WINGER_TEREZA
JF-Expert Member
- Jul 31, 2015
- 242
- 450
Ndugu zangu, kwanza nitoe pole kwa wote kufuatia kifo cha Raisi wetu mpendwa. Sasa nijielekeze moja kwa moja kwenye mada, kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 37(5) Makamo wa raisi, mama Samia, ndiye atakaye kuwa raisi wetu kwa kipindi chote kilichobakia kuelekea 2025.
Hii itapelekea kuwepo kwa viongozi wakuu wawili ambao kwa mujibu wa katiba zetu (katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na katiba ya Zanzibar) ndio wanamamlaka makubwa yanaihusu Taifa letu kwa ujumla wanaotoka upande mmoja wa Muungano yaani Zanzibar.
Kwa kuangalia hapo utaona upande mmoja wa Muungano (Zanzibar) utakuwa umetoa viongozi wakuu wenye mamlaka za juu kabisa hivyo wanaweza kutumia "fursa" hii kutatua kama sio kumalizia kabisa kero za Muungano hasa zile zilizo dumu miaka nenda rudi.
Nawasilisha, Wasalam.
PIA SOMA
- Muungano wa Tanganyika na Zanzibar: Una faida gani na kwa manufaa ya nani?