Maria Nyedetse
JF-Expert Member
- Apr 24, 2021
- 661
- 1,501
Ni miezi mitano imepita tangu Mwanafunzi wa kidato cha pili Nyumbu Secondary, Kibaha Mkoani Pwani Warda Mohamedi(15) atoweke nyumbani alipokuwa anaishi April 19,2023 na hadi sasa hajulikani alipo licha ya juhudi za Familia kumsaka huku Polisi ikisema inaendelea na uchunguzi.
Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amefika Yombo Vituka, Dar es salaam nyumbani kwa Dada yake Warda aitwaye Sophia na kuongea nae pamoja na Mama Warda ambapo wamesema Warda amepotea akiwa anaishi nyumbani kwa Mwalimu Wema Msanya wa Bokotimiza Primary, Kibaha “Majirani wanasema Mwalimu Wema na Mwanae walimpiga Warda kwa mti wa kusukumia chapati hadi ukavunjika, alilia sana akaondoka”
“Mwalimu alianza kuishi na Warda akiwa Shule ya Msingi aliomba aishi nae kwakuwa anafanya vizuri darasani akaishi nae kuanzia Kibiti, akahamia nae Ubungo kisha Kibaha hadi anaanza Sekondari, April 17 nilimpigia Mwalimu nikamsikia Mtoto analia nikamuuliza shida nini akasema usijali ni makuzi tu, April 19 akatoweka na hajarudi hadi leo”
“Mwalimu anasema Warda aliondoka baada ya kumpiga kwakuwa Walimu wa Warda walimwambia ana simu lakini Walimu wanasema sio kweli, Walimu waliomba Wanafunzi waandike wanayofahamu kuhusu Warda na wote waliandika kuwa Warda alikuwa anawaambia anateswa na Mwalimu Wema, barua za Wanafunzi ninazo, Mwalimu mpaka sasa yupo uraiani anaendelea na kazi na anatutishia tusifuatilie kesi, anatuambia hamuwezi fanikiwa kwasababu Mimi nafahamiana na Vigogo Serikalini”
“Nimeshahangaika Polisi Kibaha bila mafanikio hadi sasa, nimefika hadi kwa DC Kibaha kote wanamuita Mwalimu Wema wanamuhoji bado sijafanikiwa, Serikali inashindwa kupata ufumbuzi kweli juu ya hili!?”
Namba za Familia ni 0715446930 (Mama Warda) 0656520998 (Dada yake Warda) ….. Video nzima kuhusu kutoweka kwa Warda ipo Youtube ya millardayo