Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Nakazia huu ni ushauri mzuri sana
 
Tuwaheshinu sana wazazi lakini I'm sorry Kwa situation Yako ningekuwa Mimi ningewapa vitasa zaidi, ningewabonda haswa.... Km msamaha wao ndo wamenikosea wanitafute waniombe msamaha... Why unichape uchi? Mimi mtu mzima unanipiga makofi! Why?
 
Kwenye hadithi muhusika ni km anateswa nq hiyo hali ya kutokuwepo maelewano na wazazi wake, ila angekuwa na maamuzi magumu km kina sie aaah unanyamaza km washakuzika
Yaani mm hata muda wa kumtukuza mzee sina kila mtu kala hamsini zake. Maisha yanasonga na nikikwqma sio sababu sijapewa baraka na mzazi wala radhi zake natafutaga sababu zingine za kujijibu. Mzazi sio mungu, kama kuna mzazi humu anaamini kuwa mwanae hawez kufanikiwa kama yeye hataki atakula za uso siku yoyote! HATAAMINI
 
Nashukuru sijapata mzazi ksma wa hadithi hii, ila ndg wa wazazi wa huo umungu mtu wa kujipa umuhimu, mbaya zaidi enzi za utotoni hawakuwepo saiv ndo wananiletea hizo swaga😅😅😅😅nawafurahisha na nilivyo mjeuri hebu kwanza nicheke😅😅😅😅😅😅
 
Efeso 6: 1-9

Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi, Upate heri, ukae siku nyingi katika dunia. Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maonyo ya Bwana.

USHAURI WANGU
Fanya NOVENA YA SIKU 9 na kufunga ukiomba msamaha kwa Mungu.

Umeishi katika mateso kwa muda mrefu sana. Maandiko hayo yako upande wako. Mweleze Mungu msamaha wako. Kuhusu huyu Dada aliyekusaidia usijaribu kufanya naye mapenzi kufanya hivyo utakuwa umejiharibia milele. Baada ya kufanya NOVENA SIKU 9 mtafute mtu ambaye Baba yako anamheshimu sana mweleze na umuombe akuongoze kwenye zoezi la mtoto mpotevu kurudi nyumbani. Muonyeshe Baba yako kuwa aliyoyasema unayaona. Kwa tukio hili Mungu amekuweka kwenye mizani jitahidi kurudi nyumbani kwa wazazi. Katika Jina la Yesu Kristo wa Nazareti UTASHINDA. AMEN.
 
Na kweli ni maelezo marefu mda unaponya endelea kutafuta maisha baada ya mda hali itakaa sawa na mtaendelea kuwa na mahusiano mazuri na hao wazazi wako
Pole kwa mkasa/Mikasa. Ila lugha, ndio mitihani. Adi x Hadi ✓,, kuludi x kurudi ✓ . Lakini pia kumpiga mzazi haijalishi amekukosea vipi ni mbaya kwako. Sijasoma hadi mwisho ila NJ hadithi nzuri.
 
USHAURI WANGU:
1.
Tafuta pesa kwa bidii, save na uwe na mipango..ukifanikiwa watakutafuta wenyewe.

2. Usikimbilie kumla huyo mdada utaharibu.
Kuna wakati mtu ni mzuri sana mkiwa marafiki, mkiingiza mapenzi kuna mdudu wivu anaingia, mkiparangana na urafiki unakufa.

Chagua lililo jema
 
Asante sana, Kwa Ushauri Wa kujenga
 
Asante sana
 
kipindi, kilikua Kigumu zaidi kuliko kipindi chochote Cha maisha yangu. Nilizoea kuishi maisha ya shule ambayo kula uhakika na kulala uhakika. pia Chuo nilisaidiwa sana na wazazi na pia boom lilinifanya niweze kumudu maisha.
 
Dini zote zinafundisha kuwaheshimu wazazi ili siku zako zipate kuwa nyingi,pia mafundisho ya dini yanafundisha kama mzazi anamkosea mtoto wake,mtoto inakubidi uishi na kuongeana mzazi/ wazazi wako kama rafiki na kama kweli akifanya jitahada za ziada kama anavyoshauliwa hapa kupitia viongozi wa dini bado wazee wake watakataa kumsamehe basi awaage kwa heshima na amani akabidhi maisha yake Kwa Mungu akaendelee na maisha yake kwani wazazi na watoto wote ni Mali ya Mungu.
 
Ukweli ulikosea sana kuwapiga wazazi wako no matter walikukosea pakubwa kiasi gani
 
kipindi, kilikua Kigumu zaidi kuliko kipindi chochote Cha maisha yangu. Nilizoea kuishi maisha ya shule ambayo kula uhakika na kulala uhakika. pia Chuo nilisaidiwa sana na wazazi na pia boom lilinifanya niweze kumudu maisha.
umeona hapo anakiri wazazi walimsaidia na je anakumbuka mama yake alivyoangaika na ujauzito wake ,clinics, kunyonyeshwa ,kumnyea mama yake,kumtapikia mama yake na je kama mama yake angemtupa chooni Leo fadhila anayoiona kubwa ni kutoka mdada mshirika wa chuo aliyemsaidia matibabu na pocket money alivyokorofishana na wazazi wake kwa wazazi anachokumbuka ni kipigo TU sie wengine tulilelewa na kudundwa sana na wazazi wetu na pia walituonyesha upendo pia ile heshima ya wazazi ilitufanya tuwasitiri na makosa Yao kizazi cha sasa kikijifanya kujipima ubavu na wazazi wao jiandae kwa maisha ya fedhea na kuipambania fedhea kama sio fedhea utaipata kwenye jamii basi kwenye kizazi chako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…