Ni nani aliyeibadilisha Tanzania kwa muda mfupi hivi?

Ni nani aliyeibadilisha Tanzania kwa muda mfupi hivi?

Chagu wa Malunde

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
8,746
Reaction score
5,772
Tanzania hii ambayo ilibadilika ikawa na watu amabao waliishi maisha ya kula bata kuliko hata watu wa ughaibuni, leo imebadilika katika kila nyanja.

Kuna watu walikuwa wanajilipa mishahara hewa hadi ya watumishi 10. Na mitaani huku ilikuwa ni kula bata na kutanua na vimada leo hawapo. Mabadiliko makubwa.

Kuna watu walikuwa wanajichotea pesa kwenye halmashauri eti kisa ni wakurugenzi au wakuu wa idara, leo hii hii kitu haipo. Mzigo wote umefichwa kwenye consolidated fund.

Kuna watu walikuwa wanaenda kufanya mikutano ya bodi ya mashirika nje ya nchi. Na kujilipa posho kibao, leo hii kitu hakipo. Mikutano wanafanyia kwenye kumbi za wizara na mambo yanaenda vizuri.

Kuna wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi tena kwa ubabe. Kisa wana ujamaa na wanasiasa vigogo. Leo hii wanalipa na madeni ya nyuma waliyalipa.

Kuna watu walikuwa wanaagiza magari na kuyaleta toka nje kwa ndege. Tena magari ya kifahari baada ya kupiga dili kama EPA na Escrow, leo hii hatusikii hizi kufuru.

Kwenye vyama vya ushirika huko ndio ilikuwa aibu. Wakulima ni kudhulumiwa kila msimu. Lakini awamu hii imekuwa ni hatari. Ukimuibia mkulima kesho upo lupango.

Kubwa kabisa, ni la kutekeleza mradi mkubwa kama JNHPP kwa fedha za ndani zaidi ya Tril 6 za Tanzania! Haya madiliko nani ameyaleta. Na hii ni baadhi ya mabadiliko makubwa mabayo yamefanyika ndani ya muda mfupi sana takribani miaka minne.

Je, kwa mabadiliko haya hapa Tanzania wapinzani waweke mgombea wa urais hapo October 2020?
 
Tukajenga barabara na kutekeleza miradi mikubwa na ndege (lakini tumetoa tenda kwa RwandAir, ndege zetu zipo quarantine) kwa pesa zetu za ndani. Tumedhibiti makinikia na kubania mabeberu.

Hii hadithi ishapoteza mvuto kama chama na Jiwe.
 
Sasa unauliza ni nani aliyebadilisha Tanzania mi nikajua kuna bonge la content humu ndani. Hivi ni kweli umeuliza swali kumaanisha au unataka kutuchosha tu ndugu yangu.
Nataka kujua nani kaleta haya mabadiliko.
 
Tukajenga barabara na kutekeleza miradi mikubwa na ndege (lakini tumetoa tenda kwa RwandAir, ndege zetu zipo quarantine) kwa pesa zetu za ndani. Tumedhibiti makinikia na kubania mabeberu.

Hii hadithi ishapoteza mvuto kama chama na Jiwe.
Kwani Rwandair wamepewa tenda na Tanzania? Au kuna kampuni ya ubelgiji imewapa hiyo tenda? Tusilaumu tu.
 
Sasa hizo pesa unazosema ziko salama kipindi cha awamu hii zimekusaidiaje?

Kabla ya huyu watumishi walikuwa wakiongezewa mishahara na kupewa stahiki zao sasa hivi kama tuna hela zinatusaidia nini?
 
Sasa hizo pesa unazosema ziko salama kipindi cha awamu hii zimekusaidiaje?

Kabla ya huyu watumishi walikuwa wakiongezewa mishahara na kupewa stahiki zao sasa hivi kama tuna hela zinatusaidia nini?
Ubungo interchange imekamilika 98% itasaidia kupunguza msongamano wa magari. JNHPP itakamilika kwa wakati. Na huu utaleta faida kubwa sana kwa taifa letu.
 
Tanzania hii ambayo ilibadilika ikawa na watu amabao waliishi maisha ya kula bata kuliko hata watu wa ughaibuni, leo imebadilika katika kila nyanja.

Kuna watu walikuwa wanajilipa mishahara hewa hadi ya watumishi 10. Na mitaani huku ilikuwa ni kula bata na kutanua na vimada leo hawapo. Mabadiliko makubwa.

Kuna watu walikuwa wanajichotea pesa kwenye halmashauri eti kisa ni wakurugenzi au wakuu wa idara, leo hii hii kitu haipo. Mzigo wote umefichwa kwenye consolidated fund.

Kuna watu walikuwa wanaenda kufanya mikutano ya bodi ya mashirika nje ya nchi. Na kujilipa posho kibao, leo hii kitu hakipo. Mikutano wanafanyia kwenye kumbi za wizara na mambo yanaenda vizuri.

Kuna wafanyabiashara walikuwa hawalipi kodi tena kwa ubabe. Kisa wana ujamaa na wanasiasa vigogo. Leo hii wanalipa na madeni ya nyuma waliyalipa.

