Ni nani aliyeanzisha biashara ya parking Muhimbili?

Ni binadamu lakini sio vyema kuwatumia sehemu za jumuia ya watu wa aina tofauti tofauti. Baadala yake wawatumie watu wenye uwezo wa lugha na alama mbalimbali.


Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli wanachofanya ni sahihi lkn walinzi (lugha ya alama)wafanya usafi (lugha ya alama)pale kanteen kwao (lugha ya alama)hivi mgeni akiwa na changamoto ya maulizo huna wa kumuuliza haraka haraka maana ndio wanaopatikana kwa urahisi
 


Hii ni kasumba ya watanzania, kutupiana lawama na kumsaka mchawi wakati tunguli ziko chini ya vitanda vyao!


Kazi ya kampuni za ulinzi na kitengo cha usimamizi wa ulinzi wa hospital, mali zake na wagonjwa ni zipi?



Hizi suluhisho za kukomoana zaidi ya kujenga zinabomoa maana inturn zinaumiza wengi wasiokuwemo wakati hatua stahiki na uwajibikaji wa kila mmoja ukizingatiwa utaratibu utafuatwa.


Tatizo letu ni wavivu wa kujisimamia na hata kusimamia sheria na taratibu tunazojiwekea sisi wenyewe na huku wengine wakijali zaidi matumbo yao na kufanya sabotage za kila aina ili miradi Kama hii ya kinyonyaji ifanikiwe.
 
Usipaki hata kununua kiberiti dukani wanakulipisha parking,hao tarura kwann wasijenge parking zao ndipo walipishe

Nashangaa kwanini hawataki kujenga parking zao? I mean Kama jengo la ghorofa nane ama kumi pale Lumumba likawa parking hizo za kulipia Tatizo liko wapi?


Malipo ya parking city center yalilenga ku discourage watu kurundika magari yao mjini hasa Mida ya kazi wengine walifanya double parking kabisa.


Sasa kila sehemu mnaweka parking fee mpaka nyumba ya Maiti?



Ule mpango wa Serikali kuziagiza Taasisi zake mbali mbali kutengeneza vyanzo vyao vipya vya mapato na miradi ya maendeleo ndio huu?
 
Ni nani alieanzisha biashara ya parking MUHIMBILI?
Pesa inayopatikana inamnufaisha nani?
Ni haki kumtoza pesa mgonjwa kwa kupaki gari lake tu?
Ni kweli binadamu mtanzania amekosa utu na huruma kiasi Cha kutoza pesa WAGONJWA?
Biashara za watu hizi
 
Ni nani alieanzisha biashara ya parking MUHIMBILI?
Pesa inayopatikana inamnufaisha nani?
Ni haki kumtoza pesa mgonjwa kwa kupaki gari lake tu?
Ni kweli binadamu mtanzania amekosa utu na huruma kiasi Cha kutoza pesa WAGONJWA?
Ngoja nikwambie ilikuaje wakaanzisha.
Kupitia survey zao kwa CCTV, waligundua kuwa at any time T, kuna idadi kubwa sana ya magari ndani ya uwanja wa hospitali, kulinganisha na idadi ya staff wao pamoja na wagonjwa.
Walipofanya uchunguzi zaidi, wakagundua kuwa kuna miamba huwa wanakuja wanapaki magari hapo, na kutoka nje (wanakua hawana shughuli yoyote ndani ya hospitali), wanaenda zao labda Kariakoo au posta (city center).
Wakaumiza vichwa wanafanyaje? Wakaona isiwe kesi, watumie kama fursa, iwe 'blessing in disguise', ndo wakaweka hiyo parking fee kwa yoyote anaetaka kupaki gari hapo na sio staff, maana waliona wakianza kukimbizana na kuchunguza huyu ni mgonjwa kweli au sio, watapoteza sana muda wao. Basi, ndo wakaja na hiyo idea ya parking fees. Ndivyo ilivyokua.
 
Waangalie na maeneo Leo hata ukipaki tu nje ya nyumba yako wanakulipisha
Kwa muhimbili nakubaliana na profesa Janabi, magari yalikua yanajaa pale, ukienda kumuona mgonjwa unapata paking kwa taabu, uzuri ndani saa 1, ni bure baada ya hapo unalipia.

Kazi iko mitaani eneo la nyumba yako, wanakuchaji, yaani wanashindwa kutofautisha kariakoo, na huku uswazi, hawa wanaoumulika magari itakua wanalipwa, kulingana na magari aliyoyamulika, maana unakuta mtu ameaka anaelekea maeneo ya pakingi, njiani, akikuta gari limesimama tu analimulika.
.serikali ilitakiwa itoe ufafanuzi sehemu gani inatakiwa kulipia parking fees.
 
Ni nani alieanzisha biashara ya parking MUHIMBILI?
Pesa inayopatikana inamnufaisha nani?
Ni haki kumtoza pesa mgonjwa kwa kupaki gari lake tu?
Ni kweli binadamu mtanzania amekosa utu na huruma kiasi Cha kutoza pesa WAGONJWA?
Alianzisha Mkurugenzi wa Muhimbili prof , hukusikia alisema watu wznakwenda kupack magari pale then wanaakwenda mjini jioni wanaafata magari yao, Sasa Keisha jeuri
 
Hama nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…