Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Kijana hakutuma maombi popote azaliwe, unapoamua kuzaa kulea ni jukumu lako na sio kutia huruma au kufanya kama ni kujitolea for free kulea mtu, sababu ulizotaja hapo za hovyo, mtu keshamliza chuo unampigaje? Akili zako zitakua timamu?
 
Utadhan usipowapiga hawatokuja kufa, ni hv, mtu yeyote asivuke mipaka, iwe mzazi iwe mtoto, kua mzazi hakukupi tiket ya kufanya ujinga waliofanya hao wazee
 
Noted mkuu. Much respect for your time.
 
Noted mkuu. Much respect for your time.
Nimeshapitia hali kama yako Mkuu, jambo la kukushauri ishi na watu vizuri, usimdharau wala kumbeza mtu japo binadamu wana maudhi sana, saidia au toa msaada pale unapoweza hata kama ni sh 500 tu. Jingine Mama yako ana spirit inayomuendesha na ndiyo maana haiendani na spirit uliyokuwa nayo wewe. That's why her Spirit irritating mpaka alifikia hatua ya kukuonesha kwa vitendo hadharani. Roho zenu haziendani na Maza wako anatokea kwenye koo za Kichawi na hizo roho anatembea nazo lakini wewe roho uliyopewa na Mungu imekuwa ni ya kitofauti. Usiwaze sana maana ndio dunia ilivyo
 
Mkuu, Hakuna Mwanadamu mkamilifu. Nimetambua anguko langu la miaka mitatu iliyopita na nimeshaweka juhudi za kutosha kutafuta utatuzi na hivi bado naendelea Kupambania
pole sana Mkuu
tunajifunza kwa makosa bora ya wewe uliyetambua kosa lako na Mungu mwenyezi atakusaidia na hongera sana kwa jitahada zako kutafuta suluhu na wazazi wako ipo siku utafanikiwa .
 
Ashakum si matusi, wazazi wakapimwe mkojo.

Na kama umeisaka sana suluhu, hawataki na moyoni unaumia, mungu anaona yaliyomo ndani ya nafsi zetu, ishi maisha yako.. Usiache kuwatumia vijisent vidogo vidogo, huenda hii ikaleta suluhu
 
Ukampiga Mama
Kisha ukampiga teke Mzee.

Alafu Muda huohuo unasema Mamaako alikuwa Mkali KUPITILIZA mwenye kupenda Kúpiga na kupigana mpaka na Majirani na Mzee wako.

Unalaana ya Kurithi na àmbayo umeia-prove Kwa Kúpiga Wazazi wako

Mzazi hapigwagi hata Siku Moja.

Akikosea njia Bora zaidi NI kuondoka na kujitenga nao.

Wanasema Hasira hukaa vifuani mwa wapumbavu.

Ungekuwa hakuna sababu ñyiñgine ya maana Wala huna sababu ya kutaka uhûsiano na Wazazi wako na ukaendelea na mambo yako.

Ila Kwa Sasa unawahitaji zaidi ili kuwaomba Msamaha WA kile ulichokifanya. Yaani Hapo Fanya juu chini upate Msamaha waô.

Hasira za jinga hayo ndîo matokeo
 
Ashakum si matusi, wazazi wakapimwe mkojo.

Na kama umeisaka sana suluhu, hawataki na moyoni unaumia, mungu anaona yaliyomo ndani ya nafsi zetu, ishi maisha yako.. Usiache kuwatumia vijisent vidogo vidogo, huenda hii ikaleta suluhu

Huo ulikuwa mtihani mdogo tuu.
Yeye kafanya Kosa kûbwa, unaanzaje kumpiga Mzazi wako, mama na Baba yako.

Tenà Mtu aliyesoma Kabisa mpaka kufika chuo Kikuu. Unaanzaje kufanya Makosa Makubwa Kwa kiwango hicho?

Kama Wazazi wake amewapiga unafikiri Sisi Wengine atatufanya nini?

Hasira!

Kwamba Mtu anashindwa kudhibiti Hasira Zake Mpaka Kwa Mzazi wake?

