Ni namna gani naweza kufuatilia kupata Hati ya Kiwanja?

Ni namna gani naweza kufuatilia kupata Hati ya Kiwanja?

Man Fort

New Member
Joined
Sep 8, 2021
Posts
2
Reaction score
1
Wadau naomba mnisaidie ni procedure zipi zinafuatwa ili kupata hati ya kiwanja
Vitu vinavyotakiwa.
 
Fika Halmashauri ya wilaya kiwanja kilipo utapata maelekezo zaidi.
1. Unatakiwa uwe na NIDA number
2. Picha passport size 8.
3. Survey Plan.
Kiwanja umenunua Kwa Nani? Kama Kampuni ni rahisi wao kufuatilia. Kama ni Kwa mtu unatakiwa uwe na mkataba original Wa aliyekuwa anamiliki.
 
Kwa uzoefu wangu. Maana ni majuzi tuu nilikuwa nafatilia hiyo kitu (Hati) kwanza kabisa kiwanja kinatakiwa kiwe kimelipiwa Hapo Ardhi (Ofisi za Ardhi za kiwanja husika) na kiwe kimelipiwa pia TRA (Yaani umeshakadiliwa).

Kisha baada ya hapo unarudi tena Ardhi wanaenda kukupimia tena kwa ajili ya kutengeneza Hati sasa.

Zile form za vipimo zitaambatanishwa na form nyingine pamoja na Control number ya kulipia pamoja na form za mwanasheria.

Utasaini wew pamoja na mwanasheria. Kisha utarudisha Ardhi baada hapo ndo unapewa Hati yako.
 
Kwa uzoefu wangu. Maana ni majuzi tuu nilikuwa nafatilia hiyo kitu (Hati) kwanza kabisa kiwanja kinatakiwa kiwe kimelipiwa Hapo Ardhi (Ofisi za Ardhi za kiwanja husika) na kiwe kimelipiwa pia TRA (Yaani umeshakadiliwa). Kisha baada ya hapo unarudi tena Ardhi wanaenda kukupimia tena kwa ajili ya kutengeneza Hati sasa. Zile form za vipimo zitaambatanishwa na form nyingine pamoja na Control number ya kulipia pamoja na form za mwanasheria. Utasaini wew pamoja na mwanasheria. Kisha utarudisha Ardhi baada hapo ndo unapewa Hati yako.
Inachukua muda gani ?
 
Fika Halmashauri ya wilaya kiwanja kilipo utapata maelekezo zaidi...
Habari kaka mimi nimenunua kiwanja kwa mtu aliyekua anakata viwanja kwenye shamba lake kubwa na kuuza ila kwa bahati mbaya nimekuja kugundua kile kiwanja alicho niuzia aliniuzia kutoka kwenye shamba ambalo lilikua na hati tayari tofauti na wenzangu walio kua wanauziwa squatter sasa naomba kujua je naweza kupima kiwanja changu maana nyaraka zote za mauziano ninazo
 
Kama eneo kilikuwa na Hati tayari unatakiwa kuwa na deed of surrender.
Unaambatanisha na mkataba WA mauziano
Number yako ya NIDA... passport size. 5 then unafika Halmashauri Kwa ajili ya kupewe gharama za kulipa Kodi za Serikali.
Haichukui muda
 
Habari kaka mimi nimenunua kiwanja kwa mtu aliyekua anakata viwanja kwenye shamba lake kubwa na kuuza ila kwa bahati mbaya nimekuja kugundua kile kiwanja alicho niuzia aliniuzia kutoka kwenye shamba ambalo lilikua na hati tayari tofauti na wenzangu walio kua wanauziwa squatter sasa naomba kujua je naweza kupima kiwanja changu maana nyaraka zote za mauziano ninazo
hpo kuna kaz kidogo kwanza inatakiwa huyo mwenye hat hairudishe ikafutwe then ndio unaeza anza process za upimaji upya

Sent from my Infinix X658E using JamiiForums mobile app
 
Habari kaka mimi nimenunua kiwanja kwa mtu aliyekua anakata viwanja kwenye shamba lake kubwa na kuuza ila kwa bahati mbaya nimekuja kugundua kile kiwanja alicho niuzia aliniuzia kutoka kwenye shamba ambalo lilikua na hati tayari tofauti na wenzangu walio kua wanauziwa squatter sasa naomba kujua je naweza kupima kiwanja changu maana nyaraka zote za mauziano ninazo
Apo inatakiwa zianze taratibu za kurejeshwa/Surrender ya umiliki wa shamba husika kwa ngazi ya manispaa husika mpaka wizarani Kuna kaprocess mpaka kuipata DEED of Surrender.

