Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Elections 2010 Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Status
Not open for further replies.
mla huliwa,tuliwaonyo sana hapa javini wakina malaria sugu,tumaini na wafuasi wao juu ya hoja zao za udini hawakutaka kutusikia sisi wenye akili,real what goes around comes around,sasa vimewashika,hakika mwaka huu mtajibeba
 
Kwa kweli bado sielewi hizi arguments za ku-portray CUF ni uislamu na CHADEMA ni ukristo zinatoka wapi. Mnatumia sample or basis gani?
Mimi si mfuasi wa chama chochote lakini katika jamii inayonizunguka kuna wana-CUF wakristo wengi tu na wana-CHADEMA waislamu lukuki.
Nisitumie sample ya hao wanaonizunguka kwani ninyi hamuwafahamu. Nitoe mifano michache ya celebrities wetu ambao sisi wote (wengi wetu) tunawafahamu....
1) Ulimwengu ni muislamu....lakini angalia makala zake za Raia Mwema zilivyokuwa objective (bila udini)
2) Kubenea ni muislamu...lakini angalia makala zake za Mwanahalisi zilivyo objective (kama Ulimwengu)
3) Kuna mtangazaji mmoja wa Radio WAPO (jina limenitoka) ni mkristo....lakini amekuwa quoted akisema Lipumba ni role model wake

Nadhani tunasahau ukweli kuwa propaganda hizi zinapandikizwa kwa makusudi na CCM kwa sababu imeona dhahiri uwezekano wa anguko kuu kwenye uchaguzi huu. Tusikubali kuwasaidia CCM wafikie lengo lao hili ovu na dhalimu!
Wana JF mnawajua fika makada na propagators wote wa CCM humu jamvini kwa kauli zao. Shun them...dont help their evil course to sabotage the envisaged change come Oct 31st.
 
Mwanakijiji

Huu udini unaelekea kuwarudi waliokuwa wanauendekeza. Wiki iliyopita jopo la viongozi wa dini zote kubwa nchini, walianza matembezi ya kuongea na wagombea urais. Tumeshangaa jana kuona kundi la mashehe wanakuja tena mbele ya vyombo vya habari kutoa tamko lao peke yao. Tunajiuliza ikiwa katika matembezi ya kuwaona wagombea wanakuwa wote, inakuwaje sasa wanakuja na tamko la peke yao?

Mbaya zaidi, katika umoja wao wa madhehebu yote, walisema mambo binafsi ya wogombea yasipate nafasi katika mijadala. Jana Mufti Simba akasema, yawe na nafasi. Je alimaanisha tuanze kazi ya kupima DNA za watoto wa mitaani?

Naomba niseme kwa sauti, kuwa tamko la mashehe lina agenda ya siri na ndiyo maana walishindwa hata kutamka hata jina la mtu mmoja wanayemtuhumu kuwa anaelekeza watu kupiga kura kwa misingi ya udini.

What if wameona kuwa wenzao walitumika kuhalalisha masuala ama mtu fulani??? Unajua msimamo wa Askofu Ruzoka aliyeongoza ile timu ya vongozi wa dini kwenda CHADEMA????

Please jamani wote mnajua kuwa misikitini si makanisaani watu wanachochewa kupigia kura wale wanaodai wenzao. Wapo wanaosema kwa kutmia vipaza sauti na wapo wanaosema kwa kunong'oneza. Wapo wanaosema wazi wapo wanaotumia code words.....hapa sijaongelea wale wanaopanda majukwaani kujinadi kuwa wachaguliwe wao kwa kuwa ni wenzao na wapiga kura na wanasali pamoja....
 
Nasema kwa dhati hapa kama nilivyosema kwengine humu.Hadithi nyingi juu dkt Slaa.Makosa ya wagombea wa nchi nyengine musifananishe na kwetu.Huyu mbakaji kwa uwezo wa Allah asipate.Hana hekima katika uongozi wake.Akipata uraisi itakuwa ndio mwisho wa Tanzania.Hana uadilifu.Kwanza Allah atasimama kuwatetea waungwana.Waislamu nao watachemka na utakuwa ndio mwisho.

