Daisy Llilies
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,017
- 2,158
Jirani yangu hapa ninapoishi ni watu wenye uwezo wao. Wote wawili walikua na taaluma na walistaafu. Walijenga nyumba ya ghorofa ya vyumba sita vya kulala. Nyumba ya nyuma walipangisha.
Miaka mitano iliyopita mzee alifariki. Mama ameachwa akiwa na miaka 60+ lakini ni mama wa kileo sana na pesa ipo. Sebuleni ana bar yenye pombe zote za dunia hii. Mama wa kuvaa track suit na kufanya jogging asubuhi kama dr Gwajima Waziri.
Watoto wote wana maisha yao. Mama anaishi na dada wa kazi, na gardener. Gari anaendesha mwenyewe. Mama ni ua kinalozeeka na uzuri wake.
Mama alipata ki ben10 kiko kwenye 40’s. Mama alianza kuishi maisha aliyoyakosa. Maana walisomesha watoto, wamejenga nyumba nzuri na baada ya yote mzee amefariki. Mama alianza kwenda vacation Madagascar, Seashells, Mombasa, Zanzibar you name it.
Wamedate na kijana kwa miaka mitatu. Ghafla mama aliugua. Dalili zote za maambukizi, homa kali lakini antibiotics hazitulizi homa. Baada ya vipimo mama anakutwa na HIV. Alilia sana. Mtihani ilikua jinsi ya kuwafahamisha watoto wake. Hata akiweka iwe siri, itaandikwa kwenye cheti cha kifo siku alifariki.
Wazee wengi hawajali maambukizi iwe ni baada ya kufiwa au kuachana. Wanawake wengi tukiwa kwenye menopause tunawa.za kuwa sitapata mimba.
Wanaume pia msione fahari ya kutumia viagra, hawa mabinti wana mambo mengi.