Ni mwaka 2026 ila bado mwana JF unaruhusu mgeni alale chumba kimoja na mwanao?

Ni mwaka 2026 ila bado mwana JF unaruhusu mgeni alale chumba kimoja na mwanao?

Kuna jamaa mmoja alijizima data akazama nyumbani kwa braza ake usiku, akalabua kabinti cha kaka ake. Binti akapata mimba na alishazaa. Wenye nyumba walisafiri. Kwa hiyo mtu kula mto wa ndugu yake haoni shida, adhabu kali za kimila siku hizi hazipo. Zamani ukila ndugu unaweza kuawawa mchana kweupe au kulogwa kabisa ufe au uwe kichaa kwa kosa hilo
 
Pedophiles wataharibu watoto, tatizo mnadhania ni wahuni wahuni wa mtaani, hapana, ni watu wa karibu yako kabisa.

Watoto wengi wamebaki na childhood trauma hadi wamekuwa ukubwani

Hivi mnadhani watoto wa kiume machapati wanaanzia wapi? Wajomba zao wamerubuni na kulawiti watoto wenu.

Hivi mnadhani watoto wa kike kuukumbatia ufuska angali akiwa binti wa miaka 11, 12, 13, inaanzia wapi? Baba mdogo zao wamewabaka na kuwatishia

Kama unavyumba vyako viwili vya kualla hakikisha mgeni akusalimie jioni asepe au mtafutie gesti alale.
Magasho wengi ukisikiliza historia zao ,wengi waliharibiwa na ndugu ,wajomba ,baba wadogo ,binamu nk

Watoto hawalali na ndugu yeyote wakiwa kwangu na hata mtoto wa ndugu yangu akija kwangu analala peke yake ,ila wamama akili zao sijui zikoje huwa rahisi sana kuamini watu akiwa na watoto wake anawalaza sehemu yeyote wanajichanganya kwa pamoja bila wasiwasi.
 
hakika mkuu
 
Niliwahi kushuhudia Mjomba akifanya ngono na mtoto wa kike wa dada yake na si mara moja. Hadi leo yeye wala dogo hakuna anayefahamu kama nilikua nawaona.

Ukizingatia upande wetu wa mama kuna madem kadhaa na alikuwaga mchangamfu sana kwao hadi leo, huwa naamini kuna kadhaa alipita nao pia.

Hii ni moja kati ya vitu ambavyo nadhani nitakwenda navyo kaburini bila kuvisema mahala popote maaana inaweza ikasambaratisha ukoo na kuua baadhi ya watu kwa presha.
Plot twist unaweza dhani uyo mtoto wa kike ni victim, huenda kumbe ni yeye ndo alimtega mjomba kwa muda mrefu, mambo yakibumburuka lawama atatupiwa mwanaume, na jamii itam-consider mwanaume kama predator MastaKiraka
 
Kizazi cha nyooka na Mbwa.

Leeni watoto zenu vizuri, Mpunguze control, Utacontrol akiwa nyumbani vipi akiwa kwa marafiki? Vipi akiwa kanisani? Vipi akiwa kwenye dara dara?

Tuwekeze katika malezi P.
 
Utandawazi ndio umechangia kwa kiasi kikubwa haya mambo. Zamani tulikuwa tunalala pamoja bila kuona jambo hilo kama tatizo. Hata mashuleni, kuna kipindi kulikuwa na uhaba wa vitanda na magodoro, hivyo wanafunzi walilazimika kulala pamoja, lakini haikuwa sababu ya kutokea kwa matatizo kama haya.
Tatizo kubwa la sasa ni namna teknolojia na mitandao imefanya maudhui ya ngono kupatikana kwa urahisi sana. Kuna aina za porn zinazohusisha hata mazingira ya kifamilia kama “mama na mtoto”, “baba na mtoto”, “dada na kaka”, pamoja na maudhui yanayohusisha watoto na watu wasiowajua.
Mtu akizoea kutazama maudhui hayo mara kwa mara, anaweza kuanza kuona mambo ambayo ni mabaya na yasiyokubalika kama kitu cha kawaida. Kwa baadhi ya watu, hali hiyo inaweza kuchochea tabia hatarishi na uhalifu wa kingono.
Ndiyo maana tunahitaji kuwa makini sana na watoto, matumizi ya mitandao na aina ya maudhui wanayokutana nayo. Kulinda watoto si jukumu la mzazi mmoja tu; ni jukumu la familia na jamii nzima.
Umemaliza kila kitu Mungu tusaidie..
 
Hii ni mbaya sana wamama tuwe karibu na watoto wetu sana hao wa kuitwa ma anko ni hatari..kuna mtoto wa binamu nilimwambia ww usimbusu mwanangu aisee...yani akimbeba tuu alikua anambusu busu..yani mara shavuni mara kwny paji la uso ..nikasema hapana nikamtolea uvivu..nikamwambia iwe mwanzo na mwisho kumbusu busu mwanangu halafu wa kiume hata angekua wa kike kwanini umbusu busu? Baba yake tuu huwezi kumkuta anambusu...kwanza sijawahi ona...akanuna nikasema sawa unakuta mtu mtaani kabeba katoto ka watu janaume zima ni kumbusu busu tu mtoto mie huwa kama namfahamu mama ake naenda namwambia fulani usimpe mtoto wako maana ukute linavuta hisia zingine....
 
Aisee. Pole sana. Shetani ana mawakala kila kona.

Umakini kwenye malezi na usimamizi unahitajika,muhimu zaidi kuanza kuwafundisha kuhusu Mungu mapema ili wawe na uwezo kiroho wa kuchuja mbivu na mbichi. Neema ya Mungu izidi kuwafunika!
 
Plot twist unaweza dhani uyo mtoto wa kike ni victim, huenda kumbe ni yeye ndo alimtega mjomba kwa muda mrefu, mambo yakibumburuka lawama atatupiwa mwanaume, na jamii itam-consider mwanaume kama predator MastaKiraka
Yaani kabisa unajitetea mahakamani kwamba "Mheshimiwa hakimu sio kosa langu ni yeye ndiye alikuwa ananitega nikajikuta nimembaka".
Utetezi dhaifu sana huu!
 
Back
Top Bottom