Ni muda wa Kiswahili kutumika katika maelezo ya bidhaa na mabango elekezi

Ni muda wa Kiswahili kutumika katika maelezo ya bidhaa na mabango elekezi

Time Traveller

JF-Expert Member
Joined
Nov 16, 2016
Posts
314
Reaction score
303
Zaidi ya asilimia 95 ya watanzania wanazungumza kwa ufasaha lugha ya kiswahili, huku watanzania wanaozungumza kwa ufasaha lugha ya kiingereza ikiwa ni chini ya asilimia 20 tu.Sasa fikiria hii, umewahi kujiuliza kwa nini kuna utitiri wa mabango elekezi na mabango biashara yaliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza pekee huku walengwa wake wakubwa wakiwa wazungumzaji wa lugha ya kiswahili? haiingii akilini kabisa, kuna mahali tunakwama sana na inabidi tubadilike.

Inawezekana vipi bidhaa muhimu kama ya ya chakula ambayo walengwa wakubwa ni watanzania wazungumzaji wa kiswahili inawekwa maelezo kwa lugha ya kiingereza. lengo ni nini hasa? Tutabadilika lini? kwa nini hatukuzi lugha yetu? Tunasubiri nani aje kutuamsha? Ukitembea nchi zilizoendelea ambazo wananchi wake sio wazungumzaji wa lugha ya kiingereza kama vile Urusi, Norway, Korea Kusini, Japan, utastaajabu jinsi kila bidhaa na mabango ya maelekezo mbalimbali yamepambwa kwa lugha zao.

Kuna umuhimun mkubwa wa kuweka lugha ya kiswahili katika bidhaa kwani humrahisishia mtumiaji kuweza kujua hasa ni nini anachokwenda kutumia, kuna baadhi ya bidhaa za chakula na vinywaji zina vitu vimeongezwa ambavyo baadhi ya watu hawatakiwi kutumia lakini inakuwa ngumu kufahamu kwa sababu tu zimeandikwa kwa lugha ya kiingereza.

Zipo kampuni zinazojitahidi kuweka maelekezo ya lugha ya kiswahili ambayo imekuwa ahueni sana kwa watumiaji wao, mfano bidhaa za Rangi, dawa za mifugo,baadhi ya dawa za binadamu n.k, leo hii unaweza kununua bidhaa ya rangi ukachanganya mwenyewe na kupaka kwenye kuta kiurahisi kabisa kutokana tu na maelekezo yaliyowekwa kwa lugha rafiki.
IMG_20210927_171836471.jpg


Nitoe wito kwa shirika la viwango Tanzania ( TBS) kuja na masharti mapya kwa wazalishaji wa bidhaa. Ili bidhaa zako ziende sokoni sharti ziwe na malekezo kwa lugha ya kiswahili. matumizi ya kiswahili katika bidhaa yatasaidia kuongeza wateja, kutengezeza imani kwa walaji, kuongeza mauzo, kukuza lugha yetu, kuepusha migongano, huku ukiwapiku washindani wasiotumia kiswahili.
 
Back
Top Bottom