Nna wasiwasi sana kama kweli wewe ni muislamu.....Ondoa janja yako ya kuongeza chuki hapa
 
What if wameona kuwa wenzao walitumika kuhalalisha masuala ama mtu fulani??? Unajua msimamo wa Askofu Ruzoka aliyeongoza ile timu ya vongozi wa dini kwenda CHADEMA????

Omar ana makengeza kweli .... katika yote wewe umeona ya Askofu Ruzoka tu ..... bwa ha ha ha

Please jamani wote mnajua kuwa misikitini si makanisaani watu wanachochewa kupigia kura wale wanaodai wenzao. Wapo wanaosema kwa kutmia vipaza sauti na wapo wanaosema kwa kunong'oneza. Wapo wanaosema wazi wapo wanaotumia code words.....hapa sijaongelea wale wanaopanda majukwaani kujinadi kuwa wachaguliwe wao kwa kuwa ni wenzao na wapiga kura na wanasali pamoja....

Mliyaanzisha wenyewe ccm na sie tukawaonya hamkusikia. Mwaka huu mmelikoroga na mtazidi kupoteza kura za wasiopenda jihad Tanzania nzima
 
sikuzote maamuzi ya waislam yanaonekana udini, wakiona kofia nyingi mikutano ya cuf .. Wanasema chama cha kidini!! Anyways udini upo! Na utakuwepo.. Ni sawasawa na kusema hakuna ubaguzi wa rangi nchi za magharibi.. While in reality racism ipo,majority ya waislam wenye kuelewa mustkbal wa dini yao katika tz ya leo! Kamwe hawatopiga kura kwa slaa!!.. Ya kwangu keshaikosa!

ni kweli tuna mpigia lipumba kwasababu kikwete amna kitu, alitu ahidi mahakama yakadhi lakini ajaleta!
 
Omar ana makengeza kweli .... katika yote wewe umeona ya Askofu Ruzoka tu ..... bwa ha ha ha
Mliyaanzisha wenyewe ccm na sie tukawaonya hamkusikia. Mwaka huu mmelikoroga na mtazidi kupoteza kura za wasiopenda jihad Tanzania nzima

Sio Makengeza isipokuwa nimefundishwa ku-doubt everything.......What if I took efforts to know beyond what we were told and see??? Hivi huwezi kusema bila ya kuingiza mitizamo ya udini???
 
Omar,
Mkuu wangu Tanzania kuna Udini na unaletwa na hawa hawa watu wanaosema sema kupinga Udini hali kauli zao wenyewe zimejaa Udini. Huwezi kukosoa kosa kwa kufanya kosa hata kidogo. Udini upo na kama kweli kuna mtu anataka kuupiga vita basi asishirikiane na upande mmoja hali makosa hayo yapo pande zote. Sawa na ule msemo wa nchi zisizo fungamana na Upande wowote during cold war.

Hii ni hatari kubwa sana kwa Dr.Slaa wala tusifikirie tunampamba hapa kwani CCM mwaka huu imesimamisha wabunge zaidi ya robotatu - Wakristu, hivyo kila watu hawa wanapozidisha Udini ati watu wachague Wabunge kwa dini zao basi ni CCM pekee itakayo ibuka mshindi kwani Watanzania watashindwa kutazama tena Mapungufu ya JK na CCM ili kutazama mgombea ana dini gani..Hao wabunge wenyewe wa CCM tayari wanaanza kumkimbia JK na kujitangaza wao kama wao, leo wanakuja watu hapa na kuupika Udini pasipo kuelewa kwamba vitu hivi vimepangwa.
Weee acha tu nimesema wazi kwamba safari hii Chadema imeingiliwa tena imeingiliwa vibaya sana.
 
