Kijana nenda kwa afisa maendeleo jamii wilaya wanayoishi wazazi wako kawaombe wakusaidie kupatana na wazazi wako pia shirikisha viongozi wa dini wanakosali wazazi wako tafuta nenda kawaangukie wazazi wako.
Huyo mdada aliyekusaidia endelea kumheshimu sana muone kama dada Yako mkombozi wako, mpe heshima na dakitari boy friend wake ,usijaribu hata Kwa utani kumtongoza huyo binti alikusaidia kiubinadamu hiyo couple waweke kama ndugu zako .
Endelea kuomba toba kwa kuwapiga wazazi wako Hilo lilikuwa kosa kubwa sana ulifanya ,wapo baadhi ya wazazi madikteta inakuwa wako hivyo usiwatenge hao ndio wazazi wako wamekulea wamekusomesha mpa umepata degree na watakuwa yapo wamekufanyia mazuri wewe unaanza kuwahesabia mabaya baada ya kuona umeelimika na kujiona unayaweza maisha ,jishushe sana ukipata nafasi tena kuwaona wazazi wako kawaombe msamaha hata kwa kijutia kwa machozi na kugalagala chini ,jiulize wanao wakija kukuuliza kuhusu Babu na bibi Yao utawajibu vipi ,vp kuhusu mkeo utakaye kuja kumuona unafikiri ukoo wao watakuelewa vipi kama utakuwa umeshindwa muafaka na wazazi wako he usalama WA Binti Yao utakuwa upi?
Nakutakia Kila la kheri kwenye kuyajenga na wazazi wako na maisha yako Kwa ujumla.