Niliwahi kukutana na situation inayofanana na hii kidogo,ila mimi tulifikia kubwatizana na mzee wangu,na baada ya siku mbili nikaamua kuondoka ingawa mimi nilikuwa na kazi yangu tayari,hata hivyo kilichonipelekea kuishi tena nyumbani ni umri wa mzee ulikuwa umekwenda kiasi kwahiyo ndugu na marafiki walinishauri nikaishi naye.Baada ya mimi kuondoka ilipita kama miaka 2 hatukua na mawasiliano kabisa,ile hali ilikuwa inaniumiza sana rohoni.Siku moja nilikutana na rafiki yangu ambaye alinisihi sana nijishushe ili yaishe,ilibidi niingie kwenye maombi ya kuomba Mungu ili anipe ujasiri wa kumface tena mzee,siku isiyo na jina,nilienda mpk nyumbani,nikagundua kuwa hata yeye kumbe alikuwa amenimiss sana,maana alinikumbatia aliponiona,tukakaa pamoja,nikaomba radhi kwa yaliotokea,akanisamehe na so far tuko naye vizuri sana.Kwahiyo kama inawezekana kwa hili la kwako ningekushauri umgeukie Mungu,usitumie akili zako mwenyewe kwani inaonekana wazazi wako kidogo ni watata,kwakuwa Mungu anajua dhamira yako ni kutafuta suluhu,yeye atakuwa tayari ameshakusamehe,na kwa neema yake atakufungulia mlango ambao utalifanya jambo hili kuisha na yote yakapita...