Cobra70
Senior Member
- Jan 2, 2020
- 178
- 376
Nawiwa kusema kila siku matukio ya ajabu ya kutisha na ya kikatiri yanazidi kuota mizizi nchini mwetu.
Sababu kubwa ya haya matukio yanatokana na msongo wa mawazo wa muda mrefu wenda mtu amefanyiwa hujuma, usaliti, magonjwa ya muda mrefu, kipato duni, kufukuzwa kazi, kukosa ajira, ugomvi wa mali, unyanyasaji, dhuluma na imani za kishirikina.
Hivyo kutokana na matatizo haya ya kisaikolojia imepelekea watu kukosa taarifa sahihi na watu sahihi (wataalam) ambao ni rafiki (wasiri) wa kuwapa njia sahihi au mbadala wa kutatua changamoto zao zinazowakabili na hivyo kupelekea kujidhuru au kuwadhuru wengine kwa njia ya kujiondoa au kuondoa uhai wa wengine.
Ki ukweli matukio haya ya mauaji yanamea sana na huko mbeleni hakuna mtu atakayekuwa salama mana watu wamebeba mengi mazito mioyoni mwao na pa kuyatua hawapajui.