Sio Makengeza isipokuwa nimefundishwa ku-doubt everything.......What if I took efforts to know beyond what we were told and see??? Hivi huwezi kusema bila ya kuingiza mitizamo ya udini???

naona kama wewe ndio umeingiza udini hapo? Nimeshangazwa na one sided view uliyonayo kwenye masuala ya udini.... esp hapa JF.

All of a sudden umekuwa concerned na watu kuweka picha za vibandiko wakati ulikuwa kimya muda wote watu wakipondea ukristo na upadri wa Dr Slaa hapa jamvini.
 
Omar,
Mkuu wangu Tanzania kuna Udini na unaletwa na hawa hawa watu wanaosema sema kupinga Udini hali kauli zao wenyewe zimejaa Udini. Huwezi kukosoa kosa kwa kufanya kosa hata kidogo. Udini upo na kama kweli kuna mtu anataka kuupiga vita basi asishirikiane na upande mmoja hali makosa hayo yapo pande zote. Sawa na ule msemo wa nchi zisizo fungamana na Upande wowote during cold war.

Hii ni hatari kubwa sana kwa Dr.Slaa wala tusifikirie tunampamba hapa kwani CCM mwaka huu imesimamisha wabunge zaidi ya robotatu - Wakristu, hivyo kila watu hawa wanapozidisha Udini ati watu wachague Wabunge kwa dini zao basi ni CCM pekee itakayo ibuka mshindi kwani Watanzania watashindwa kutazama tena Mapungufu ya JK na CCM ili kutazama mgombea ana dini gani..Hao wabunge wenyewe wa CCM tayari wanaanza kumkimbia JK na kujitangaza wao kama wao, leo wanakuja watu hapa na kuupika Udini pasipo kuelewa kwamba vitu hivi vimepangwa.
Weee acha tu nimesema wazi kwamba safari hii Chadema imeingiliwa tena imeingiliwa vibaya sana.

Mkandara, wewe unapenda kucheza nice..... Lipumba alicheza nice na ccm na matokeo yake unayajua. CCM walifanya kila wanachoweza kupamba CUF ionekane chama cha kidini. Kwa vile Lipumba alichukua mkondo wa ubora, akapoteza game ya propaganda dhidi ya ccm.

CCM walianza hapa taratibu wakiwatumia watu wasomi kama Game Theory na wenzake kukipaka chadema kuwa ni chama cha kidini na kikabila. Wakati wote huo CHADEMA walikaa kimya tu wakidhani kuwa ccm wataacha, matokeo yake wote tunayajua.

CCM hawajaacha na kila siku wanazidi kuandika kwenye magazeti yao kuwa chadema ni chama cha wachaga na wakatoliki (kasome ile article ya Antari Sangari). CCM ukiwaacha tu kwenye hii game, wewe ndiye unapoteza.

Afadhali kupambana nao tu, hata kama ni kupoteza, tutapoteza tukijua kuwa tulipambana vilivyo lakini wao kwa kutumia dola na vyombo vyote vya habari wakatuzidi.
 
Mkuu wangu wala sichezi nice hata siku moja inapofikia maswala ya dini ya mtu yeyote. Na mimi sii mgeni hapa JF nakumbuka mwaka 2002 nilikuwa mbele sana kutetea Uislaam na CUF nikisema wazi kwamba CUF ni chama kinachosimamia maslahi ya Wazanzibar zaidi ya bara hivyo maadam Waislaam ndio wanajenga asilimia 99 ya visiwani kuna kila sababu watu wafikirie kwamba hicho ni chama cha Waislaam, na kuihusisha CUF na Uislaam ni upotoshaji. Nilipingwa vita sana humu JF na wengine hata kunambia ubishi wa dini siuwezi hivyo nirudi ktk siasa hali wao wakitumia dini ndani ya siasa.

