Ni mwaka wa tatu nipo kwenye uadui mkubwa na wazazi wangu; siwasiliani nao wala sishirikiani nao kwa lolote

Kuna siku ilikuwa kidogo nimtoe roho wife, alidiriki kumpiga mtoto bao kubwa la kifua kisa eti amemchoma na kitana wakati anamchezea nywele. Nilisikia ‘puuh’, aisee..,
Nilipiga , kwakweli sijawahi piga mtu tena namna ile maishani mwangu, harudii tena kupiga watoto bila sababu. Mtoto aadhibiwe kwa sababu, si ujinga ujinga tu
 
Wewe ni dini gani?
Tafuta matu wa dini yenu nyumbani waelezee na uwatumie kutafuta suruhu na wazazi wako.

Ikishindikana hii mdogo wangu ishi maisha yako.
Tena kaa kimyaa na uwe msiri katika hatua zako na mambo yako.
 
I wish wanawake wote wa JF waisome hii na wajifunze kitu, si wao tu wanaopaswa kusaidika ktk mahusiano, bali hata wanaume nao wanahitaji msaada vilevike, wanawake wa kipindi hiki wamebase kivyao wamejawa tamaa kwakujiona niwao tu wanaopaswa kupewa, yaan wamejawa uchoyo hawajui kutoa zaidi ya kupokea.

Wanawake wa aina hiyo tajwa na mtoa mada kweli mebaki wachache sana, na ukikutana nae jichunge usiendekeze tamaa za kipumbavu,

wewe mtoa mada huyo mwanamke mheshimu kamwe usije kumtongoza wala usijekuwa chanzo cha mahusiano yake kuharibika, weka tamaa pembeni usijeharibu mambo, mfanye kama dada na ondoa hisia za mahusiano ya kimapenzi, bali jenga hisia za kindugu.

Usikubali kuwa ktk mahusiano naye labda atengane na mtu wake, wanawake wa aina hiyo ni wachache saanaa, ukimpata usimpoteze.

Kama ndugu walikukataa yeye akabaki nawewe why umpoteze?, kama wazazi, marafiki na washikaji hawakukusaidia lkn yeye kakupa mwanga wa maisha why umpoteze? Chunga moyo wako kijana, huyo Ndie malaika wako na mkombozi wa maisha yako, na wengine tunatamani tungekuwa na wanawake wa aina yako, lkn ndio vile tena.

Kama vipi mods, thread wailazimishe iwafikie members wote hasa wale wanaosemekana kuwa ni jinsia jike, waisome hii wajifunze kitu.

Alafu hao wazazi wako achana nao pambana na life lako, hawawezi kubadirika kama wangekuwa na moyo wa kubadirika, mzazi mwenye uchungu wa mwana hawezi ruhusu mwanae akateseke asikokujua hatakama kakosea vipi, huyo si mzazi ni mtu tu aliyetumia uzazi wake kukuleta dunian, na hapaswi kunyenyekewa maana mthamah ushaomba, why uendelee kujitesa? Kuna wazazi wana roho za ushirikina&matatizo ya akili hivyo solution ni kuachana nao.

Tunza afya yako ya akili&mwili,
 
Kuna wazazi wapumbavu hata akiomba mthamah vip haitosaidia, jambo la msingi niyeye kukubaliana na ukweli, muhimu ashatambua kosa na kufikisha mthamah, na wao wamegoma, so why ajitese?.

Tusipende kuendekeza ujinga na upumbavu tuliolishwa utotoni kuwa mzazi sijui hakosei wala hafanyiwi vitu gani, hivyo vitisho ndivyo vimeharibu jamii na watoto wengi kwa kuwalazimisha waende nje ya ndoto zao kwa kufuata matakwa ya vitisho vya wazazi wapumbavu.
 
Some things cannot be changed, let them flow.

NB: Kwa mara nyingine tena wakataa ndoa wanabeba points tatu kiulaini kabisa.
 
Hao wazazi hasa mama alikuwa mzinguaji ila na wewe pia ulikuwa na nafasi ya kuhakikisha kuwa miguu yako haikusaliti kuepuka kinachoendelea sasa hivi. Endelea kutulia kidogo huku ukitafuta watu wanao heshimiana na wazazi wako uongozane nao mpaka nyumbani ukaombe msamaha kwa majuto makali.

Wengine wanahusisha ukabila ila mimi nadhani ni tabia ama matatizo ya akili anayo mama yako sasa na baba yako hajalitambua hilo.

Ingelikuwa Ukuryani kama wanavyohisi washiriki kuna mtu angelichalangwa mapanga palepale na wala story tusingeli subiri mpaka leo kuifahamu.
 
Pole sana mkuu, maisha huwa hayatabirikii nimejisikia vibaya sana kwa mambo ambayo wazee wako wanakufanyia mkuu.......

Ila kaka wewe kazana na mambo yako mkuu ndo maana sometimes huwa naona ni bora kuwa na marafiki wa faida kama hao kuliko ndugu mkuu.....


Mkuu kwa kumaliziaa USIMTONGOZE HUYO BINTI WA KISHUA 🤐🤐🤐

OVER
 
Waheshimu baba na mama (wazazi wako) upate heri na maisha marefu duniani. Hakuna tija kuwa adui wa wazazi wako kwa sababu yoyote ile. Tuna deni kubwa kwa wazazi wetu ambalo hatuwezi kulilipa, na ukitaka kujua thamani ya mzazi, kutana na watu ambao hawana mtu wanayeweza kumwita baba au mama na uone walivyo, wanavyojisikia na wanayotamani, lakini hawawezi kuyapata.
 
Mhuuu! Ukitaka kujua thamani ya mkia wa ng'ombe ukate. Usidhani rafiki anaweza kuchukua nafasi ya ndugu yako. Katika maisha kuna nafasi ya ndugu (na si ya rafiki) na kuna nafasi ya rafiki (na si ya ndugu). Unaweza kuweka moyo wako asilimia 100 kwa rafiki, je na yeye anafanya hivyo kwako? Marafiki baada ya muda fulani wanaweza kubadilika, lakini ndugu hawabadiliki, wanabaki wale wale.
 


Uko sahihi, ila Kuna eneo kumekuwa na tu tangawizi kabisa, ladha yake nimeisikia kwenye chai!
 
Kosa lako ni kofi la kwanza ulilompiga Mama yako, Pamoja na hasira zangu na ujinga wangu wote na miaka 52 sasa;

Hata jana Baba tumepishana nilipomtembelea; Akigomba nanyamaza!

Yani ukiongea na Baba au Mama, ukiona joto linapanda; Shuka haraka, ukicheza utafikia point of no return!

Nafikiri ni chai kwamba ukitafuea Wazee ukawatumia hela wakakaa na Mzee wako watashindwa mmudu!

Issue yako Ina ukweli ila ina tutangawizi na mdalasini kwa wingi kwenye maeneo mengi sana!

Omba Tena maombi kama ya Daniel uelewane na wazazi wako; huna adabu kabisa!
 
CHUKUA HUU USHAURI
 
Mungu huyohuyo aliyekuletea malaika ambaye "greenlight" zimeanza kuwaka, muombe akupe kibali cha kupata nafasi kwa wazazi wako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…