Kijana anamatatizo Makubwa kuliko Stori na mambo yaliyomtokea
 
Niliwahi kukutana na situation inayofanana na hii kidogo,ila mimi tulifikia kubwatizana na mzee wangu,na baada ya siku mbili nikaamua kuondoka ingawa mimi nilikuwa na kazi yangu tayari,hata hivyo kilichonipelekea kuishi tena nyumbani ni umri wa mzee ulikuwa umekwenda kiasi kwahiyo ndugu na marafiki walinishauri nikaishi naye.Baada ya mimi kuondoka ilipita kama miaka 2 hatukua na mawasiliano kabisa,ile hali ilikuwa inaniumiza sana rohoni.Siku moja nilikutana na rafiki yangu ambaye alinisihi sana nijishushe ili yaishe,ilibidi niingie kwenye maombi ya kuomba Mungu ili anipe ujasiri wa kumface tena mzee,siku isiyo na jina,nilienda mpk nyumbani,nikagundua kuwa hata yeye kumbe alikuwa amenimiss sana,maana alinikumbatia aliponiona,tukakaa pamoja,nikaomba radhi kwa yaliotokea,akanisamehe na so far tuko naye vizuri sana.Kwahiyo kama inawezekana kwa hili la kwako ningekushauri umgeukie Mungu,usitumie akili zako mwenyewe kwani inaonekana wazazi wako kidogo ni watata,kwakuwa Mungu anajua dhamira yako ni kutafuta suluhu,yeye atakuwa tayari ameshakusamehe,na kwa neema yake atakufungulia mlango ambao utalifanya jambo hili kuisha na yote yakapita...
 
Wazazi ni kitu chengine hapa ulimwenguni na hakuna mbadala wake. Uliwakosea. Mzazi hapigwi.
Tumia mbinu zote ikiwa ni pamoja na KUOMBA lakini wakusamehe!
 
Huwezi kuwalipa mazuri waliyokufanyia wala hayo matukio sii kipimo cha ubaya walio nao. Pamoja na mapungufu ya wazazi wako, shika amri ya Mungu

Waheshimu baba na mama
 
Unaweza vipi kumtwanga kofi mamaako au kumpiga babaako hautafanikiwa kwa lolote na ukifa ni motoni fanya ufanyavyo usuluhishwe hili kabla ujakata moto
 
Kijana hakutuma maombi popote azaliwe, unapoamua kuzaa kulea ni jukumu lako na sio kutia huruma au kufanya kama ni kujitolea for free kulea mtu, sababu ulizotaja hapo za hovyo, mtu keshamliza chuo unampigaje? Akili zako zitakua timamu?
wahenga walisema mtoto kwa mzazi hakui mtoto atabaki mtoto tuu hata uwe na miaka mingapi.

Kumaliza chuo na miaka 24 tayari unajiona mkubwa maisha ni safari ndefu hapo bado hujawa na watoto na wajukuu ,nyie ndio kizazi Cha mabus ya njano mmeanza maisha ya kujitegemea , mlikuwa mkipanda daladala na mabegi ya shule mnakaa kwenye siti hamtaki kupisha wakubwa eti mmechoka Leo mmemaliza chuo mnaanza kuhesabu mabaya ya wazazi ,mngeishi kwenye makazi ya watoto yatima mngekuwa na jeuri hiyo acheni shisha ,Bangi na pombe zisiwatoe ufahamu kama imetokea ukalelewa na mzazi mkatili vumilia ukianza kujipata ondoka nyumbani kwa amani ,usifanye kosa la kutunishiana msuli na wazazi wako eti haukuomba kuja Duniani , wewe utajisikiaje ukipata watoto na wajukuu wako wakaanza kukwambia maneno hayo kwamba hawakuomba kuzaliwa utawaelewa?

Ni bahati mbaya sana kulelewa na wazazi wakatili , wapo watoto wengi tu innocent wakajikuta wanachukiwa na wazazi wao kwa sababu mbalimbali hasa wanazozijua wazazi wenyewe , ukiwa na wazazi wa namna hiyo ni msala usiweke kinyongo jiwazie future Yako wakati upo chini yao , utakuwa umepata fundisho jinsi ya kulea familia Yako tofauti na ulivyolelewa wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…