Kuna watu walikuwa wanaagiza magari na kuyaleta toka nje kwa ndege. Tena magari ya kifahari baada ya kupiga dili kama EPA na Escrow, leo hii hatusikii hizi kufuru.

Kwenye vyama vya ushirika huko ndio ilikuwa aibu. Wakulima ni kudhulumiwa kila msimu. Lakini awamu hii imekuwa ni hatari. Ukimuibia mkulima kesho upo lupango.

Kubwa kabisa, ni la kutekeleza mradi mkubwa kama JNHPP kwa fedha za ndani zaidi ya Tril 6 za Tanzania! Haya madiliko nani ameyaleta. Na hii ni baadhi ya mabadiliko makubwa mabayo yamefanyika ndani ya muda mfupi sana takribani miaka minne.

Je, kwa mabadiliko haya hapa Tanzania wapinzani waweke mgombea wa urais hapo October 2020?
mzee mm siku zote husema jamani wacheni bangi hivi kipi cha maana kafanya huu ni mwaka wa 60 tangu ccm waanze kutawala nchii




KWA WALE MSIO IJUA TANZANIA VIZURI SOMENI KWA MAKINI UTAJIRI WA TANZANIA HALAFU JIULIZE KWA NINI NI MASIKINI WA MWISHO NA MALI ZOTE HIZI



1.Tz ilipata uhuru mwaka 1961 ina miaka 59

tangu ipate uhuru ikiwa ni ya kwanza afrika

mashariki.



2.Tz Kwa miaka 57 hii inchi imeongozwa na ccm

peke yake ambayo ni zao TANU na ASP.



3.Tz ni nchi ambayo hajawahi kupata majanga

makubwa kama matetemeko ya ardhi,magonjwa

ya mlipuko kama ebola,mafuriko na vimbunga au

ukame.



4.Tz ni nchi ambayo imekuwa na kitu ambacho

nnchi za Africa zimekikosa AMANI kwa miaka

yote 54 ya uhuru hajawahii kupigana vita vya

wenyewe kwa wenyewe.



5.Tz ina ukubwa ukubwa wa 945,000 km square

yani sawa na uchukuwe Denmark,France,United

kingdom(uk),Netherland,Ireland ujumlishe zote

kwa pamoja.



6.Tz ina eneo la bahari lenye ukubwa wa 1,424

kilometers bahari inaleta fursa za usafirishaji,uv

uvi,utalii na nyinginezo.



7.Tz ni nnchi ambayo imepakana na nchi za

(Uganda,Rwanda,Burundi,Zambia,Malawi,Drc

congo) ambazo zinategemea bahari yetu kwa

usafirishaji wa mizigo na ni fursa nzuri ya

kuzipelekea bidhaa za viwanda vyetu



8. Tz ina maziwa makubwa manne na mengine

madogo mengi.

Maziwa matatu makubwa yako kwenye kumi bora

za ukubwa duniani na Maziwa makubwa matatu

yote yapo Tanzania..Ziwa Victoria ni la tatu kwa

ukubwa duniani(la kwanza afrika) na ziwa

Tanganyika ni la sita kwa ukubwa(la pili afrika)

na la kwanza kwa kuwa na kina kirefu

duniani.Ziwa nyasa ni la tisa kwa ukubwa duniani

(ni la tatu afrika).



9.Tz ina mito mikubwa kumi ambayo ni mto

kagera,mto Ruvuma,mto rufiji,mto wami,mto

maragarasi,mto mara,mto pangani,mto mara,mto

gombe,mto mweupe wa nile.na ina mito midogo

mengi kama mto kilombero,mto mbemkuru n.k



10.Tz ndiyo nchi ya kwanza afrika kuwa na maji

mengi yasio na chumvi yaliyokuwa kwenye uso

wa dunia(fresh surface water) kutokana na kuwa

na mito na maziwa mengi na kupitiwa na bonde

la ufa.



11.Tz ni nchi ya nne kwa uzalishaji dhahabu

afrika baada ya afrika kusini,ghama na mali na

ipo top 20 duniani.

Kuna migodi nane inayochimbwa dhahabu na

miwili imefungwa.

migodi inayochimbwa ni Buzwagi gold mine-

(Shinyanga),Geita gold mine-(Geita),Golden pride

gold mine-Nzega(tabora),Bulyanhulu gold mine-

(Shinyanga).New leuka Gold mine-(Mbeya),

Tulawaka gold mine-(kagera),North mara gold

mine-(mara).Iliyofungwa ni Kirondatal gold mine-

(Shinyanga),Senkenke gold mine-(Shinyanga).



12.Tz ina madini ya almasi yanayopatikana

mwadui shinyanga mgodi huo umeanzwa

kuchimbwa tangu mwaku 1940 mbaka leo ado

unachimbwa,unamilikiwa nakampuni ya

wingereza.



13.Tz ni nchi ya kwanza na ni nchi pekee

inayozalisha madini ya tanzanite duniani.mkufu

wa kuva shingoni unatengenezwa na tanzanite na

almasi unauzwa hadi milioni 25 za kitanzania.



