Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Akiwa anajiandaa anipige tena, nilimshindilia teke la Kifua Mithiri ya Mtu aliedhamiria kuvunja mlango uliokataa kufunguka mara kadhaa, akadondoka chini.
🤣🤣🤣🤣🤣


Mzazi hapigwi
Mzazi ni mzazi..

Usitume watu kukuombea msamaha Kwa kipondo ulichowapa..nenda mwenyewe.

Ipo siku hutakuwa na wazazi
Utawakumbuka sana,
Unatamani wangekuwepo,hata kama walikuwa wamekukosea..
Tengeneza sasa angali wapo.
 
Ushauri huu umemaliza kila kitu,uzingatie
 
Ingia kwenye maombi ya kufunga na kutoa sadaka ukimuomba Mungu aingilie kati hili jambo ili kukupatia Amani, amini nakwambia jibu litapatikana pasipo nguvu ya kibinadamu, Yeremia 33:3 Mungu anasema “mniite nami nitaitika, nitawaonyesha mambo Makubwa na Magumu msiyoyajua”
-Kama kuna upepo mbaya uliwapitia basi Mungu atawaunganisha kwa njia zake mwenyewe.
 
Pole kijana!
Naamini hukuwapiga wazazi kwa kutaka bali ilikuwa ni hasira ya kunyanyaswa nao kwa muda mrefu! Hata kama ni Wazazi kwa upande mmoja walikosea.
Maadamu ulichukua hatua zote za kuwaomba radhi Wazazi lakini hawakutaka,huna hatia mbele za Mungu.
Kwa namna ile ulivyomwomba Mungu akufungulie mlango ukiwa katika hali mbaya mpaka akakupa ufunuo wa kumkumbuka huyo dada ambaye amefanyakazi kama Msamaria,piga magoti mbele za Mungu umwombe akusaidie jinsi ya kupatana na wazazi wako! Na kwa hakika atafanya.
Huyo dada mheshimu hata kama Shetani atakupitia usithubutu kufanya ngono naye.
Lakini huwezi kujua mipango ya Mungu huenda huyo binti akawa ni Mwenzi wako wa Maisha.
Hata hili mwombe Mungu akupe ufunuo ujue kama ndiye wako wa maisha.
Mwisho fanya juu chini hakikisha unatafuta chumba chako mwenyewe! Nguo ya kuazimwa haistiri uchi.
Nakutakia maisha mazuri kijana.
 
Kijana nenda kwa afisa maendeleo jamii wilaya wanayoishi wazazi wako kawaombe wakusaidie kupatana na wazazi wako pia shirikisha viongozi wa dini wanakosali wazazi wako tafuta nenda kawaangukie wazazi wako.

Huyo mdada aliyekusaidia endelea kumheshimu sana muone kama dada Yako mkombozi wako, mpe heshima na dakitari boy friend wake ,usijaribu hata Kwa utani kumtongoza huyo binti alikusaidia kiubinadamu hiyo couple waweke kama ndugu zako .

Endelea kuomba toba kwa kuwapiga wazazi wako Hilo lilikuwa kosa kubwa sana ulifanya ,wapo baadhi ya wazazi madikteta inakuwa wako hivyo usiwatenge hao ndio wazazi wako wamekulea wamekusomesha mpa umepata degree na watakuwa yapo wamekufanyia mazuri wewe unaanza kuwahesabia mabaya baada ya kuona umeelimika na kujiona unayaweza maisha ,jishushe sana ukipata nafasi tena kuwaona wazazi wako kawaombe msamaha hata kwa kijutia kwa machozi na kugalagala chini ,jiulize wanao wakija kukuuliza kuhusu Babu na bibi Yao utawajibu vipi ,vp kuhusu mkeo utakaye kuja kumuona unafikiri ukoo wao watakuelewa vipi kama utakuwa umeshindwa muafaka na wazazi wako he usalama WA Binti Yao utakuwa upi?

Nakutakia Kila la kheri kwenye kuyajenga na wazazi wako na maisha yako Kwa ujumla.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…