Ni ukweli usiopingika kwamba Wafuasi wa CCM ndio walianza na hizi habari za CUF kuwa chama cha Kidini lakini walipata washabiki wengi sana wa Chadema hapa JF hata Mbowe alipokuja gombea uchaguzi wa mwaka 2005 ndio bao likageuka baada ya Chadema kuonekana tishio la CCM. Hivyo CCM wanatumia mbinu zao na zinafgahamika siku zote kumkoma mpinzani mbadala, lakini wewe unapojibu makombora ya CCM kwa kutumia jina la dini zetu ndipo unapokosea hata kama hao kina Malaria Sugu wanawabeza wagombea wa Chadema kwa dini zao. Dr.Slaa ni Mkristu na alikuwa Padre lakini Ukristu sio Dr. Slaa wala hawakilishi Ukristu hata kidogo.

Leo hii wewe unaweza kunibeza mimi na Uislaam utakavyo wala haitanishtua roho lakini unapohusisha Uislaam na makosa nayoyafanya mimi, hapo unakuwa umevuka daraja yaani yaonyesha wewe huna imani na Waislaam na sio mimi ati kwa sababu tu Mkandara kasema hivi na vile kuhusiana na mgombea wa Chadema.

Pengine nikufahamishe tu kwamba ktk Uislaam hakuna mbora isipokuwa yule mwenye kuabudu Mwenyezi Mungu. hakuna Sheikh wala Maalim aliye juu yako wewe ikiwa wewe unafanya ibada kamilifu hivyo Sheikh hana la kukwambia mbele ya maisha yako. Sheikh hawezi kuchagulia watu viongozi wao hata siku moja, bali anaweza kukemea mabaya sana sana atakuwa anaganga njaa. Na waislaam wanajua hilo hata kama wataimba ktk hizo vipaza sauti usiku kucha kama Sheikh Yahya na Unajimu wake ambao ni kufur.

Sheikh haweki mkate mezani kwako wala yeye hana alijualo kisiasa zaidi yako kuganga njaa. Hii sii fani yake ni mpigakura kama wewe hivyo hushawishika kama binadamu wengine na pengine yeye ni mbovu na mwenye maamuzi mabaya kuliko hata wewe na ndio maana Waislaam tunasisitizwa kufuata mafundisho na sio yale wanayoyafanya Masheikh wetu..

Kwa hiyo mnapopiga kelele hapa hali mkifikiria jinsi Ukristu ulivyoji organise na kuwapa nguvu kubwa Mapadre hata ktk masiha yenu basi mnafikiria hata Uislaam uko hivyo hivyo. Mkuu waache wasem wanaotaka kusema lakini siku ya kura ni sawa na siku ya kufa..Ndani ya sanduku la kura kila mmoja wetu atachagua chama na mgombea ampendaye na sii kiongozi wa dini au dini anayoifuata.
 
Kanda2,
Bibi Ntilie si Mwanakijiji. Hii naweza kukuapia kabisa. Hata angalia staili ya maandishi yao ni tofauti kabisa kama unajua na kuweza kusoma umetulia.
 
Kanda2,
Bibi Ntilie si Mwanakijiji. Hii naweza kukuapia kabisa. Hata angalia staili ya maandishi yao ni tofauti kabisa kama unajua na kuweza kusoma umetulia.

Yeye kila mtu hapa ni mwanakijiji. Ukiona kuzidiwa katika hoja ndio kama kawaida yake huyo. Soma maandishi yake kibao utagundua kuwa asilimia hamsini yamejaa utalebani na iliyobaki ni kuhusu mwanakijiji.
 
