Ni mwaka 2026 ila bado mwana JF unaruhusu mgeni alale chumba kimoja na mwanao?


Bora tusiwe tunatembeleana tu kama ndo tumefika hii hatua.

Kila mtu alale kwake, Sheria zipitishwe 😌
 
Unajenga hoja ya chuki na malezi yako inaonyesha ni low class, uswahilina na utovu wa nidhamu.

Maisha hayo nimelelewa na ndugu zangu, familia moja inakaa nyumba moja na wote na maadili.
Huyo uncle , baba mdogo ama mkubwa ni utovu wake wa nidhamu , ambao amelelewa kama wewe usiye na nidhamu.
Kwanini haya mambo tunayasikia Buza, Temeke , Mbagala, Chanika, na hatuyasikii Mbweni JKT, Masaki , Mikocheni, Oysterbay?

Ushaona bango la nguvu za kiume Masaki , Oysterbay au Mbezi?

Endeleeni na umaskini wa Fikra.
 
Una X-ray machine ya kuimulika nia ya mtu?

Huko Mbweni,Masaki n.k kuna ufinyu wa malazi kwa wageni kwenye makazi ya wakazi wa huko?.

Hata kama una hofu ya Mungu ni ujinga kuamini kwamba kila mtu ana hofu ya Mungu kama ulivyo wewe!
 

Wazee wa kutupa lawama hao.
Wao ni kila saa kunyooshea wengine vidole.

Kuna mmoja kasema watoto wa ndugu zake wakija kwake hawalali na watoto zake 🤣

Ila wakienda boarding school wanalala na watoto wa wazazi wasio wajua kabisa 🥲.

Hawa ndo wale wazazi walio tukataza tusicheze na watoto wao, Sasa tumekua maisha yanawafundisha vzuri watoto wao namna ya kuishi na watu.
 
Mbona sasa umeshasema mkuu, na mwanaukoo nimeshaona. Au tayari umeshaingia kaburini.
 
Una X-ray machine ya kuimulika nia ya mtu?

Huko Mbweni,Masaki n.k kuna ufinyu wa malazi kwa wageni kwenye makazi ya wakazi wa huko?.

Hata kama una hofu ya Mungu ni ujinga kuamini kwamba kila mtu ana hofu ya Mungu kama ulivyo wewe!

Issue sio ufinyu wa malazi issue ni kua Familia za Masaki ziko civilized kukiko za Tabata.

Tujenge Familia/Koo zetu katika Misingi mizuri kuepuka uthenge kama huo kuibuka kati kati ya Familia
 
Hongera mkuu. Ni kitu mbofu mtu kumbusu mtoto.....
 
Mwaka 47, mgeni ilikuwa anafikia na kulala kwa balozi wa nyumba 10, maana hakukuwa na nyumba nyingi za kulala wageni (guest houses) kuliko ilivyo sasa

Hii ilitokana na masimulizi ya matukio ya kuchuna ngozi, kunyonya damu na kuwaingilia kingono watoto

Siku hizi kuna guest house hadi za 15,000 yanini ukabanane kwa watu

Binafsi siruhusu mgeni kulala na watoto wangu, afterall nina chumba kwaajili ya dharula ya wageni
 
Na huo ndo ukweli
 
Issue sio ufinyu wa malazi issue ni kua Familia za Masaki ziko civilized kukiko za Tabata.

Tujenge Familia/Koo zetu katika Misingi mizuri kuepuka uthenge kama huo kuibuka kati kati ya Familia
Nimekuelewa Mkuu lakini binadamu ni kiumbe Tata Sana. Tahadhari muhimu bila kujali background na status!.

Hayo mambo yanachochewa na mengi ikiwemo Imani za kishirikina,maagano ya Giza n.k
Hata hivyo kuna tofauti kati ya mstaarabu na mtakatifu.
 
Ni Roho mbaya Tu hapa hakuna mambo makubwa hivyo, Sisi wengi tumekaa Sana kwa Ndugu wametusaidi hdmi tumefika hapa kama wangetutili Mashaka kama mnavyotaka nyie tusingetoboa
 
Big up sana mkuuu🔥🔥🔥
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…