Ni nani aliyeibadilisha Tanzania kwa muda mfupi hivi?

Nkajua hiyo ya risasi na utekaji ilikuwepo tokea zamani; umewasahau Mwangosi, Kibanda, Ulimboka(Mwakingwe), kwa kuwataja wachache?

Tudeal na mapya yaliyo anzishwa awamu hii, hizo habari za risasi,utekaji tokea enzi zilikuwepo tu..
 
Rubbish thread

Sent using Jamii Forums mobile app

👍 Nakuunga mkono. Hii ni moja ya mada ya kijinga. Iliyojaa unafiki na kujipendekeza. Imeegemea upande mmoja wa kumsifia mungu mtu.

Sasa kama kuna hayo mabadiliko mbona maisha yamezidi kuwa magumu kwa wananchi walio wengi na matamu kwa watu wachache kama akina bashite?
 
Kuna Kiumbe kinakula Bata Chato hivi sasa ..

Mishahara hewa!!! Mwambe ni moja ya Mfano..Ni Mbunge hewa na bado anachukua Mshahara.

Magu anagawa pesa mabarabarani..

Bora hao wanaagiza Magari..Magu anatuma ndege Madagascar kuchukua chupa mbili za juice.. Kwa familia yake ..
Waliowadhulumu Wakulima wa Korosho kwa Maagizo ya kipuuzi ya Jiwe mpaka Leo wako Uraiani..

Lugola pekee ni zaidi ya EPA na escrow ..na bado yuko mtaani anatembea na Ilani ya CCM.
 
Ni wale mliokuwa mnakula pesa za umma kwa kulipa mishahara hewa,kula pesa za halmashauri kula rushwa Tra ili kujinufaisha
Mbona sisi tunalima mboga mboga na tumezoea.
 
Mh... Chadema imejaa mabichwa maji. Lugola kuna pesa alizochota? Au uo mkataba ulikuwa umekamilika?
 
Kuna vitu umeongea vya uongo, mfano, sidhani kama hiyo miradi ni pesa za ndani, maana kila siku deni la taifa linapanda. Lakini pia angalia mambo mengine yanayofanyika kinyume cha katiba, hauo yanafanya nione serikali hii haifai. Unaweza ukawa msafi lakini uchafu mmoja mdogo utakuondolea usafi wote. Yaani kosa moja litafuta mazuri mengi uliyonayo
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni wale mliokuwa mnakula pesa za umma kwa kulipa mishahara hewa,kula pesa za halmashauri kula rushwa Tra ili kujinufaisha
Mbona sisi tunalima mboga mboga na tumezoea.

Mimi nataka tu kujua hizo hela unazotuambia ameziokoa na hivyo kuleta hayo unayo yaita ' mabadiliko' ziko wapi? Au ndiyo zile anazo gawia watu kienyeji barabarani?

Na kama yeye ni msafi na malaika asiye na dhambi, ni kwa nini hataki kukosolewa?
Ni kwa nini anahujumu wapinzani wake kisiasa wa ndani na nje ya chama? Kwa nini amehujumu uhuru wa vyombo vya habari? Kwa nini hataki demokrasia itamalaki nchini mwetu?

Huko kulima hizo mboga mboga zako hata hakunihusu kwa chochote. Sisi tunachotaka ni uwepo wa mgawanyo sawa wa keki ya Taifa. Na siyo kiumbe mmoja na kikundi chake waishi maisha mazuri, halafu walio wengi waishi maisha ya kuunga unga! That is an outdated Absolutism in the 21st Century.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…