Mwafrika,
Mkuu wangu JF ipo siku nyingi sana walichobadilisha ni jina la kwanza tu mwanzo ikiitwa Jamboforums....Na pengione hukunisoma vizuri kwani yote niloandika ni kutolea mfano kwani naelewa fika kwamba hatujawahi kufikia hapo, ila nimesema tu kwamba wewe au mtu yeyote anaweza kunibeza mimi na Uislaam wala isinipe homa kwa sababu unanizungumzia mimi (mathlan). Useme aaah! Mkandara bana ati Muislaam mbona tunakutana Sinza kwenye Ulabu. Hapa yaonyesha unajua Uislaam unakataza kitu gani na mimi ndiye mkosefu hivyo huna maana mbaya kwa dini isipokuwa mimi na maamuzi yangu ya kunywa pombe. Lakini unapoingiza Uislaam ili kuhalalisha Pombe kwa sababu umeniona mimi na kunywa hapo ndipo huniacha hoi mwenzako..

Ndicho nachokiona hapa kijiweni, watu kuzihusisha dini na matendo ya baadhi ya watu, na mara zote huu ndio Udini wenyewe kwani unatoa hukumu ya dini kwa sababu fulani kafanya... Sasa swala la Dr.Slaa, kwa mwenye kupima anajua fika kwamba Dr, harepresent dini yeyote kisiasa hivyo kwa kila lawama anayopewa inaonyesha wazi jinsi CCM wanavyohaha lakini mtu mwingine ktk kujibu utetezi wa hoja hiyo akitumia Uislaam hali aliyesema ni Malaria Sugu na ukashindwa kumweka yeye kama msemaji bali Waislaam wote hapo ndipo napochoka miye.

Najua fika kwamba Ukristu una madhehebu mengi lakini wazo la kiongozi mmoja linaweza sana kuathiri waumini wa madhehebu yote ya Kikristu. Kwa mfano Kakobe kazungumza na tunajua yeye sii katoliki lakini amepata mapokezi ya hoja toka kwa wakristu wengi wasione ubaya wa hoja yake..halafu basi kibaya zaidi unaongelewa Uislaam kana kwamba alichosema Kakobe kinawahusu kuwatenga waislaam. Na hao Masheikh unakuta wanaibuka kutokana na tuhuma kama hizi kwani nakumbuka hata vita ya Iraq kilichotokea ni kuuhusisha Uislaam na 9/11 kiasi kwamba Waislaam wote wakatengwa kuwa na Materrorist.

Sasa unapoanzisha vita ya waislaam ukitegemea wao watakua sitting duck, hilo halipo kwao huungana na wakarudisha majibu kwa kutumia lugha ile ile ulotumia.Vita ya Iraq ilikwisha siku Marekani walipoingia Baghdad -vita ilikwisha! lakini makosa yalikuja pale vita na Saadam ilipogeuka na kuwa vita ya Waislaam. Na hili Marekani hawatakiri hata siku moja ingawa wanajua fika kwamba walifanya makosa kuita vita ile ni dhidi ya Waislaam hadi Bush alikuja rekebisha maneno yale when its too late.
 
Mkandara said:
Mwafrika,
Mkuu wangu JF ipo siku nyingi sana walichobadilisha ni jina la kwanza tu mwanzo ikiitwa Jamboforums....

Bob, hata jamboforums haikuanza kabla ya 2005 labda kama kumbu kumbu zangu sio nzuri
 
naona kama wewe ndio umeingiza udini hapo? Nimeshangazwa na one sided view uliyonayo kwenye masuala ya udini.... esp hapa JF.All of a sudden umekuwa concerned na watu kuweka picha za vibandiko wakati ulikuwa kimya muda wote watu wakipondea ukristo na upadri wa Dr Slaa hapa jamvini.

Moja, kwani Dr Slaa sio Padri? Ni wapi mimi nimewahi kuhusisha upadre wake na mapungufu yake kama mbunge ama rais mtarajiwa. Actually, If there was one thing I used to have a bit of trust na CHADEMA sio Mbowe bali ni Dr Slaa kwa kuamini kuwa background yake inamsaidia kuwa Mwadilifu. lakini wewe u always try to connect mapungufu ya Kikwete na uslamu wake.

