Ni mwaka 2026 ila bado mwana JF unaruhusu mgeni alale chumba kimoja na mwanao?

Kuna jamaa mmoja alijizima data akazama nyumbani kwa braza ake usiku, akalabua kabinti cha kaka ake. Binti akapata mimba na alishazaa. Wenye nyumba walisafiri. Kwa hiyo mtu kula mto wa ndugu yake haoni shida, adhabu kali za kimila siku hizi hazipo. Zamani ukila ndugu unaweza kuawawa mchana kweupe au kulogwa kabisa ufe au uwe kichaa kwa kosa hilo
 
Magasho wengi ukisikiliza historia zao ,wengi waliharibiwa na ndugu ,wajomba ,baba wadogo ,binamu nk

Watoto hawalali na ndugu yeyote wakiwa kwangu na hata mtoto wa ndugu yangu akija kwangu analala peke yake ,ila wamama akili zao sijui zikoje huwa rahisi sana kuamini watu akiwa na watoto wake anawalaza sehemu yeyote wanajichanganya kwa pamoja bila wasiwasi.
 
hakika mkuu
 
Plot twist unaweza dhani uyo mtoto wa kike ni victim, huenda kumbe ni yeye ndo alimtega mjomba kwa muda mrefu, mambo yakibumburuka lawama atatupiwa mwanaume, na jamii itam-consider mwanaume kama predator MastaKiraka
 
Kizazi cha nyooka na Mbwa.

Leeni watoto zenu vizuri, Mpunguze control, Utacontrol akiwa nyumbani vipi akiwa kwa marafiki? Vipi akiwa kanisani? Vipi akiwa kwenye dara dara?

Tuwekeze katika malezi P.
 
Umemaliza kila kitu Mungu tusaidie..
 
Hii ni mbaya sana wamama tuwe karibu na watoto wetu sana hao wa kuitwa ma anko ni hatari..kuna mtoto wa binamu nilimwambia ww usimbusu mwanangu aisee...yani akimbeba tuu alikua anambusu busu..yani mara shavuni mara kwny paji la uso ..nikasema hapana nikamtolea uvivu..nikamwambia iwe mwanzo na mwisho kumbusu busu mwanangu halafu wa kiume hata angekua wa kike kwanini umbusu busu? Baba yake tuu huwezi kumkuta anambusu...kwanza sijawahi ona...akanuna nikasema sawa unakuta mtu mtaani kabeba katoto ka watu janaume zima ni kumbusu busu tu mtoto mie huwa kama namfahamu mama ake naenda namwambia fulani usimpe mtoto wako maana ukute linavuta hisia zingine....
 
Aisee. Pole sana. Shetani ana mawakala kila kona.

Umakini kwenye malezi na usimamizi unahitajika,muhimu zaidi kuanza kuwafundisha kuhusu Mungu mapema ili wawe na uwezo kiroho wa kuchuja mbivu na mbichi. Neema ya Mungu izidi kuwafunika!
 
Plot twist unaweza dhani uyo mtoto wa kike ni victim, huenda kumbe ni yeye ndo alimtega mjomba kwa muda mrefu, mambo yakibumburuka lawama atatupiwa mwanaume, na jamii itam-consider mwanaume kama predator MastaKiraka
Yaani kabisa unajitetea mahakamani kwamba "Mheshimiwa hakimu sio kosa langu ni yeye ndiye alikuwa ananitega nikajikuta nimembaka".
Utetezi dhaifu sana huu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…