeliangaliwa Tena na Senate kama tungekuwa nayo.

Tukiamua tunaweza.
 
Mambo kama haya ya tozo yangeliangaliwa Tena na Senate kama tungekuwa nayo.

Tukiamua tunaweza.
Tukubaliane tu kwamba sisi wote as a nation, we are corrupt. Usitegemee kupata masenator watakaokuwa tofauti na hawa wabunge tulionao.

Hii habari ya tozo wabunge wangeweza kuizuia kama wangekuwa na utashi.
 
Idea nzuri lkni senate sio bunge la mabwanyenye ,la Hasha ,mantiki na historia yake ni bunge la wazee ambao wanafikiria mambo kwa utaratibu,na haliharakishwi,, Na seneti kazi yake ni kufanya kilicho sahihi sio kilicho maarufu, Yani "what is right is not always what is popular" ambayo ni tofauti na mabunge ya kawaida... Tatizo seneti hapa Tanzania ukiiweka tu wataingia watu wa ajabu ,tuweke hata kiwango cha elimu maana kwenye bunge la kawaida wabunge tunawazidi akili hata sisi wa kawaida..
 
Sasa wewe stroke mbona mnnapinga katiba mpya hiyo senete itapatikanaje?
 
Maoni hayo yamepelekea kuibuka kwa mijadala mizito ambayo kwa ufupi nimeona suluhisho lake ni kuwa na Senate au Bunge la Mabwanyeye ambalo litasaidia kupunguza lawama lukuki inazotupiwa serikali na viongozi wakuu wa nchi.

Hapa mimi pia naunga mkono, ma Senate hawa wanatakiwa kuwa watu wenye fikra huru zisizoegamia itikadi ya chama chochote wawe na sifa za kusema kweli daima, walipwe mishahara minono kama ya majaji na wateuliwe na wananchi wa maeneo yao moja kwa moja bila shindikizo la chama, serikali au imani yao.

Kifupi maseneta wawe ni watu wenye msimamo.
 
Kwenye rasimu ya warioba senete ni kama bunge la muungano wa Tanzania,
serekali
Macongress (2) ni mabunge ya tanganyika na zenji
 
Tukubaliane tu kwamba sisi wote as a nation, we are corrupt. Usitegemee kupata masenator watakaokuwa tofauti na hawa wabunge tulionao.

Hii habari ya tozo wabunge wangeweza kuizuia kama wangekuwa na utashi.
Kungekuwa na chances walau za kireview miswada kabla haijawa Sheria.

Ila kubakia na bunge ambalo Kila mtu anaweza chagua anayetaka,

Matokeo yake ndio kama hivi.
 
Kabisa mkuu ,

Tupunguze viti maalum na MaDC hawa waungwana wawepo.

Sio vibaya tukawa na mawazo mbadala baada ya kikao Cha kwanza Cha Bunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…