Pili, kuna vitu vitatu vimeni-dissapoint kutoka kwa Dr Slaa.

Moja, ni kushindwa kwake kumdhibiti Mbowe anapofanya mauzauza yake...na wakati huohuo akipambana na wengine wafuate UWAJIBIKAJI.
Pili, Ni suala la kutaka kuhalalisha ama kurasimisha mahusiano yake kimwili na mke wa mtu na hii imeniumiza zaidi sio tu kwa sababu inajenga picha mbaya miongoni mwa jamii tunayolalamikia kuwa kuna muanguko wa maadili lakini zaidi ni kuwa linafanywa na mtu ambaye amekulia katika makuzi ya Upadre ambayo mimi hata kama sio mkristo llakini ninauthamini na ninauheshimu....actually sometimes I tend to have more trust to Mapadre kuliko mashehe wetu...

Tatu, ni hili la kujigamba kuwa NUSU YA USALAMA WA TAIFA WANARIPOTI KWAKE......
 
mla huliwa,tuliwaonyo sana hapa javini wakina malaria sugu,tumaini na wafuasi wao juu ya hoja zao za udini hawakutaka kutusikia sisi wenye akili,real what goes around comes around,sasa vimewashika,hakika mwaka huu mtajibeba

Na unadhani athari zake zitawakumba wao tu????
 
Mmejaa Udini mno....Dhambi hii itawatokea puani!
 
Afadhali kupambana nao tu, hata kama ni kupoteza, tutapoteza tukijua kuwa tulipambana vilivyo lakini wao kwa kutumia dola na vyombo vyote vya habari wakatuzidi.

Jifunze kupambana nao kama mimi ninavyopambana nawe...utafanikiwa
 
Moja, kwani Dr Slaa sio Padri? Ni wapi mimi nimewahi kuhusisha upadre wake na mapungufu yake kama mbunge ama mtarajiwa. Actually, If there was one thing I used to have a bit of trust na CHADEMA sio Mbowe bali ni Dr Slaa kwa kuamini kuwa background yake inamsaidia kuwa Mwadilifu. lakini wewe u always try to connect mapungufu ya Kikwete na uslamu wake.

Hukusema chochote na ulikuwa kimya tu wakati pumba kibao za kina MS na wenzake zinawekwa hapa. Nilipoanza kujibu moto kwa moto ndio watu kama wewe mnakuja na vilio kibao eti kuna mambo ya udini. Udini umeanza kuuona leo?

Kikwete hafai kwa kila kitu na hiyo si kwa sababu ni muislam ....... haya ni maneno yako mwenyewe.

Pili, kuna vitu vitatu vimeni dissapoint kutoka kwa Dr Slaa.

Moja, ni kushindwa kwake kumdhibiti Mbowe napofanya mauza uza yake...na wakati huohuo akipambana na wengine wafuate UWAJIBIKAJI.

Wewe na chuki yako dhidi ya Mbowe nani akufahamu, hujawahi kupenda chochote cha chadema kwa vile wewe ni mwana ccm damu damu.

Pili, Ni suala la kutaka kuhalalisha ama kurasimisha mahusiano yake kimwili na mke wa mtu na hii imeniumiza zaidi sio tu kwa sababu inajenga picha mbaya miongoi mwa jamii tunayolalamikia kuwa kuna muanguko wa maadili lakini zaidi ni kuwa linafanywa na mtu ambaye amekulia katika makuzi ya Upadre ambayo mimi hata kama sio mkristo llakini ninauthamini na ninauheshimu....actually sometimes I tend to have more trust to Mapadre kuliko mashehe wetu...

Yale yaleeee

Tatu, ni hili la kujigamba kuwa NUSU YA USALAMA WA TAIFA WANARIPOTI KWAKE......

Kwani ni uongo, nyeti nyingi za serikali ya ccm nani anampa Slaa kama sio hao wanausalama?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom