Wadau ni matumaini yangu kuwa harakati za Christmas zimepita Salama na sasa tuelekee mwaka mpya na mambo mapya. Baada ya kuona serikali ikiungana na mameneja pamoja na waajiri (wamiliki wa migodi) kuwahujumu wafanyakazi wa migodini na kuhakikisha wanabakia kuwa kwenye Tabaka la wanyonge ili waendelee kunyongeka. Sasa ni muda muafaka kuunda umoja utakaowaunganisha wanaapolo wote nchi nzima na huo umoja wao uweze kuwa na majukumu yafuatayo:
(1)- Kubaini, kusajili na kuwaunganisha wafanyakazi wote walioajiriwa migodini ili kuyalinda maslahi yao ya kiuchumi na kijamii.
(2)- kupigania uboreshaji wa miahahara, posho,stahili zao nyinginezo pamoja na mazingira ya kazini kwa kufanya maongezi na kutumia njia nyingine za kisheria kwa majibu wa sheria za nchi.
(3)- Kusimamia na kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa migodini unalindwa pindi wawapo kazini.
(4)- kusimamia na kupigania uboreshaji wa maslahi ya kisiasa, kijamii, na kiuchumi ya wafanyakazi wa migodini na wasiokuwa kazini.
(5)- kuhimiza umoja na mshikamano miongoni mwa wafanyakazi wa migodini.
(6)- Kuanzisha na kusimamia mambo yote yanayolinda maslahi ya wafanyakazi wa migodini kwa mjibu wa sheria za nchi.
Ndugu wadau kumbuka hili kundi ni muhimu katika sekta ya madini na pia ieleweke kuwa ni kundi ambalo linafanya kazi katika mazingira hatarishi. Pamoja na mambo niliyoorodhesha hapo juu wewe kama mdau unaweza ukaboresha na kuchangia zaidi.
Karibuni kwa mchango..
By
Mwanaapolo anayejitambua.