Then Deed of Surrender ikipatikana ndipo maombi ya kufuta upimaji wa ilo shamba yanafanyika kuanzia ngazi ya manispaa mpaka ngazi ya mkoa kwa maana Kanda husika na mwisho utapata kitu kinaitwa Consent for plot/farm cancelation.

Baada Consent kutoka Apo ndipo unaweza kupima Kama mmiliki mpya wa kupande Cha ardhi na kufanya taratibu za kupata hatimiliki.

Nimejaribu kusummarize apooo kidogo
 
Mimi nilinunua kiwanja kwà mtu kipo kwenye eneo lililopimwa tayari ila sijaenda kupiga picha wala Serikali hainitambui ila ninamkataba wa mauziano. Utaratubu ukoje
 
Utaratibu uko hivi:
1. Unatakiwa kupata kampuni itakayofanya kazi ya kupima.
2. Kampuni hiyo itaenda ardhi kuangalia kwenye ramani iwapo eneo hilo limepangiwa matumizi.
3. Kutokana na majibu yatakayopatikana toka ardhi. Kampuni ya upimaji itaenda ofisi ya halmashauri kuomba kibali cha kupima. Wakati mwingine unaweza kuhitajika kuomba kubadilisha matumizi ya eneo husika.
4. Kiwanja kitapimwa na kuwekewa mawe.
5. Mawe yataenda kusajiliwa ardhi ili yaingie kwenye ramani rasmi.
6. Utakabidhiwa michoro ya eneo lililopimwa au unaweza kuiruhusu kampuni iendelee na hatua zinazofuata.
7. Hatua inayofuata ni kwenda halmashauri kwa ajili ya kuomba hati.
8. Mwanasheria atajaza fomu za kuhalalisha umiliki wako.
9. Ardhi watamtuma mthamini kwa ajili ya kutathmini thamani ya eneo husika.
10. Thamani hiyo itatumika kukadiris gharama za transfer fees (inalipwa halmashauri) na gharama za capital gain tax (inalipwa TRA).
10. Ukishalipa kodi TRA utapewe certificate ya kuthibitisha kuwa kodi imeshalipwa.
11. Unarudi halmashauri kwa ajili ya kujaza ombi la kupewa plot number na hati.

Mlolongo wake kama unavyoona sio mdogo, ndio maana watu wenye kiwanja kimoja huwa ni ngumu kufuata utaratibu huu. Utaratibu huu ni rahisi iwapo watu wengi mashirikiana au ukiwa na viwanja vingi kwenye eneo moja.
 
Ndugu zangu naomba mnipe mwongozo pa kuanzia mimi nimenunua kiwanja kutoka kwenye kampuni inayouza viwanja lakini wao walikuwa bado hawajavirasimisha ila walikuwa waneshavipima wao tu tukuvikata zen wakauza. Nilinunua nikawa na document za mauziano kupitia seeikal za mtaa lakini nahitaji kukata lessn ya umiliki kwa hiyo naomba mnielekeze pa kuanzia
 
Kampuni mnauzianaje Serikali ya mtaa?Hakuna mwanasheria?
 
Mkuu umenunua kiwanja wap?

Ondoa shaka mchakato wa kufuatilia Hati miliki kutoka wizarani sio mgumu sana ila unahitaji

Ramani ya mipango mji (TP)
Lazim kiwanj kiwekwe Beacons kutok wizarani

Na process zingine zifuate

Lakini ni vizur hiyo kampuni iliyokuuzi wangewasaidia kwa pamoj kufany process za hati kuliko kufanya peke ako
 
Kampuni mnauzianaje Serikali ya mtaa?Hakuna mwanasheria?
Kwenye mkataba lazima kuna mwanasheria atakua ame sign

Ni vigumu kila mteja anayeuziwa kiwanja akutanishwe na mwanasheria

Kampuni zingine huwa zina scan ile signature ya mwanasheria so kwenye kila contract ina appear
 
Back
Top Bottom