14.Tz ina madini ya chuma yanayopatikana

mchuchuma,ludewa- njombe mgodi unamilikiwa

na wachina mgodi huo una hifadhi ya madini ya

chuma tani milioni 122 ambayo yanawezwa

kuchimbwa kwa zaidi ya miaka 100.



15.Tz ina madini ya makaa ya mawe

yanayochimbwa kule kiwira mbeya,mchucuma na

liganga njombe unamilikiwa na wachina pamoja

na ngaka kule mbinga-ruvuma unamilikiwa na

kampuni ya tancoal ya Australia.hifadhi ya

madini ya makaa ya mawe iliyopo ni tani bilioni

2.makaa yam awe ndio chanzo cha pili ya

umeme wabei nafuu duniani baada ya maji.



16.Tz ina hifadhi ya madini ya uranium kule

Dodoma(bahi) na mgodi ambao unamilikiwa na

warusi pia madini haya yanapatikana pia

Namtumbo (Mkuju),Galapo, Minjingu, Mbulu,

Simanjiro, Lake Natron, Manyoni, Songea,

Tunduru, Madaba and Nachingwea.



17.Tz ni moja ya nchi tatu Africa pamoja

Zimbabwe na madagascar kwa kuwa madini

mengi ya graphite madini haya yapo

Tanga,Mahenge-Morogoro,mererani-

manyara.Madini ya graphite ndiyo yanayotumika

kutengenezea betri za simu,kwenye injini na

brake za gari na kwenye karamu ya risasi

(pencili)



18.Tz ina madini ya nickel yanayopatikana kule

kabanga kagera,milima ya ulurugulu-morog

oro,north mara,Ngasoma-mwanza.



19.Tz ni nchi ya tatu duniani kwa kuwa na

hifadhi kubwa ya magadi soda mengi duniani

baada ya marekani na uturuki.magadi soda

hutumika kutengeneza vioo vya aina zote vyo

nyumbani hadi magari pia kutengeneza sabuni na

dawa mbalimbali za usafi



20.Tz ina hifadhi na mgodi wa madini ya niobium

uliopo Panda hill mbeya ambao ndio utakuwa

mgodi mkubwa wa kwanza Africa na wanne

duniani,mgodi huu unamilikiwa na kampuni ya

uastralia.Madini ya nibioum ni magumu sana

hutumika kutengeneza mabomba pamoja na

madini chuma pia hutumika kutengeneza baadhi

ya sehemu za injini za ndege na vyombo

vinavyoenda nje ya uso wa dunia,vioo vya

computer na lenzi za camera.



21.Tz ni nchi ya kwanza Africa na ya pili duniani

kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ya

kwanza ikiwa brazil. Nchi zilizokuwa kwenye tano

bora kwa utalii Afrika ni Tanzania, Botswana,

Afrika Kusini, Kenya na Zambia.



22.Tz ina mbuga zipatazo 16 na ile mbuga

maarufu kuliko zote duniani Serengeti na mbuga

iliyopakana na bahari saadani na mlima mrefu

kuliko wote Africa Kilimanjaro.



23.Nadhani kila mtz anajua juu ya sifa ya

Tanzania kwenye swala ya kuwa na ardhi ya

rutuba inayofaa kwa kilimo



24.Tz ina gesi ya asili ya carbon dioxide(CO2)

inayovunwa kule kyejo,rungwe-mbeya na

kampuni ya TOL,gesi ya asili ya cardon dioxide

inatumika sana kutengenezea vinywaji laini kama

soda,bia, na pia kutengenezea madawa,kwenye

viwanda vya makaratasi na kutibia maji.



25.Tz ina gesi ya asili inayopatikana katika

kisiwa cha songo songo mkoa wa lindi gesi hii

imekuwa ikichimbwa na kusafirisha Dar as

salaam tangu mwaka 2004 na inayomilikiwa na

kampuni ya songas ya uingereza



26.Tz imengundua gasi ya asili yenye ujazo wa

zaidi ya trioni 55.3 cubic meter iliyongungulika

katika maeneo ya bahari ya lindi na mtwara.

Pamoja na sifa zote hizi Lakini Tz ni nchi

iliyokwenye kundi la nchi maskini duniani ambao

asilimia kubwa ya raia wanaishi chini ya dola

moja na hali ya huduma za kijamii zikiwa duni.



TATIZO NI NINI?NI NANI ALIYESABABISHA HUU

UMASKINI WA TAIFA HILI?......
 
Tuulizie pia nani katufanya tuwe makatili na wauaji! Nani kawaua kina Bensaa8, Mawazo, Azory? Zile maiti kwenye mifuko ya sandarusi zilitoka wapi? Nani kaanzisha utekaji wa watu? Nani kaanzisha upigaji risasi wa watu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hizi ni criminal matters na kwa sababu unaoushahidi naomba ukawape polisi sababu ni kosa kukaa kimya wakati unafahamu juu ya huu uovu.
 
Back
Top Bottom