Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Ama kwa hiari (kupenda) au kwa lazima (shuruti) ni wakati muafaka sasa kwa majeshi ya Tanzania kuingia moja kwa moja uwanja wa vita (Full scale) huko DRC ili kurejesha amani na kuwafutilia mbali waasi wa M23. Sababu za kufanya hivyo zipo na kwa uchache sana nitaziweka hapa.
1. DRC ni jirani muhimu wa Tanzania akiwa mdau mkubwa zaidii wa Tanzania kibiashara kupitia bandari ya Dar. Hivyo kuzorota kwa amani ya DRC ni kuzorota kwa biashara ya bandari hapa Tz.
2. DRC ni mwanachama kamili wa jumuiya ya Africa mashariki, jumuiya ambayo kuwepo kwake kumechangiwa na juhudi za Tanzania huku jumuiya ikiwa na mikataba inayotamka kila mwanachama kusaidiwa kulindwa dhidi ya adui yoyote anayevamia au kuteteresha amani ya nchi mwanachama. Ni muda wa vitendo sasa.
3. Kwa kuwa hakuna mgongano wowote wa kimaslahi kama Tanzania itaingia kuisaidia DRC (Mpaka sasa hakuna nchi yoyote iliyokiri kuwasaidia waasi wa M23 (Japokuwa sote tunajua Rwanda ndio mhusika mkuu) na wakati huo huo Tanzania hatufungamani na waasi wa M23), hivyo uwanja upo wazi.
4. Historia ya Tanzania kujiingiza kwenye mizozo ya namna hii na kufanikiwa iko wazi. (Tanzania ilifanya hivyo 2013 huko huko DRC kwa kufurusha hao M23, na ilifanya pia hivyo kule kwenye visiwa vya Comoro).
5. Tayari askari kadhaa wa Tanzania wanaolinda amani huko DRC wanaripotiwa kutekwa na kuuwawa na waasi wa M23 katika kipindi hichi cha uchukuaji wa mji wa Goma. Tuna sababu ya kuchukua hatua!
6. Utawala wa DRC tangu kuondolewa kwa dikteta Mobutu mwaka 1997 mpaka leo hii umekuwa ni utawala rafiki na ndugu katika nyanja zote muhimu za kiserikali. Kama Tanzania itaamua kukaa kimya wakati huu DRC ikiteketea basi hakutakuwa tena na maana ya kuendeleza undugu na urafiki na DRC. Utakuwa ni unafiki kwa 100%.