Ni mwaka wa tatu sijapata kitambulisho cha NIDA

Naona hili la kitambulisho cha nida ni janga,mimi tangu 2018 mpaka leo sijapata kitambulisho na kila ukiulizia hamna majibu ya uhakika ya kuvipata
Nyinyi mnakwama wapi. Watu mbona vinapotea na wanapewa vingine haraka ti baada ya kulipia 20 Kama taratibu zao zinavyoelekeza!
 
Mimi walinipigia nikachukue cha kwangu, nilipofika nikakuta kitambulisho changu kina taarifa ambazo sio zangu, kitu pekee kilichokua sahihi ni jina langu lakini vingine vyote sio vya kwangu kuanzia tarehe ya kuzaliwa, mwaka na hata picha ni ya mtu mwingine, mpaka sasa ni miaka miwili sijapatiwa kitambulisho
 
Kuna sehemu natakiwa nipeleke copy ya kitambulisho Cha NIDA. Hawapokei Cha kupigia kura wa la cheti Cha kuzaliwa
Kwa sasa hakuna taasisi inayoweza kukulazimisha upeleke copy ya kitambulisho cha NIDA ksbb taasisi zote wanajua vitambulisho havitolewi. Isipokuwa namba tu ya NIDA inatumika mahala popote kwa sasa. Hata unapo-aplay passport kwa sasa unadaiwa namba tu ya NIDA. Hata wanafunzi wa vyuo waliokuwa wana-aplay juzi kati wametumia namba tu.

Hivyo vitambulisho vitachukua time kutoka. Maana kama unavyoijua hii nchi aliepewa hiyo kazi akajipigia mpunga akasepa. Wanapiga blaa blaaa tu sasa
 
Duh,wakati changu miaka mitatu ijayo kina-expire..pole.. nlikipata 2014
 
Mkuu pole sana, hata mimi kuna kipindi nilikua operator na nilivokuja kujiandikisha pia nilipata wasiwasi sana kupata namba, ila Mungu mkubwa nna namba nangoja kitambulisho tu.
 
Wenzio mwaka wa 5 huu na hatulalamiki
 
Namshukuru Mungu mm nimepata mwezi uliopita nilijiandikisha 2019

Kilichonisaidia mm nilikuwa napiga simu NIDA makao makuu toka mwaka huu mwez wa tano nikawa nawasumbua kila wiki napiga nakuwadanganya kuwa nimepata chuo nje so wanataka ID ya taifa

Mwez wa nane mwanzon nikawapigia wakaniambia mbona kimetoka nenda ofisi yako ya mtaa ulipojiandkikishia

Kweli nilipoenda nikakipata kitambulisho changu

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kama ulimsaidia mtu, itabidi kitambulisho kitoke kwanza. Then mchukue huyo mtu uende nae NIDA na hiyo ID yake. Watamtoa kwenye system haraka sana.
 
Tupatie na sisi mawasiliano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…