Ili uweze kupata hatimiliki.....labda tuanze kupeana short summary ktk umiliki wa viwanja.....Guys umiliki wa viwanja upo ktk nyanja mbili ambao Ni umiliki wa kumila na umiliki wa kiserikali....Ndugu zangu naomba mnipe mwongozo pa kuanzia mimi nimenunua kiwanja kutoka kwenye kampuni inayouza viwanja lakini wao walikuwa bado hawajavirasimisha ila walikuwa waneshavipima wao tu tukuvikata zen wakauza. Nilinunua nikawa na document za mauziano kupitia seeikal za mtaa lakini nahitaji kukata lessn ya umiliki kwa hiyo naomba mnielekeze pa kuanzia
Umiliki wa kimila n vile unaandikiwa mkataba wako wamauziano ukielezea ukubwa kwa kuzingatia physical feature zinazoonekana ardhini Kama sehemu ya mipaka mfani mti,mnazi,mto,mkuza etc...na unakuwa umesainiwa na pande zote mbili baina ya muuza na muuziwa mbele ya mashaidi wao.......
Umiliki wa kiserikali n ule umiliki ambao unatambulika kikatiba na uliosajiliwa na wizara husika ya maswala ya ardhi.
Tunavyotaka kupata umiliki wa kiserikali apa Kuna vitu vyakuzingatiwa ambapo Tp (Mchoro wa mipango miji),survey plan (Ramani yenye kuonyesha plot number ya kiwanja ambayo inatambulika na wizara ya ardhi) na afusa ardhi....na moja ya vitu muhimu Sana ila vikisindikizwa na atribute nyengine Kama mkataba wa umiliki apa kutaka kujua ulipataje kiwanja chako,kitambulisho Cha nida na vinginevyo....
Hivyo basiii ili uweze kupata hatimiliki ya kiserikali inatakiwa utengenezewe Mchoro wa mipango miji unaoonyesha matumizi halisi ya kiwanja chako kupitia kwa afisa mpango miji(wa serikali au Binafsi wote wanaweza kufanya hii kazi kwa Bei mtayoafikiana)...mpango miji ukiwa umekamilika mpima aka Surveyor atakuja kutekeleza Mchoro wa mpango miji ardhini ikiwemo na kukupa Ramani yenye plot number ambayo itakuwa imesajiliwa na wizara,apa pia mpima Binafsi au wa serikali wote wanaweza kulifanyia hii kaziiii.....
Baada ya Mchoro wa mpango miji na Ramani ya upimaji kuwa zimekamilika hapo utaandika barua ya maombi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa kwenda kwa manispaa au wilaya husika kwa Afisa ardhi ili uweze kukadiliwa Kodi na gharama za uchapwaji wa hatiiii...kutoka Apo hatimiliki yako inaweza kupatikana kutoka kwa wizara kupitia kwa ofisi za Kanda ya mkoa husikaaaa